Wanawake this is the harsh reality

Umeongea vizuri sana sis, malezi yasibague eti huyu wa kiume asikuzwe kuwa mume bora wakati jamii inafanya kila iwezalo kuwafanya wakike kuwa wake bora. Tusitengeneze jamii ya mke kuvumilia yote huku mume anakula bata na mahawara kama wote, nah Ila tufunsishane kuwa wasikivu, heshima, utii na upendo. Pande zote zinahusika kwa asilimia zote ili kujenga nyumba bora. Japo huwa naamini sio kila mtu anafaa kuwa mke au mume, sio kila mtu anaweza kuyamudu mahusiano. Wale wasioweza basi watupishe ..teh!

Lakini reference ya wazungu, nah! Taasisi ya ndoa na malezi kwa Europeans na Americans nadhani imewashinda, sidhani(labda kwa tamaduni zao) kama wamefaulu katik kulea, ndoa ndio kabisa wameshindwa.
 
Ifike mahali km ni wa kristo basi na tufate mafundisho yaliyopo! Enyi wanawake watiini waume zenu, enyi wanaume wapendeni wake zenu. Sikuhizi hata kupendwa kwa manati, kwakweli najitahidi mno kutiii kila kitu na kuitikia kwa heshima ila UNAFIKI siwez jaman ndo unanizingua tu. Ha ha ha ha haaaaaaaaa.......salam kwa wanafamilia wote wa Mungu, amani iwe nanyi. Wanaume tunaomba Mtupendeeeeeeee jamaniiiiiii
 
Tunapoelekea, kama tutaendelea tu kubagua watoto wa kiume kwenye malezi; suala la ndoa litakuwa ni janga la kitaifa.w Siku hizi wale wanawake wa jamii itanioanje wanapungua taratibuuu. Na kwa kusema kweli, taasisi ya ndoa hata huku kwetu ni hekaheka. Ni vile tu sisi tunajali sana wazazi sijui jamii haitotuelewa; but haimaanishi kwamba sisi ndiyo tumeziweza ndoa. Wewe ni shahidi; mtu akija tu hapa akaisifia ndoa yake heheheheheheh sio kwa hayo mapovu. That tells alot hali ya ndoa za wengi wetu; ukisema una furaha na ndoa yako unaonekana kama unajimwambafy jamani mweeh
 

hapana mkuu, sijui kwa nini ila naamini kukiwa na heshima PANDE ZOTE mbili itakua ni mahusiano yenye afya na haitatokea sehemu yoyote ile utii utakua wa upande mmoja, unless uje na vivid example/scenario where mahusiano yana afya ila utii ni wa upande mmoja??!!...
 
Nimebaki neutral, sijataka kusuluhu nisioneka naegemea upande wa mmoja wapo.
Kwa yeyote aliyeku akifanya upatanisho alikuwa anaegemea upande mmoja??sio kweli!ukitaka kusulihisha hatakiwi kuegemea upande wowote.

Ila sio kesi mkuu🥂🥂🥂
 
Mke amheshimu na kumtii mume, mume ampende mke.
 
Wenye ndoa zenye furaha hawajitokezi kuanza kujisifia, siku zote mtu anayejisifia Kuna kitu anaficha, kwa tabia ya binadamu,ndoa nzuri haionekani kwa wahusika kujisifia, na wahusika huwa wako makini Sana kutokuonyesha kwa watu.

Watu wanaoweza kujua ndoa nzuri ni sadists only, Hawa ni watu waliokata tamaa na Maisha yao katika nyanja zote na hawezi kukaa na kuona wengine wanafanikiwa, hawa Wana uwezo mkubwa Sana wa kujua ndoa nzuri, waharibifu Hawa huwa wanainusa ndoa nzuri na kuanza harakati za kuibomoa.

Kwa Maisha ya Sasa ndoa nzuri ziko chache Sana, huu ndio ukweli, na hii inatokana na watu kutokuishi kwa uhalisia.

uhalisia unapatikana katika uumbaji wa Mungu na asili ya vitu na viumbe mbalimbali akiwepo mwanadamu, Rehema mbalimbali alizotupa kama vipawa, elimu mbalimbali ya mazingira yetu, viumbe mbalimbali na tabia zake za asili na vitabu vyake vya dini, vinafundisha yote haya.
 
Jamani kuna watu wana ndoa nzuri na waaongea; not necessarily kubrag ila kuna namna tu mtu anaongea unaona hapa mambo ni byee. Kuna wakati furaha inazidi unaamua tu kuongea; na wakati mwingine anaongea kuwatia moyo wengine kwamba ndoa nzuri zipo. So usigeneralise

Afu waafrika huwa tunafurahisha sana; so hata nisimuongelee mke/mume wangu vizuri kisa kuna watu watatuonea wivu wataharibu ndoa yetu. Hizi ndoa zinazotetemeshwa huku mitaani; wahusika walijisifia kwa watu? Ndo yale tukiona mtu kampost tu mke/mume tunaanza kusema "mmh hawana lolote". Tumezoea sana kusikia na kuona vitu vibaya; kiasi kwamba hata tunapoona au kusikia kizuri tunaona ni fake. Maisha hayana SI Unit.

