mbongo_halisi
JF-Expert Member
- Apr 16, 2010
- 7,757
- 6,290
Happy 2018!!
Nina swali dogo lakini laweza kuwa muhimu, hasa kwa jamaa zangu wa kiumeni waliopo ndoani. Fikiria ni holiday time, wale ndugu zangu wenye desturi ya kurejea kwao/kwa wazazi wanajiandaa kwenda kufurahi na ndugu, marafiki na majirani.
Wakati huo mke anakwambia "hubby naomba likizo/sikukuu hii tuitumie kwa wazazi wangu", tuseme kuanzia tar. 20 Dec hadi tar. 7 Jan. Nawe mwanaume unakubali kwa sababu ni ukweli kuwa wazazi wa mke ni wazazi wako pia.
Swali langu hapa;
*Je utaweza kukaa kwa wakwe kuanzia 20th hadi 7th?
*Ni sahihi (kwa mtizamo wako) kukaa kwa wakwe kwa mda mrefu kama wiki na zaidi?
*Mila zetu zinasemaje kuhusu mwanaume 'kupiga kambi' ukweni?
Again, happy 2018 MMU family.
Kiualisia, tatizo hapa hakuna. Ila ukioa wale jamaa zetu wapenda sensa unaweza patwa na hasira au hata kujiua kama una DNA ya Kihehe. Ukiwa ukweni kwa jamaa zetu hawa wa sensa (wa kuhesabiwa) kubali kutumiwa kama mtumwa, maana watakuja ndugu wa hajabu hajabu hata mkeo hawajuwi toka azaliwe na kudai kuwa wewe ni shemeji yao na hawakutambui, hivyo uwanunulie pipa la mbege na mbuzi mzima wa kuchoma ili utambulishwe. Mbege hiyo itakuwa inauzwa ama kununuliwa kwa ndugu wa mkeo na mbuzi hivyo hivyo. Kama pipa la mbege ni shilling 20,000, ghafla utaambiwa pipa ni shilling 100,000 na mbuzi hivyo hivyo. Na hii inaweza ikakutokea kila siku maana hawa jamaa ni waharibifu sana wa uchumi wa mtu. Kwa hiyo kama unakusudia kukaa huko uhesabiwe na wewe, basi jihesabie kula hasara za mamilioni huku wewe mwenyewe ukiambulia machungu ya moyo na majuto ya kuoa huko.