Wanawake mna Mapepo Kama sio Laana

Wanawake mna Mapepo Kama sio Laana

Joshua Mbezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
1,934
Reaction score
4,178
Miaka miwili iliyopita nilikuwa penzini na bidada mmoja na ukweli n kwamba kipindi kile sikuwa vzr kiuchumi

Sasa huyu bidada alinidharahu na kuniona kuwa Mimi sio type yake

Aliwahi kunitamkia kuwa yupo na Mimi ila Kuna idadi kubwa ya wanaume wanamfuata kumtongoza , hii kauri ilinifanya niwaze sana moyon mwangu

Alionesha kutokunisikiliza kbc na mm nikaamua kufungasha vilago kwa style ninayoijua mm , siku Moja alinipigia simu na kuniambia kamwe nisije wahi kumtafuta kama akiwa hai labda nimtafute akiwa marehemu

Na Mimi maelekezo yake niliyapokea na kuamua kuyafanyia Kazi tangu siku hyo sikuwahi kunyanyua simu yangu kumpigia Wala kumtumia msg

Na kwa kunikomoa zaidi akaamua kwenda zake mjini Dar es salaam Mimi nikabaki zangu mkoani nikila mihogo na bamia

Akawa anajigamba kuwa anaenda kufungua biashara yake, ajenge nyumba yake na vingine vingi ,

Siku zikapita miaka ikasogea Mungu muweza wa yote akafungulia koki la baraka kichwan mwangu hela ya kununua mboga ikaanza kupatikana na uhakika wa kubadilisha nguo nikawa nao , kukatiza mitaa ya benki mara Moja Moja ikawa n uhakika

Sasa bidada sijuhi taarifa kapata wapi 😂 tangu wiki Jana akaanza kunitafuta salamu kwa Kasi , msg kibao Mimi namzoom tu😎

Siku ya kwanza amenitafuta katanguliza kauri ya kujihami alisema hivi "usidhan nimekutafuta kwa ajiri ya kukuomba hela me nakusalimia tu" na mm nikaitikia Asante

Mimi nimekusudia ndani ya moyo wangu nitaitimiza Ile kauri yake aliyoniambia kuwa nisiwahi kumtafuta akiwa hai labda nimtafute akiwa marehemu.

Dada zetu punguzeni midomo muwe na akili ya kuwaza ya kesho.
 
Sio lengo langu kuwakosea adabu wanawake wote lkn kila nikikumbuka visa na vihoja vya baadhi ya wanawake najisahau najikuta wote nimewakusanya kapu moja
 
Mimi nimekusudia ndani ya moyo wangu nitaitimiza Ile kauri yake aliyoniambia kuwa nisiwahi kumtafuta akiwa hai labda nimtafute akiwa marehemu.

Dada zetu punguzeni midomo muwe na akili ya kuwaza ya kesho.
Usimlaumu Nyoka kung'ata, maana ndio ameumbwa kung'ata, so akifanya hvyo ni anatimiza wajibu. "Midomo".

Endelea na msimamo wako huohuo, Focus na mambo ya msingi zaidi na huyo mwanamke asikupotezee muda.

Be a Man, yajue ya kuzingatia ili uachane na habari za ex wako kabisa, Mpuuze.
 
1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9...
20260612_141140.jpg
 
Kutenga muda wako adhimu na kuandika hichi ulichokiandika ambacho kinaakisi uwezo wa utendaji kazi wa akili yako......bado akili yako haijakomaa kuingia kwenye purukushani za mahusiano na watoto wa kike!!!

Ngoja ukue kwanza kiakili na kifikra then utaingia kwenye purukushani za mahusiano ukiwa umekomaa kiakili kiasi cha kujua kuwa mwanaume hapendwi mpaka uwepo wake uwe unaongoza thamani sehemu alipo
 
Usichukulie serious sana masuala ya wanawake, ndo wameumbwa hivyo mkuu.
Nilikuwa nawaanalyse sana wanawake as if wao ni malaika, ila niliposhtuka kwamba hao sio malaika ni wanadamu kidogo nilianza kubadilisha akili yangu juu ya mwanamke. Ukiwekeza nguvu kumwelewa mwanamke hutoboi.
 
Back
Top Bottom