Ukiishia kufanya vitu ili upendwe unadharaulika

Ukiishia kufanya vitu ili upendwe unadharaulika

Matunzo 02

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2026
Posts
1,186
Reaction score
2,268
Huruma siyo malezi
1.unamlea mtoto au wew ndo unaendeshwa na mtoto? Unamlea siyo kwa misingi ya dunia unafanya vitu ili upendwe na mtoto mwisho wa siku anakudharau hata kama nikifanya hivi baba/mama hawezi kunifanya chochote.

2.mtoto anajilea mwenyewe kama kila analofanya kwako ni safi tu akitukana safi tu dunia ina misingi yake huwezi kupaa kama ww sio ndege, ety uruke juu usiludi chini?

3.mara zote anapendwa mzazi mwenye misimamo ambaye hataki ujinga hata asipopendwa ataheshimika.
Kumbuka heshima = upendo

4.sina maana tuwe watu wabaya kwa watoto wetu bali tuwafunze kuishi kwa maadili mema ya utu
Wahenga walimaliza ASIYEFUNZWA NA MAMAYE HUFUNZWA NA ULIMWENGU.
 
WAhenga walishajua kuwa Gen Z wengu watalelewa na ma single mama ndio maana wakasema Asiyefunzwa na mamaye
 
3.mara zote anapendwa mzazi mwenye misimamo ambaye hataki ujinga hata asipopendwa ataheshimika.
Kumbuka heshima = upendo
Lakini misimamo iendane na utoaji wa huduma Maana wengine ni kuweka Tu hata Unga robo ni mtihani
 
Mzazi bora ni yule anayemfunza mtoto wake kukosa na kupata
 
Back
Top Bottom