Happy 2018!!
Nina swali dogo lakini laweza kuwa muhimu, hasa kwa jamaa zangu wa kiumeni waliopo ndoani. Fikiria ni holiday time, wale ndugu zangu wenye desturi ya kurejea kwao/kwa wazazi wanajiandaa kwenda kufurahi na ndugu, marafiki na majirani.
Wakati huo mke anakwambia "hubby naomba likizo/sikukuu hii tuitumie kwa wazazi wangu", tuseme kuanzia tar. 20 Dec hadi tar. 7 Jan. Nawe mwanaume unakubali kwa sababu ni ukweli kuwa wazazi wa mke ni wazazi wako pia.
Swali langu hapa;
*Je utaweza kukaa kwa wakwe kuanzia 20th hadi 7th?
*Ni sahihi (kwa mtizamo wako) kukaa kwa wakwe kwa mda mrefu kama wiki na zaidi?
*Mila zetu zinasemaje kuhusu mwanaume 'kupiga kambi' ukweni?
Again, happy 2018 MMU family.