Wanaume walio ndoani na "holiday ukweni"

Wanaume walio ndoani na "holiday ukweni"

kama huna ela ukikaa ukweni kazi za kukata kuni, kuchota maji na kusaga Mahind kwa ajili ya sembe la ugali zinakua ni zako hivyo ni bora kujiandaa kisaikolojia pia
 
Mwanaume unalala ukweni kwani umeolewa huko?

Labda kama hukupeleka posa na mahari ndio utajilaza kwa wakwezo...
 
Kuna kaugumu fulani hivi, sie tukienda home tunashinda kwa mama ila kulala tunaenda kwa dada, hata mi sijui kwanini.
Umeita wanaume sorry nmekuja kumuwakilisha mwanaume wangu .
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Sijui kama nimejichanganya. "why not" nilimaanisha kwa nini wasikae? Kwa kabila langu nimesema kama mkwe ni chasaka anakaa ukweni na hakuna wa kumshangaa. Muda mrefu sijui ni upi maana wewe umetaja wiki au zaidi. Kama wameamua "holiday" ni wiki moja au mwezi hakuna shida maadam hana lengo la kuhamia ukweni.
CHASAKA!! mchaga wewe!
 
labda mila za mtoa mada ndo haziruhusu. Mila za kwetu unaweza kuishi hata mwaka mzima kama muda wako unaruhusu. Wale ni wazazi wako kama walivyo wazazi waliokuzaa. Tena mara nyingi wakwe wanawapenda sana wakwe zao kuliko hata binti yao wakati mwingine. Mimi nikienda likizo huwa tunaanzia kwa wakwe, tunachinjiwa kuku siku ya kwanza kupasha. siku ya pili wanachinja Mbuzi, tukimaliza kumla kama siku mbili tatu hivi tunachinjiwa tena kuku. hapo ni siku si chini ya siku saba tunakuwepo kwao. Then tunahama mji kwenda kwetu kwa idadi ya siku kama tulivyoka kwa wakwe. Mtindo ni huo huo wa kula kuku na mbuzi hadi watoto wanaanza kugoma kurudi mjini. Inabidi wadanganywe kuwa wanatusindikiza sisi then wao watarudi kwa bibi na babu. ni full raha. kama hupendi kukaa kwa wakwe zako basi una matatizo binafsi. wale ni wazazi wenu wewe na mke wako.
 
Alilala siku mbili ila sasa alikuwa kama yuko jela khaaah!!!
Ni nyingi mno, nimeshindwa kabisa kulala. I just wanted others' experience asee.
 
Ni nyingi mno, nimeshindwa kabisa kulala. I just wanted others' experience asee.
Kwa wanaume hii naona ni ngumu mnoo kwao, yaani unamuona tu mtu anavyopata shida, ila ni vile tu hamna namna.
 
Back
Top Bottom