Wanaume, tupeni majibu hapa...

Wanaume, tupeni majibu hapa...

umekuzwa vzr sana.
ila wewe wenzio hawakushanga ama mkeo hakushangai kuskia kwamba unamwomba msamaha??

Kwani nini cha ajabu hapa mama nanihii?Msamaha hauna jinsi......kusema huu ni msamaha wa kike na huu ni wa kiume hiyo kitu hakuna. Masamaha ni UNISEX. Mimi huwa siogopi, naomba halafu nabaki na amani yangu ya kutosha.

kwani nini cha ajabu hapa mama nanihii?msamaha hauna jinsi......kusema huu ni msamaha wa kike na huu ni wa kiume hiyo kitu hakuna. Masamaha ni unisex. Mimi huwa siogopi, naomba halafu nabaki na amani yangu ya kutosha.

barikiwa sana mkuu.msalimie sana thando
 
Binafsi niko kwenye mahusiano na mara nimkoseapo mwenzangu huwa nakiri na kuomba toba bila shuruti.
Tofauti na nitegemeavyo,mwenzangu hunifanyia makusudi kisa nimekiri basi huwa inakuwa sababu ya kila jambo ufanyalo tofauti na matakwa yake kukusema siku nzima.Siku hizi,nakiri ila namkazia ili asinipelekeshe siku nzima.Tunatofautiana.
 
Mimi binafsi namkosea wife mara kibao, sasa ningekuwa nakubali makosa yote si angeshaniacha? Aidha natafuta namna ya kujustify au nakataa katakata kuwa sijafanya. Mara chache tu naweza admit halafu nikamwomba msamaha. Tungekuwa tunaomba msamaha tungeomba mara ngapi? Mfumo dume umetuharibu, sio kosa letu. Believe me, makosa tunafanya na mademu zetu tunawapenda sana sana!!!
 
hapo bold unamaanisha mtu huyo huyo ama?
 
Binafsi niko kwenye mahusiano na mara nimkoseapo mwenzangu huwa nakiri na kuomba toba bila shuruti.
Tofauti na nitegemeavyo,mwenzangu hunifanyia makusudi kisa nimekiri basi huwa inakuwa sababu ya kila jambo ufanyalo tofauti na matakwa yake kukusema siku nzima.Siku hizi,nakiri ila namkazia ili asinipelekeshe siku nzima.Tunatofautiana.
mkuu Mayunga6, huo ni udhaifu wa baadhi ya wanawake ambao wao msamaha hautoki moyoni. ukimuona mtu anasema nimekusamehe lkn sitakusahu ujue haja samehe kabisa. samahani huwa haihesabu mabaya wala gharama wala haiangalii wakati.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo wanawake wengi ukiwaambia ukwel ndo umeharibu ndoa yako, bora udanganye coz hawapend kuambiwa ukweli.

Kinachoharibu ndoa hapo ni ukweli au ni madhambi yako uliyofanya??

We endelea kudanganya lakin za mwongo ni 5 lol.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hivi kwanini wenzetu nyie si wepesi hata kidogo wa kukiri makosa yenu na kuomba msamaha? Kwanini mara nyingi huwa mnatafuta means ya kujusfty makosa kuliko kuomba msamaha? je ni ubabe ama ni aibu ama mnahisi kufanya hivyo ni kujishusha hadhi yani kutoka kuwa mwanaume na kuwa mtu mwingine?

je na kwa wale mnaokiri na kuwaangukia wake zenu kwa samahani, je wake zenu wamewahi kubadili heshima yenu ama hata kukudharau?

leo akina mama tukae tuwatupie maswali kwa kila hoja watakazo leta hadi tujue nini ni nini.

nawasilisha.

moja ya laana ya mungu kwa hawa pale eden ni kuwa "mmeo atakutawala"
watawala daima huwa hawa apologies hata wanapokosea ila uweza kusahihisha kosa lake kwa njia nyingine iwapo atagundua....

hii inatoka kwenye theory za utawala za dunia, waliosoma hiyo wanajua

hivyo mungu aliweka utawala ndani ya mwanaume...ndio maana imedumu hadi leo, mwanaume hawez, (ni vigumu) kwenda miguun kwa mwanamke kirahisi kujishusha, labda ndo penzi liwe jipyaaaa...
akisha nanii hii mara tatu tu, baaaasi
atushikiki tena, (equally) na watawala. kuna mbunge aliwai salimia shikamoo wote mkutanon, wakati wa kampeni.
mugombea wa urahisi apishwi barabara akiwa ajawa rais..lkn akiupata wote mnapaki pemben wakati anapita...(kiburi cha utawala)

mungu alimpa utawala mwanamme juu yenu

naomba kuwakilisha.
 
Ni wazito wa kuomba msamaha sababu sisi ni wepesi, tunakuwa lege lege sana, kakosa yeye msamaha unaomba wewe. Ukishamjengea mtu wako mazingira hayo usitegemee atakosea na akiri kosa!
Wanawake wa kulia lia, unyenyekevu usio na maana wabadilike sasa

God have mercy on me!
I see nitaishi maisha magumu all my life......
 
Teh! Teh ! nimependa hii ya "Afadhali kuishi kwenye paa la nyumba kuliko kuishi na mwanamke mgomvi" by the way huwa tunaomba msamaha hata kwa kupiga magoti tatizo nyie mna "vidomodomo" tukiwaomba msamaha namna hiyo kesho hiyo habari utaikuta "Dar eS salaam stock of exchange (soko la hisa na mitaji la Dar) " inauzwa mpaka mtaani unaona kinyaa!
 
