Wanaume walio ndoani na "holiday ukweni"

Wanaume walio ndoani na "holiday ukweni"

Happy 2018!!

Nina swali dogo lakini laweza kuwa muhimu, hasa kwa jamaa zangu wa kiumeni waliopo ndoani. Fikiria ni holiday time, wale ndugu zangu wenye desturi ya kurejea kwao/kwa wazazi wanajiandaa kwenda kufurahi na ndugu, marafiki na majirani.

Wakati huo mke anakwambia "hubby naomba likizo/sikukuu hii tuitumie kwa wazazi wangu", tuseme kuanzia tar. 20 Dec hadi tar. 7 Jan. Nawe mwanaume unakubali kwa sababu ni ukweli kuwa wazazi wa mke ni wazazi wako pia.

Swali langu hapa;
*Je utaweza kukaa kwa wakwe kuanzia 20th hadi 7th?

*Ni sahihi (kwa mtizamo wako) kukaa kwa wakwe kwa mda mrefu kama wiki na zaidi?

*Mila zetu zinasemaje kuhusu mwanaume 'kupiga kambi' ukweni?

Again, happy 2018 MMU family.
Kwa Mariooooooooooooooz, no problems. Ila wa Shababi, that cant happen. Ita upoteza uhuru, ujasiri na power ya Mume ni Kichwa cha familia. Kama ni dharura sawa, just foa single emergency day. Vinginevyo, ni mwendo wa hotel.
 
Unaweza kwenda kwa mama smart na kukaa zaidi ya wiki mbili?
Kwa mwanamke 2 weeks ukweni kidogo ina mashiko but kwa mwanaume mhmh haikuji asee!
Na ndomana wanaume wengi huwapeleka wake zao ukweni but for certain reasons!

All in all Kukaa muda mreeeeefu iwe ke au me sio kabisa

Cc Smart911
 
Nimeamua kujenga nyumba kwenye mji anaotoka mke wangu ili kukwepa hili suala la kulala ukweni ,ikifika jioni naaga zangu kiroho safi naenda kulamba bia town na kulala kwangu wife namuacha kwao
 
Nimeamua kujenga nyumba kwenye mji anaotoka mke wangu ili kukwepa hili suala la kulala ukweni ,ikifika jioni naaga zangu kiroho safi naenda kulamba bia town na kulala kwangu wife namuacha kwao
Safi sana mkuu, ukiwa na uwezo wa kujenga ni vizuri zaidi, ila usijenge kiwanja cha wakwe[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Happy 2018!!

Nina swali dogo lakini laweza kuwa muhimu, hasa kwa jamaa zangu wa kiumeni waliopo ndoani. Fikiria ni holiday time, wale ndugu zangu wenye desturi ya kurejea kwao/kwa wazazi wanajiandaa kwenda kufurahi na ndugu, marafiki na majirani.

Wakati huo mke anakwambia "hubby naomba likizo/sikukuu hii tuitumie kwa wazazi wangu", tuseme kuanzia tar. 20 Dec hadi tar. 7 Jan. Nawe mwanaume unakubali kwa sababu ni ukweli kuwa wazazi wa mke ni wazazi wako pia.

Swali langu hapa;
*Je utaweza kukaa kwa wakwe kuanzia 20th hadi 7th?

*Ni sahihi (kwa mtizamo wako) kukaa kwa wakwe kwa mda mrefu kama wiki na zaidi?

*Mila zetu zinasemaje kuhusu mwanaume 'kupiga kambi' ukweni?

Again, happy 2018 MMU family.

Kwa mila za kwetu:
1: hurusiwi kulala ukweni au kukaa hadi zaidi ya saa Sita :usiku
2: Ikidhibitika ume jamba ukweni Faini ni mbuzi
3:Ukivua viatu soksi zikatoa harufu faini Laki.
4:Marufuku kukopa ukweni.
 