 
Yaan nimekuelewa vizuri sana my sista, sema kuna mahali kidogo tu hujanielewa vizuri.

Hii ya kuhimiza mwanamke ina mizizi yake tangu enzi na enzi, yaan tangu huko Bibliani. Haya mnayoyasikia leo na kuyaona yamepinda khs nafasi ya mwanamke na mwanaume kwenye mahusiano ni mapokeo ya mizizi hiyo ya enzi na enzi. Ukisoma vizuri Biblia tangu agano la kale hadi jipya utaona mwanamke anavosisitizwa kuwa mtiifu kwa mumewe. Mtu mtiifu automatically anapendwa, hii iko hivo hata ktk maisha ya kawaida tu.

Sasa ukishahubiri usawa, tayari una dilute utii uliokusudiwa na Mungu. Matokeo yake kila kitu mnabaki kujiuliza why me and not him. Mbona yeye anachit jamii haimshangai, ila nikichit mimi jamii inaninyooshea vidogo. Hahaaa mna kazi kwa kweli.

Wenzetu wazungu wamefanikiwa kuachana na mapokeo haya ya dini na kuweka usawa kwenye mahusiano. Lakini usawa huo unawatesa hadi leo, mahusiano yao hayadumu hata. Ni divorce na break ups kila kuchao. Wameweka usawa hadi kwenye malezi ya watoto, matokeo yake hadi watoto wamewashinda, and many of them don't even see the need to have children. Even their population is declining now coz watu hawazai, wanaona mtoto kero tu.

Halafu maisha yao ni 50/50 ndani ya nyumba. Huku kwetu me nabeba 98% ya majukumu halafu nirudi home hata kunipet pet tu hakuna, kisa unajiuliza why asinipet pet yeye, hahaaa rudini kwenye maisha yetu asilia bana, achaneni na hizo habari za Beijing zinawapoteza
 
Mke amheshimu na kumtii mume, mume ampende mke.

imebidi ni google mkuu kuhusu utii labda nilikua sijui maana yake...

ila imekuja in english ni obedience,sasa hii ni mwanamke tu anatakiwa ku obey??? ...

Kumpenda mke, sio kumsikiliza,kumu obey (kumtii) ..???

 
Mimi sijaongelea usawa; nimeongelea kila mtu atimize wajibu wake. Fanya sehemu yako kwa 100% na mkeo afanye kwa 100%; give your all to make sure ndoa yako ipo salama. Hata sisi ni rahisi sana kumtii mtu anayetupenda; lakini mtu asiyekupenda, kumtii ni wito. Kupetiwa petiwa sawa tu; ila kuna dhambi kwani na wewe siku nyingine ukimpeti peti wife au kumfanyia kile anachokipenda yeye? Mahusiano ni give and take; sio wewe una-take tu aaah. Wote tupate raha
 
Hahaa kumbe tuko pamoja
 
imebidi ni google mkuu kuhusu utii labda nilikua sijui maana yake...

ila imekuja in english ni obedience,sasa hii ni mwanamke tu anatakiwa ku obey??? ...

Kumpenda mke, sio kumsikiliza,kumu obey (kumtii) ..???

View attachment 1609555
Katika upendo kuna yote, ila mwanamke ameambiwa amtii mume wake, naturally mwanaume anapenda kuheshimiwa, ni kama mtawala anavyopenda kuheshimiwa, so mimi nimeichukulia hapo. Sisi kuwapenda ni kuwafanyia yote yanayoambatana na upendo.
 
hongera mkuu unaonesha kujielewa
 
Hili somo la kupenda na kutii tunalirahisisha Sana, ni somo lenye content ndefu, na la mida mrefu, tafsiri na mafunzo ya kumpenda mke inahusisha majukumu mbalimbali ikihusisha yale nje ya nyumba(ya kijamii), ndani ya nyumba (ndani ya familia kama baba na kiongozi wa familia) na bedroom (kama sehemu ya kuwa mume kimwili na kihisia).

Na hivyo hivyo neno kumtii Lina majukumu yake pia. Watu wanatafsiri kwa kutumia dictionary, hapo tunakosea kwa kiwango kikubwa.
 
Hio akili haihusishi mie kuishi katika sonona lakini. Kwamba i have to endure all the troubles and chaos the woman makes to me because of her crazy hormones. Niishi miserable life kwa sababu naogopa kumtia kibao mwanamke kisa atani victimize kwa physical violence.

Hio haifanyi kazi kwangu aisee, ntakuelewesha kwa mdomo mara 2/3 ukijitia nunda nakudunda tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…