Wanawake pesa yao chungu kweli kutoa

Wanawake pesa yao chungu kweli kutoa

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,933
Reaction score
11,865
Hivi kwanini wanawake wengi pesa yao inakuwa chungu kutoa yaani ikitokea mwanaume ukamuomba mwanamke pesa yake lazima akunyime au akukopeshe wakati sisi tunawapa kiroho kisafi wakituomba, wakifungua mradi hawataki kusema wanapata faida kiasi gani?Kuna rafiki yangu kamfungulia mke wake mradi lakini mumewe wake kila akimuomba msaada hasa pale anapokwama anasema hana pesa hali mbaya.

Hivi karibuni babake jamaa yngu ameugua akamleta mjini kwa ajili ya matibabu akatumia akiba yote aliyokuwa nayo ikaisha akamwambia mwanamke amuongezee chochote alicho nacho akadai hana kitu jamaa akajipiga piga kiume tena kwa kukopa akapata pesa akakamilisha matibabu ya mzee.

Sasa cha kushangaza ni juzi ametoka kazi akakutana na list ya benki mkewe ana million 5 kwenye akaunti wakati alikuwa anadai hana kitu na huo mradi ambao umemuingizia pesa kiasi hicho jamaa ndo alimpa mtaji.Najiuliza tu ingelikuwa mwanamke ndo amekutana na jambo kama hili si angenuna mwaka mzima na matangazo mtaa mzima.
 
Msikate tamaa endeleeni tu kutupa zenu. Zetu msiziulizie mtaumwa kichwa lols
 
Ukiijua pasword yake zinatoka kiulaini tu.

Kuijua hiyo password ndiyo shughuli yenyewe!
 
Wakija watakwambia unakimbia majukumu...ngoja uone
 
Msikate tamaa endeleeni tu kutupa zenu. Zetu msiziulizie mtaumwa kichwa lols

😂😂😂😂🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🙈🙈🙈🙊🙊 Valentina 'Vale' lolest lol...!!!
 
Last edited by a moderator:
Ili kumfanya mwanaume awe ngangari

Si unaona baada ya kunyimwa kapigana (hata kwa kukopa) hadi kapata

Sasa angekuwa mjanja angemwambia mkewe "mie nimekopa...hivyo humu ndani maswala ya msosi umeme maji nk kwa miezi mitatu shughulikia wewe mie nazichanga nilipe deni"
 
😂😂😂😂🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🙈🙈🙈🙊🙊 Valentina 'Vale' lolest lol...!!!

Endeleeni kutugawia zenu buana,za kwetu zinakazi maalum
 
Last edited by a moderator:
Ili kumfanya mwanaume awe ngangari

Si unaona baada ya kunyimwa kapigana (hata kwa kukopa) hadi kapata

Sasa angekuwa mjanja angemwambia mkewe "mie nimekopa...hivyo humu ndani maswala ya msosi umeme maji nk kwa miezi mitatu shughulikia wewe mie nazichanga nilipe deni"

Sasa mkuu mpaka anaenda kukopa huruma hamna wakati mwenzake ana pesa.
 
Molembe

Watu wengine wana roho ngumu sana na ni wavumilivu,mi nikikutana na wa hivyo mbona taraka atazibebea kwenye fuso la mchanga!
 
Last edited by a moderator:
Wake wa sampuli hizo uwa mnawatoa wapi??....sio kila mwanamke anafaa kuwa mke
 
Watu wengine wana roho ngumu sana na ni wavumilivu,mi nikikutana na wa hivyo mbona taraka atazibebea kwenye fuso la mchanga!

Mkuu unaweza kuacha ukaoa mwingine yakawa yale yale.
 
Back
Top Bottom