Wanaume, tupeni majibu hapa...

Wanaume, tupeni majibu hapa...

teh teh teh...nimekusoma. Kumbe ndo maana mzee wangu alisema mwanamke akisema we kaa kimya maana atakuwa amepata ushindi....sasa siwezi nifanyaje

Hiyo ndo best policy,ila akizidi chukua hatua.........
 
na kama moshi unavyoumiza macho ndani ya chumba cha jiko ndivyo ilivyo kuish na mwanaume mkorofi ndani ya nyumba.

mwanamke ukitaka ufurahie noa yako,wewe mtii mume wako tu basi,hata zawadi zitakuwa za kufikia tu.ila tu na mwanaume anatakiwa ampende mke wake.
 
Labda nikuulize: wanawake wanapo kataa kukiri ni kwanini?
Uliweka assumption yako ya mwanzo vibaya: ungesema watu
Maana hii tabia ipo kote kote, kwa wanawake kama wanaume

yaelekea uzi wangu uliopita juu ya wanawake kwenye hii mada ulikupita but tuliongea na kila mtu akaweka sababu na tukaonyeshana njia nzuri ya kuomba na kukiri kosa.
 
Hahahaha...kwanza umeishamjibu gfsonwin kwanini ni mgumu wa kuomba msamaha

Mzushi tu gfsonwin,anauliza majibu bana amekuwa kama kova anayeuliza wapi pa kumpata aliyemtia mkong'oto kaka Uli.
 
Last edited by a moderator:
Kabisa kabisa ,wanawake wanaongea jamani,ukimkoroga leo akianza ku rap atakumbushia na hata ulivyomkonyeza matron siku ya harusi,tukio la miaka arobaini iliyopita,kha!

Bishanga umenichekesha mbavu sina....wakijua kuumudu mdomo suala la kusema sorry mbona dogo sana
 
yaelekea uzi wangu uliopita juu ya wanawake kwenye hii mada ulikupita but tuliongea na kila mtu akaweka sababu na tukaonyeshana njia nzuri ya kuomba na kukiri kosa.
Kweli sikuona... sorry about that.
Hata hivo, nadhani the premices were wrong,
na ndio maana unawaona wanabisha sana.
 
mwanamke ukitaka ufurahie noa yako,wewe mtii mume wako tu basi,hata zawadi zitakuwa za kufikia tu.ila tu na mwanaume anatakiwa ampende mke wake.

so kwenye upendo hakuna kuomba samahani ila kwenye kuheshimu ndo kunakuomba msamaha? mbona jamani ule uzi wa namna bora ya mwanamke kuomba msamaha mlitupa mawazo hapa hamtak kujisema? mbona sisi tuliyaongea mapungufu yetu wazi wazi?
 
Mzushi tu gfsonwin,anauliza majibu bana amekuwa kama kova anayeuliza wapi pa kumpata aliyemtia mkong'oto kaka Uli.

bishanga uzushi wangu ni upi tena? kuuliza haya? FYI nilitaka niandike kama jinsi ambavyo niliuandika ule wa namna bora ya mwanamke kukiri na kuomba msamaha lkn nikasema hapana hapa ntumie busara hii manake itakuwa kama shetani kaingaia mbinguni nikaja kwa stail tofauti kabisa lakin bado mnakuwa wagumu kweli wanaume miaka 2000 tena ndo tutaanza kuwaweza.
 
Kabisa kabisa ,wanawake wanaongea jamani,ukimkoroga leo akianza ku rap atakumbushia na hata ulivyomkonyeza matron siku ya harusi,tukio la miaka arobaini iliyopita,kha!

Yaani hapa umenimaliza mbavu zangu.
hii inaukweli fulani ndani yake. wanawake tumezidi mdomo jamani.
mimi nimejitahidi sana kulimit mdomo wangu, na inanisaidia sana, but still nitahitaji kuombwa samaha pale ninapokosewa
 
Kweli sikuona... sorry about that.
Hata hivo, nadhani the premices were wrong,
na ndio maana unawaona wanabisha sana.

hebu iweke basi katika perspective nzuri zaid ili watoe wajibu?
 
lakini Blaine mwanamke akiomba samahan siyo dhaifu?
(according to malezi) udhaifu sio sifa ya uanaume so hatutakiwi kuwa nayo. kuhusu mwanamke udhaifu inakubalika maana wao wapo chini yetu (according to malezi)
 
gfsonwin sio wote kwa maneno yako ambao huwa hawaombi samahani
Kuna mazingira ambayo kabisa unajiona umeenda mchomo na hukupaswa kusema au kutenda na unaomba msamaha kwa mwenzako
yaweza isiwe ni yale maneno ya moja kwa moja kuwa samahani dear nimefanya kosa ila vitendo vingine vinaashiria kumuomba samahani
Sio kwamba dhana ya ubabe au kuwa mwanaume ndio ikifanye uwe na roho ngumu kung'ang'ania kitu ambacho kabis unajua ni kosa
 
Last edited by a moderator:
bishanga uzushi wangu ni upi tena? kuuliza haya? FYI nilitaka niandike kama jinsi ambavyo niliuandika ule wa namna bora ya mwanamke kukiri na kuomba msamaha lkn nikasema hapana hapa ntumie busara hii manake itakuwa kama shetani kaingaia mbinguni nikaja kwa stail tofauti kabisa lakin bado mnakuwa wagumu kweli wanaume miaka 2000 tena ndo tutaanza kuwaweza.

Achika nikuoe uone utakavyostarehe.
 
Back
Top Bottom