Vi rendra
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 3,320
- 5,748
Nmekua ila siyaoni
Labda kwakua naogopa ugomvi
Labda kwakua naogopa ugomvi
Kuwa utayaona
Kuwa utayaona
Basi hongera sana Mungu aendelee kukupa moyo huo maana tunayokutana nayo mungu mwenyewe anajuaNmekua ila siyaoni
Labda kwakua naogopa ugomvi
Poleni sanaBasi hongera sana Mungu aendelee kukupa moyo huo maana tunayokutana nayo mungu mwenyewe anajua
Mwanaume anapigwa na mwanamke mpaka anazimia??? Huyo mwanamke au shoga??
Wanawake wafupi naona ndio wanaongoza kwa ukorofi. Nimeshuhudia hiliNi leo asubuhi nimetoka kugombana na mrembo wangu. Kaniambia anajiskia anaumwa tumbo na miguu anajiandaa kwenda hospitali. Nikamuuliza una pesa, akanijibu ndiyo ninayo Tsh16000; nikamuuliza hiyo pesa inatoshakwenda hospitali? Ni hospitali gani inatibu kwa hiyo pesa? Hilo likawa kosa akawa mkali, eti dharau sipendi! Nikamuuliza dharau zinatoka wapi tena kuuliza ni dharau? Akawa mkali tena, eti kuuliza gani huko. Duh nikamwambia basi nenda huko hospitali ila hiyo pesa haitoshi. Tukamaliza kwa style hiyo, lakini nikawa najiuliza kwa nini wanawake wengi ni wagomvi wanapenda sana maisha ya purukushani na ubabe ubabe hasa wale wanawake wafupi wana matatizo sana.
Hizo si hasira zakawaida bali wehu uliochanganyika ujinga ndani mwakeKabisa we unadhani hasira gani hizo mpaka mtu anachana makochi anavunja tv we bado uko nae tu kesho c atakuchoma kisu!?!?
Haaaaaa duuh hao wanaume au wavulana? Cjui Kama kweli mwanaume kbsa unapigwa mpaka usaidiwe au unaumia haswa duuuuhNakumbuka visa Vingi lakini hizi Ndio vilikuwa too much.
1.jirani zetu,
Wote wanyakyusa lakini mwanaume alikuwa anapigwa mpaka anatoka nje kuomba pooh na msaada. Yaani anatoka nje baada ya kujaribu kuzichapa ndani,akiona amezidiwa na anavuja damu kabisa anatoka nje kuomba msaada,wanazichapa mpaka mwanaume anatoka nje yuko uchi kabisa wa mnyama. Tuliamulia mpaka tukachoka wakawa wanaokoa polisi jamii,mpaka mwenye nyumba akawapa notice na mtaani wakatimuliwa Maana mjumbe alisha wachoka na kesi zao kila siku.
2.Shangazi yangu
Ni mkorofi typically,Yaani yeye bila ugomvi kwa siku hajalala vizuri aisee. Anazichapaga na mume wake mpaka mwanaume anazimia. Kuna siku wakawekwa kikao na ndugu wa mume,sasa vile walivyokuwa wanamsema na mume wake akachangia maeno machafu sana,aisee alinyanyuka akaanza kutembeza kichapo kwa mumewe,akakimbilia ndani akamfuata huko huko alipiga mpaka mwanaume akawa anavuta pumzi kama anakufa hivi lakini bado anaendelea kupiga. Baba Ndio alikuwa ana wasili eneo la tukio,alikata nyaya akamgusisha nazo alipigwa na shoti Ndio akaacha.
3. Rafiki yangu,
Alikuwa mtata jamani sijawahi kuona wala Ku image,mzuri na ana msambwanda kama basi la Kilimanjaro. Ilikuwa akianza kuzichapa na bwana ake,mpaka wanakatana nyembe na kushikiana visu,full ngeu kila siku. Siku moja akatuita Mimi na Marafiki zetu wengine wa4,tumsindikize ubungo. Alawasha gari yake tukaingia sisi haoooo to ubungo. Alivyofika akapark,akaenda kugonga nyumbani Fulani wakati Huo na sisi tunashuka. Yule msichana aliyefungua,alivutwa kama mwizi. akaanza kumpa kipondo,alipiga,mwanamke anapigana kama john cena. Akaja kaka wa yule binti,akaingilia ugomvi. Rafiki etu akarudi kwenye gari,kwenye buto alitoa nondo na nyundo,ule ugomvi uliamuliwa na wanajeshi. Maana ilikuwa anapiga watu wawili na anawachakaza.
