Wanaume wa JF mnaweza kufanya hivi?

Wanaume wa JF mnaweza kufanya hivi?

Mnaacha kabisa shughuri zenu mko bize kuchungulia nyumba za watu, kuna binadamu waajabu mkimaliza kufanya umbeya mnalalamika maisha magumu wakati kutwa pua zenu mumezitegesha nyumba za watu.
 
Habarini wanaJF.

Niende kwenye mada bila kuchelewesha muda, ni hivi kuna jirani yangu ambaye kabla ya kuolewa na mume aliye naye alikuwa tayari amezaa mtoto anayeitwa Mary na bwana mwingine.

Jana baba yake Mary akaja nyumbani kwa mzazi mwenzie kumuona mwanae.
Mume wa ndoa wa huyu mama alikuwepo home, pia mama Mary alikuwepo.
Mama Mary na mumewe wa ndoa walimpokea kwa bashaha Baba Mary.
Walikaa pamoja, yaani mume wa Mama Mary wa sasa ambaye wamefunga ndoa, Huyo mzazi mwenzie mama Mary ambaye ndie baba Mary halisi, Mary mwenyewe na Mama Mary walikuwa wanaongea na kucheka kwa furaha.

Baadaye mgeni wao (mzazi mwenzie mama Mary) aliaga na wote kwa pamoja akiwemo mume wa ndoa wa mama Mary walimsindikiza na kuagana kwa furaha.

Majirani wambeya wambeya tulikuwa tunachungulia tu na kufurahia amani iliyokuwa imetawala eneo lile na hasa kuona jinsi mume wa ndoa wa huyu mama alivyokuwa hana wivu, ni MNYAKYUSA na mama Mary ni Mzaramo, Baba Mary halisi ni Msukuma

Nawasilisha
Ikitokea unajua mwanamke alizaa na mtu mwingine na wewe ukamuoa na ukalea mtoto mzazi wake akija hakuna shida kwangu mimi,ila aje nyumbani kwangu sio amuite kwake yeye waende na motto,hata hyo jirani yako lingemshinda!
 
Mnaacha kabisa shughuri zenu mko bize kuchungulia nyumba za watu, kuna binadamu waajabu mkimaliza kufanya umbeya mnalalamika maisha magumu wakati kutwa pua zenu mumezitegesha nyumba za watu.
misstrace, humu duniani tuko mchanganyiko, uko wewe mstaarabu,niko mie hapa shambenga basi yaani ni mchanyato wa kila tabia
 
Ikitokea unajua mwanamke alizaa na mtu mwingine na wewe ukamuoa na ukalea mtoto mzazi wake akija hakuna shida kwangu mimi,ila aje nyumbani kwangu sio amuite kwake yeye waende na motto,hata hyo jirani yako lingemshinda!
alaaa kumbe!
 
Hakuna tatizo hapo, hiyo inaonesha ukomavu wa akili, upendo na heshima kwa wote. Lazima tukubali historia zilizopita za wapenzi/wana ndoa wenzetu. Sio kila jambo ni la kutilia mashaka ili mradi kila mmoja ana nia njema.

Ila sikuona sababu ya wewe kutaja makabila ya wahusika. Tukio unalolielezea halina uhusiano na makabila yao. Laweza kutoa kwa mtu wa kabila lolote au lisitokee.
waungwana bwana,bado asingemsindikiza ndio wangesema kabisa kuwa Mama Marry na mtaliki wake wamekumbushia enzi zao
 
Makabila yao ya Kinyakyusa, Kizaramo na Kisukuma yaliweza kutengeneza ' Chemistry ' nzuri ya ' amani ' sasa kwa moyo wako huo huo wa ' ufukunyuku ' Mkuu hebu tusaidie kuangaza angaza huko na kule tukio kama hilo la Watu wenye makabila ya Kikurya, Kimasai na Wahehe ili tujue kama na wao hii ' Chemistry ' yao italeta ' ushirikiano ' wa kutukuka.
Assignment uliyonipa nitaifanyia kazi!!!
 
Ushasema mtangulizi msukuma, ataachaje kufurahi japo kinafiki!!
 
Au mwende kwa mkemia mkuu wa serikali hahahahaahahhahahah

Kwa mkemia mnaenda kuhakiki matokeo ya taste.

Yaani kama ile testing ya taste ilitengeneza kiumbe ndo mnaenda kuhakiki kama kweli matokeo hayo ni ya ile test.
 
Back
Top Bottom