Kuweka Mipaka na Wazazi kwa Vijana

Shining Light

JF-Expert Member
Jan 8, 2024
214
288
Ninafahamu kuwa kila familia ina utamaduni wake na maoni yake kuhusu jukumu la watoto kwa wazazi wao. Hata hivyo, binafsi ninaamini kuwa wazazi wanabidi wajue kuwa sio rahisi kuwahudumia, au kuhudumia familia nzima hasa pale unapojikuta hali yako ya Uchumi ni tete, au ajira imekuwa changamoto kubwa sana.

Wazazi huwa wana tabia ya kufananisha wewe na mtoto wa fulani hivyo huweza sababisha hali ya kwanini, wivu na kufanyiana visa na watu katika maisha yanayo kuzunguka. Pia inaweza leta msongo wa mawazo ukahisi kuwa umeshafeli maisha.

Nina imani kuwa kuheshimu wazazi wako haimaanishi kufanya kila wanachosema unapaswa kufanya. Wazazi wako wanapaswa kuelewa kuwa wewe ni mtu mzima na una haki ya kufanya maamuzi yako. Una majukumu pia yako na malengo yako na haipaswi kuwa kila lengo lako liwahusishe na wao.

Hivyo sio makosa kuweka mipaka na wazazi wako kujua kitu gani unaweza kufanya na kipi huwezi kufanya, Ila pia nafahamu wazazi wanaweza "guilty-play" ili uweze jisikia vibaya katika kuwasaidia katika mambo mbalimbali.
 
Back
Top Bottom