Nilivunja urafiki nae days ahead,nikawa simpokelei simu wala sijibu Sms zake.
4. Cousin wangu,
Ameolewa toka mwaka 2014. Around 2016 mume wake akawa anachepuka,lakini she is decent and hakuwa anamfuatilia. Na Hata alipo ambiwa mumeo huko Hapo somewhere na mchepuko hakuwahi kumfatiliza.
There is a day yule bwana akajichanganya,akamwambia cousin "Yaani wewe malaya umenichosha,bora ningeoa mama ako" ile siku ni alimpiga sitaki Kukumbuka ni alipiga kwa kiasi gani,akapiga tu simu nyumbani akasema jamani nimeua huku. Tulivyoenda jamaa hajitambui,alikaa ICU mwezi mmoja. Cousin nae akawekwa ndani na ndugu wa mume wake,sababu wakwe walivyofika Wifi mmoja akaleta jeuri aKampa kipigo akachanika mdomo na jicho wakaenda polisi. Mume wake alivyoamka akasema namtaka mke wangu,good thing mpaka Leo wapo pamoja,mwanaume alijua makosa yake,yakaisha. Wakafuta kesi polisi.
dah mkuu huyu bado upo naye mpaka leo?Usiombe!...
Hapa ninapoandika hii text nimehamia chumba kingine na kutandika godora chini.....(Nalala huko).Ni HATARI..Huyu wangu ni hatari...Yeye akishachukia...hubomoa Milango,kuvunja TV,kuchana masofa....
YAANI...Bora wasio oa...hii ndoa yangu ni ngumu mno....
Na ukitaka kukusanya mtaa mzima uwe unajibizana naye....So me nimechagua kuto kujibizana naye na kuhamia room nyingine....
Kabla ya kuoa msio oa....
Waangalieni Vizuri wadada
Hahahaa huu uzi umenichekesha sana nimejikuta nausoma wote aisee
Inawezekana kabisaMie namuona mwanaume. Kama shoga basi ni siri yake na anaembandua
Ila mkasa wako ndo umeniacha hoi mkuu pole jamani hahahaaa naamini sasa una amani teleHuu uzi naukumbuka sana,tulianza na 2017..du maisha bn!
Ana tatizo huyoKabisa we unadhani hasira gani hizo mpaka mtu anachana makochi anavunja tv we bado uko nae tu kesho c atakuchoma kisu!?!?
[emoji847]Mmachame wangu ni hatarii ila amenipata! Akimwaga ugari namwaga maharage ya nazi. Uwa napiga za chembe usiku unasikia anakuletea simu ongea na mama. Akinipa nasikia msamehe mwenzio! Mamaye!
Mkuu una roho ngumu sana!Niliwahi kumchumbia mdada mmoja hivi. Tulipoendelea kwa mda nikaona ananizoea kwa haraka sana. Akawa ananifuatilia nyendo zangu zote. Baadae ikafika mahali ni km vile hataki nisalimiane na mwanamke yeyote, nikaona ni mpuuzi sana. Nikamtosa kiaina, akawa hataki, nikamweleza wazi sikutaki! Akaliaa. Kumbe alichukua uamuzi aende kwetu aeleze habari ya uchumba wetu, eti tatizo mi sieleweki kwa haraka... Nashangaa naitwa nyumbani nikaelezwa habar ile huku wakikauka kucheka. Nilipatwa na hasira sana, kwa bahati nzuri jioni ya siku hiyo alikuja geto kwangu, nilipandisha hasira nikachukua kisu nikamfukuza. Ikawa ndo mwisho wake kunifuata fuata
[emoji16][emoji16]Nastahili tu kupewa tuzo ya mwaka ya uvumilivu.
Nastahili kutunikiwa nishani ya jeshi maana depo nimemalizia nyimbani.
Huyu mwanamke ni mkorofi na kisirani wa kutosha. Ila 31-12-2018 nakuacha mama rasmi nenda kamtese na mwingine.