Wanaume wengi hukosa wapenzi kwa kufanya makosa haya wanapokutana mara ya kwanza (first date)

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Umekutana na mwanamke ukapata namba yake na mkapanga mkutane mara ya kwanza mahali ili muongee/ mle/ mpate kinywaji.

Kuna muda hili jambo linatia mawazo sana. Unajiuliza utafanyaje ili umpate kabisa umuweke ndani
Kukutana na mwanamke mara ya kwanza huwa ni kwa ajili ya kujuana zaidi. Sio kwenye simu tu.

Hivyo mkijuana vizuri katika hiyo mara ya kwanza mnaweza kukiss kabisa (sio kwenye shavu) na kupeleka mambo mbele. Lakini ili ufanikiwe hadi kukiss (ikiwezekana) ni muhimu usifanye haya makosa.

Kutojiamini
Hichi ndio cha kwanza mwanamke kukupima. Mwanamke ili aendelee kuwa nawe lazima aone una ujasiri zaidi yake. Kutojiamini kunaweza kujionesha kwenye kuongea, kukaa au jinsi unavyoendesha mazungumzo na mwanamke.

Hata kama hukuamini kukutana naye, usioneshe hilo, limeze. Ukibadili wazo lako ili kufanana na lake ni kosa ataona huna msimamo.

Kutojiamini kwingine ni kunaonekana vile unavyokaa, ukikaa kwa kujikunja/ kujibana utaonekana hujiamini/ una wasi/ uzuri wake unakuendesha.

Katika mazungumzo, kutojiamini kutaonekana unaposhindwa/ kuogopa kuuliza maswali, kuwa siriazi sana, kumuachia mwanamke ayaongoze mazungumzo (hasa kumuambia tuongee unachotaka). Kushindwa kuchombeza. Na kuongea kwa wasiwasi.

Kumshawishi mwanamke kwa hela/ zawadi
Zawadi na hela ni kwa ajili ya kudumisha upendo. Unapotumia hela nyingi mwanzoni kwa ajili ya mwanamke anaona we unataka kumnunua tu huna lolote. Inaweza jionesha pale unampeleka sehemu ya gharama kwa mara ya kwanza, au kumnunulia zawadi.

Kwa mara ya kwanza haina haja ya kujitumbua sana. Lengo ni kujuana kwanza. La sivyo utawavutia wanaotaka kukutumia tu kwa hela zako. Sehemu za hela nyingi au zawadi zihifadhi kwa ajili ya kudumisha upendo.

Kutaka kumvutia mwanamke
Wanaume wengi wanajua kumtongoza mwanamke ni kujisifia vile ulivo bora. Wanajikuta wanatumia muda mwingi kumwambia kuhusu mafanikio yake na hela alizonazo. Ili mwanamke aone anamfaa na amkubalie. Lakini hiyo mbinu haina matunda mazuri zaidi ya kuvutia wanyonyaji.

Hauna haja ya kutaka kumvutia mwanamke. Kitendo cha yeye kukutana na wewe maana yake tayari amevutiwa na wewe, sasa anataka akujue wewe.

Pia kumsifia kupita kiasi ili umvutie sio vizuri. Mwanamke unaweza msifia mara moja tu, basi inatosha, sio kila muda.

Kutaka kuingia kwenye mapenzi haraka.
Wanawake wanapenda taratibu. Mwanamke akikutana na wewe mara ya kwanza ni kwa lengo la kuona mambo yataendaje. Sio kuwa mke wa mtu haraka. Au kutaka kujua kiasi gani unampenda.

Wengi wanawafungukia wanawake mapema wakihisi kwamba ndio jambo litakalomshawishi mwanamke kumpenda pia. Lakini ye atakuona una haraka. Na unampa nguvu ya kukukataa mapema. Anaweza kukuambia “mi sihitaji mpenzi kwa sasa” japo alikua anahitaji lakini umeharibu.

Pia kuongelea ngono.
Ukiongelea ngono muda mrefu mwanamke anaona we lengo lako kufanya naye ngono tu.

Kuangalia wanawake wengine
Kuangalia/ kuthaminisha wengine wakati upo naye. Kutotuliza macho kwake. Kuna mwanamke nlikutana naye mara ya kwanza, nikiwa namuangalia akaniambia “kuna mdada ana matako nyuma yako” kwa ndani yangu nkawa na hamu ya kuliona hilo “tako” lakini najua kabisa huo ni mtego.

Aone kama ntaangalia au ntaendelea kuweka nguvu zangu kwake. Anaweza akakazia macho kumwangalia mwanamke mwingine/ kumsifia ili uongie kwenye mtego wake. Ukikubali tu kuingia kwenye huo mtego, anakuona we ni mwenye tamaa. Unataka kula tunda tu na kuondoka.

Kwenda naye sehemu zisizoshawishi mazungumzo.

Kwenda kwenye muvi, kwenda kwenye makelele, kwenda sehemu mnayoonekana sana (hasa mchana). Sehemu hizi kiufupi huwezi pata muda wa kujuana, huwezi chombezana kwa amani au sehemu ambayo mwanamke anajulikana, sio nzuri. Ukimpeleka mwanamke sehemu kama hizo utakua umejilipua mwenyewe.

Lengo kuu la kukutana mara ya kwanza ni kujuana zaidi, kujuana kama mtaendana. Ukishakutana naye hiyo mara ya kwanza usimuombe mwanamke kukutana naye siku nyingine, kwanini? Sababu ni heri urudi nyumbani ujiulize kwanza je, mnaendana? Je, unamtaka kujenga naye maisha. Kisha ndo uamue kukutana naye tena au la.
 
Mbona huu mjadala tulishaufunga..MANENO KIDOGO PESA MINGIIII.
 
Back
Top Bottom