Wanaume walio ndoani na "holiday ukweni"

Wanaume walio ndoani na "holiday ukweni"

ERoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
54,708
Reaction score
127,624
Happy 2018!!

Nina swali dogo lakini laweza kuwa muhimu, hasa kwa jamaa zangu wa kiumeni waliopo ndoani. Fikiria ni holiday time, wale ndugu zangu wenye desturi ya kurejea kwao/kwa wazazi wanajiandaa kwenda kufurahi na ndugu, marafiki na majirani.

Wakati huo mke anakwambia "hubby naomba likizo/sikukuu hii tuitumie kwa wazazi wangu", tuseme kuanzia tar. 20 Dec hadi tar. 7 Jan. Nawe mwanaume unakubali kwa sababu ni ukweli kuwa wazazi wa mke ni wazazi wako pia.

Swali langu hapa;
*Je utaweza kukaa kwa wakwe kuanzia 20th hadi 7th?

*Ni sahihi (kwa mtizamo wako) kukaa kwa wakwe kwa mda mrefu kama wiki na zaidi?

*Mila zetu zinasemaje kuhusu mwanaume 'kupiga kambi' ukweni?

Again, happy 2018 MMU family.
 
Kimsingi hamna tatizo lolote kama nyie wenyewe mmekubaliana na pia ni jambo jema sababu mtaimarisha bond ya mahusiano ya familia zenu na inakuwa nzuri zaidi kama mtafanya hizo visiting kwa zamu zamu, mwaka huu kwao, mwakani kwenu n.k

Binafsi naona hamna ubaya sababu hata litakapotokea tatizo kama msiba n.k lazima uende na huwezi kukwepa kulala ukweni
 
Wakwe ni wa kwenda kuwasalimia tu, siku moja au 2 kisha unatembea mbele. Unakuta dume zima limepiga kambi kwa wakwe wiki mbili eti anakula sikukuu.

Wanaume wengi wa hivyo unakuta mke ndie boss, anakua hana namna. Unakuta hata nyumba wanayoishi walipewa zawadi na wakwe, jamaa lazima awe mpole tu.

Yaani nina kwangu alafu nikakae kwa wakwe wiki 2 eti nakhla sikukuu?
 
Kuna kaugumu fulani hivi, sie tukienda home tunashinda kwa mama ila kulala tunaenda kwa dada, hata mi sijui kwanini.
Umeita wanaume sorry nmekuja kumuwakilisha mwamaume wangu .
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]eve wewe
 
Why not? Ushaasema ""holiday". Wakwe ni wazazi kwa mke wako na kwako kama wa kwako walivyo kwako na kwa mkeo. Hapo kwenye "mila zetu" fafanua maana kila kabila lina mila zake. Kwa jamii yangu ya kimachame wakioana wamachame kwa wamachame wanajua mila inasema mwanaume hawezi kulala kwa wazazi wa mwanamke na hata mwanamke hawezi kulala kwa wazazi wake hata kama kuna msiba. Kama wameoana wenyewe kwa wenyewe ina maana wana miji yao hivyo hakutatokea haja ya mwanaume kulala kwa wakwe. Lakini mila zinasemaje kuhusu kuoa chasaka au mnyika? Makabila yote duniani yangependa watoto wao wasioe au kuolewa na kabila lingine lakini kwa wengi imeshindikana. Kwa hiyo mnyaturu akioa mchaga kuna siku tu atalala ukweni. Si ajabu wala hakuna ubaya.
 
Sidhani kama kukaa ukweli kwa siku zote hzo ni jambo zuri. Ukweni ni sehemu ya kukaa siku moja mbili ya tatu unaondoka. Imagine wazazi wanapata picha gani pale unapowatakia usiku mwema? wanajua daaah!! jamaa linaenda kumuumiza binti yetu. si picha nzuri kwakweli. Tusikae sana ukweni
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] we jamaa wewe
Ila cyo lazima ku do kila cku
 
Mada fikirishi sana hii. Mimi nina miaka 16 ya ndoa na sijawahi kulala ukweni hata kwa siku moja. Sijawahi kukatazwa ila naamini sitakuwa na amani... Japo ukweni kuna chumba cha kulala wageni ... mimi huwa nalala lodge ya karibu.

Asubuhi nawahi kifungua kunywa... napiga stori kidogo then nasepa kitaa... mchana nakuja kugonga lunch na story nyingi then nasepa. Usiku nakuja kugonga dinner.... story nyingi sana then naenda zangu lodge kulala.... wife analala kwao. (Angalizo sitafuti mchepuko)

Maximum kukaa ukweni ni siku tatu kama kuna msiba wa karibu sana. Kusalimia.... nikifika leo keshokutwa mapema sana kabla jogoo hajawika mi huyoooo nshasepa zangu. Wife tutakutana mbele ya safari au jijini Daslam

Mpaka sasa sijajua kwanini....
 
Mkuu Asprin sasa huo ndio utaraatibu mzuri kaka. Na tunatakiwa tuwafundishe vijana wetu hawa silka na tamaduni kama hizi.
 
Mada fikirishi sana hii. Mimi nina miaka 16 ya ndoa na sijawahi kulala ukweni hata kwa siku moja. Sijawahi kukatazwa ila naamini sitakuwa na amani... Japo ukweni kuna chumba cha kulala wageni ... mimi huwa nalala lodge ya karibu.

Asubuhi nawahi kifungua kunywa... napiga stori kidogo then nasepa kitaa... mchana nakuja kugonga lunch na story nyingi then nasepa. Usiku nakuja kugonga dinner.... story nyingi sana then naenda zangu lodge kulala.... wife analala kwao. (Angalizo sitafuti mchepuko)

Maximum kukaa ukweni ni siku tatu kama kuna msiba wa karibu sana. Kusalimia.... nikifika leo keshokutwa mapema sana kabla jogoo hajawika mi huyoooo nshasepa zangu. Wife tutakutana mbele ya safari au jijini Daslam

Mpaka sasa sijajua kwanini....
Hata mm hua najiuliza ni kwa nini inakua ngumu kulala ukweni ingawa sioni tatizo..
 
Kama hamna tatizo au sherehe siwezi kwenda ukweni zaidi ys siku 1 na sijawahi kulala ukweni nashangaa sana ndugu zangu waliooa migombani wanavyoenda Xmas na mwaka mpya ukweni! Kuna wanaume wanastahili viboko
 
Mi ni mwanamke Niko kwa ndoa zaidi ya miaka 15 huwa tunautaratibu wa kwenda holiday Xmas kwa mama mkwe Na New year kwetu ila si Mara zote new year Mme wangu anakuja kwetu. Tukiendq nae huwa tunalala hotel iliyo karibu Na kwetu ila watoto tunawaacha kwa bibi Na babu halafu pia wale waliooa Dada zangu Na pia kaka Na mabinamu zangu ndio wakati wetu muafaka wa kukutana Na watoto wetu kujuana so Mara nyingi tunakula kwa wazazi au ndugu wengine Na pia kula bata na San Na kulala ni hotelini.
 
Back
Top Bottom