Wanaume wa JF mnaweza kufanya hivi?

Wanaume wa JF mnaweza kufanya hivi?

Habarini wanaJF.

Niende kwenye mada bila kuchelewesha muda, ni hivi kuna jirani yangu ambaye kabla ya kuolewa na mume aliye naye alikuwa tayari amezaa mtoto anayeitwa Mary na bwana mwingine.

Jana baba yake Mary akaja nyumbani kwa mzazi mwenzie kumuona mwanae.
Mume wa ndoa wa huyu mama alikuwepo home, pia mama Mary alikuwepo.
Mama Mary na mumewe wa ndoa walimpokea kwa bashaha Baba Mary.
Walikaa pamoja, yaani mume wa Mama Mary wa sasa ambaye wamefunga ndoa, Huyo mzazi mwenzie mama Mary ambaye ndie baba Mary halisi, Mary mwenyewe na Mama Mary walikuwa wanaongea na kucheka kwa furaha.

Baadaye mgeni wao (mzazi mwenzie mama Mary) aliaga na wote kwa pamoja akiwemo mume wa ndoa wa mama Mary walimsindikiza na kuagana kwa furaha.

Majirani wambeya wambeya tulikuwa tunachungulia tu na kufurahia amani iliyokuwa imetawala eneo lile na hasa kuona jinsi mume wa ndoa wa huyu mama alivyokuwa hana wivu, ni MNYAKYUSA na mama Mary ni Mzaramo, Baba Mary halisi ni Msukuma

Nawasilisha
Inashindikana nini??ulitaka wapigane au warushiane matusi????[emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] amani na upendo ndo cha msingi sikuhizi
 
Mwenye mali kwa sasa anajiamini anajua mavi ya zamani hayanuki mwanamke wa kweli anaejua thamani yake harudii matapishi
 
Back
Top Bottom