Wenye maadili hayo niwachache sana - wengine wanaiga tu sababu kama kweli una maadili ya kiafrika kama Babu zetu waliotangulia mbona kutwa kucha kwenye mitandao kuperuzi picha za ngono na kungonoka kila mara kama sio unafki kijifanya maadili yamekujaaa!!!,Hawa ndio wanajifanya wemaa makalioni wanatembea na TUNGURI, Nyakati zinabadilika kama hukubali sikulazimishi pyeeeeeeeeeee[emoji40][emoji40]
 
Safi sana mkuu, ukiwa na uwezo wa kujenga ni vizuri zaidi, ila usijenge kiwanja cha wakwe[emoji16][emoji16][emoji16]
hilo ni kosa kubwa sana mkuu ,ni mbali kabsa na siendi kila siku napitisha hata siku tatu ndo naenda tena kuwasalimia ,raha ya ukweni uwe na jeuri jeuri flani kwa mbali ,kama hawakuelewi elewi hivi
 
Mm ukweni kukaa mwisho siku mbili,
Ukae zaidi ya week unatafuta nn mwanaume mzima kuangaliana pua na wakwe, mwishoe dharau zianze
Mwanamke ndo akae kwa wazaz wangu hata miez!!
 
Ukiacha maigizo, uhalisia ukweni ikilazimu sana iku 1 tu! Kule unaenda unasalimia unarudi.
Utaamkaje asubuhi umefunga taulo kiunoni banaa!
Umeona eeh!! Wewe ndio unajua maana ya likizo. Likizo shuuurti ujiachie, kwa nafasi😉
 
Niliwahi kwenda ukweni ila nilikaa siku tatu niliona kama nimekaa miaka mi3, na hapo sikuwa nalala ukweni na pia hivyo hivyo siwezi mpeleka mke wangu kwetu nikamuweka zaidi ya siku moja...labda kuwe na dharula....kwanza siwezi kwenda kukaa kwa mtu zaidi ya siku tatu...siwezi aisee....
 
yaani nitaenda leo, nashinda kesho, keshokutwa asubuhi nduki. namwacha wife aongee na mama na watoto wacheze na bibi yao over
 
Mada fikirishi sana hii. Mimi nina miaka 16 ya ndoa na sijawahi kulala ukweni hata kwa siku moja. Sijawahi kukatazwa ila naamini sitakuwa na amani... Japo ukweni kuna chumba cha kulala wageni ... mimi huwa nalala lodge ya karibu.

Asubuhi nawahi kifungua kunywa... napiga stori kidogo then nasepa kitaa... mchana nakuja kugonga lunch na story nyingi then nasepa. Usiku nakuja kugonga dinner.... story nyingi sana then naenda zangu lodge kulala.... wife analala kwao. (Angalizo sitafuti mchepuko)

Maximum kukaa ukweni ni siku tatu kama kuna msiba wa karibu sana. Kusalimia.... nikifika leo keshokutwa mapema sana kabla jogoo hajawika mi huyoooo nshasepa zangu. Wife tutakutana mbele ya safari au jijini Daslam

Mpaka sasa sijajua kwanini....
Hongereni ...wakuu nyie mmebahatika kuoa kwenye familia ziishio mijini!! Sisi wengine wakwe zetu wako bush lazma tulale make hakuna jinsi...!
Mi ni mwanamke Niko kwa ndoa zaidi ya miaka 15 huwa tunautaratibu wa kwenda holiday Xmas kwa mama mkwe Na New year kwetu ila si Mara zote new year Mme wangu anakuja kwetu. Tukiendq nae huwa tunalala hotel iliyo karibu Na kwetu ila watoto tunawaacha kwa bibi Na babu halafu pia wale waliooa Dada zangu Na pia kaka Na mabinamu zangu ndio wakati wetu muafaka wa kukutana Na watoto wetu kujuana so Mara nyingi tunakula kwa wazazi au ndugu wengine Na pia kula bata na San Na kulala ni hotelini.
 
Mimi sijaweka utaratibu wowote kwa mama mkwe. Mama mkwe huwa hapendi vijana wake na wake zao walale nae in the same roof. So we mletee wajukuu nyie mtafute pa kulala. Nikienda mwenyewe Na watt ananiruhusu kulala kwake.
Nimempenda buure! Mambo mengine hayahitaji mila, unajiongeza tu. Sasa yule shemeji yako mkubwa keshaoa kwani jamani. Huyu mama mkwe wako atanifaa sana😀
 
Back
Top Bottom