Mimi nimeoa mnyiramba, ase nikienda kule nakaribishwa kama nfalime
Mama mkwe hudeki chumba mwenyewe siku ya kwanza
Ananyunyizia urashii
Mwendo wa kula kuku tu
Ila Sasa misumari kutoka kwa mashemeji na wajomba Ni shida
Mama mkwe hajawahi kuniomba pesa direct huwa anaomba kupitia wife ananiheshim sana
Wajomba na mashemeji wa kinyramba Ni pasua kichwa
Wanafika saa mbili asubuh kuja kusalimia, wananisubiria nakunywa Chai naoga afu wanasema twende tukakutenbeze
Wananpitisha kwa ndugu moja then break ya pili utasikia shem makoo yanawasha tukajipooze kwanza buana
Nawapenda sana so charming Sema vyuma vimekaza
Siku unasepa unapewa kuku, mahind, mlenda wa kukausha, nk
Ukisikia Mayo ujue upo kwa wanyiramba