Hivi kwanini wenzetu nyie si wepesi hata kidogo wa kukiri makosa yenu na kuomba msamaha? Kwanini mara nyingi huwa mnatafuta means ya kujusfty makosa kuliko kuomba msamaha? je ni ubabe ama ni aibu ama mnahisi kufanya hivyo ni kujishusha hadhi yani kutoka kuwa mwanaume na kuwa mtu mwingine?

je na kwa wale mnaokiri na kuwaangukia wake zenu kwa samahani, je wake zenu wamewahi kubadili heshima yenu ama hata kukudharau?

leo akina mama tukae tuwatupie maswali kwa kila hoja watakazo leta hadi tujue nini ni nini.

nawasilisha.
gfsonwin nilikuwa sijaona haka kauzi!
Dah hata mimi sijajua ni kwanini ila ukweli ni kwamba kukiri kosa kwa mwanaume ni nadra sana labda kwa wasio magentleman wa ukweli lol
Unajua tatizo ni la kwenu....ni kikiri kosa hilo kosa ndio litakuwa mfano wa kila siku...utasikia eeeeh si umezoea kwenda kwa mwaJ nenda tu makelele kibaaaao ndo maana ni bora usijue lolote hata uniue sikiri kosa sababu ya midomo yenu mirefu kama pua ya Rejao
Mtu inatakiwa nikikiri kosa usiendelee kulikumbuka ila kwenu inakuwa ndio mfano kila siku na utaliobeba hadi mtaa wa pili
Heheheee I will never admit the mistake unless nimewekwa kwenye kachupa!
 
Last edited by a moderator:
Kwa mnaopenda kunukuu maandiko out of its context, kwa Wakristo Biblia inasema "Enyi waume wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda Kanisa" Je, YESU KRISTO alilipendaje Kanisa? Alijitoa kwa ajili yake akalinunua kwa damu yake.. na analipenda upeo mpaka sasa kwa Upendo wa AGAPE (Unconditional LOVE)!! Kwa hiyo wanaume wenzangu malezi yetu tuliyolelewa (MFUMO DUME) tusipokuja kuya subject kwa NENO la Mungu (For Christians here) Ndoa zetu zitakuwa na MIGOGORO isiyokwisha...Kumbukeni hawa wanawake wetu wasomi wa sasa hivi ni TOFAUTI na wale wa zamani wa NDIYO MZEE tukitaka kuwa treat the same way our old parents used to treat them... NDOA KWISHNEY... au dada zangu mnasemaje... thi nimethema ukweli jamani!!!!
 
gfsonwin nilikuwa sijaona haka kauzi!
Dah hata mimi sijajua ni kwanini ila ukweli ni kwamba kukiri kosa kwa mwanaume ni nadra sana labda kwa wasio magentleman wa ukweli lol
Unajua tatizo ni la kwenu....ni kikiri kosa hilo kosa ndio litakuwa mfano wa kila siku...utasikia eeeeh si umezoea kwenda kwa mwaJ nenda tu makelele kibaaaao ndo maana ni bora usijue lolote hata uniue sikiri kosa sababu ya midomo yenu mirefu kama pua ya Rejao
Mtu inatakiwa nikikiri kosa usiendelee kulikumbuka ila kwenu inakuwa ndio mfano kila siku na utaliobeba hadi mtaa wa pili
Heheheee I will never admit the mistake unless nimewekwa kwenye kachupa!

hahahah! nashindwa kuamini niichokisoma hapa.
ukiona unashindwa mdomo na mkeo jua unatatizo na uanaume wako. inakuwaje mkeo aweze kuwa na mdomo mchafu mbele za mumewe??

mwanaume lazima uwe wa kiume na unapokoasea kuaonayesha u-anaume wako unasema naimekosea nisamehe huku ukimaaanisha kwamba huhitaj huruma bali unahitaj hak aya msamaha. na ikisemwa nimesamehe ujue kwamba hakuna neno litakalo toka zaid ya hapo kwan hutakuwa makaosa bali utakuwa unatafutwa ugomvi.
 
mie nadhani inategeana na ubashiri wa mwanaume juu ya mwitikio wa mkewe baada ya kukiri kosa. kama anahisi hatasamehewa kwa urahisi ni vigumu kukiri. lakini pia namna baadhi ya wanawake wanavyowasilisha kesi kwa kuhukumu kabla ya kusoma shitaka inapelekea kutokiri kosa.
 
Kukiri kosa ni udhaifu wa namna yake! Bora kujenga mazingira ya kujitetea na inapotokea ukabanwa sana bora useme "BASI YAISHE MPENZI WANGU; KAMA NIMEKUKOSEA NISAMEHE"

Neno kama linauzito mkubwa katika kubadili sentensi nzima.
 
mie nadhani inategeana na ubashiri wa mwanaume juu ya mwitikio wa mkewe baada ya kukiri kosa. kama anahisi hatasamehewa kwa urahisi ni vigumu kukiri. lakini pia namna baadhi ya wanawake wanavyowasilisha kesi kwa kuhukumu kabla ya kusoma shitaka inapelekea kutokiri kosa.

safi sana!
 
Hivi kwanini wenzetu nyie si wepesi hata kidogo wa kukiri makosa yenu na kuomba msamaha? Kwanini mara nyingi huwa mnatafuta means ya kujusfty makosa kuliko kuomba msamaha? je ni ubabe ama ni aibu ama mnahisi kufanya hivyo ni kujishusha hadhi yani kutoka kuwa mwanaume na kuwa mtu mwingine?

je na kwa wale mnaokiri na kuwaangukia wake zenu kwa samahani, je wake zenu wamewahi kubadili heshima yenu ama hata kukudharau?

leo akina mama tukae tuwatupie maswali kwa kila hoja watakazo leta hadi tujue nini ni nini.

nawasilisha.

Dawa ni kuwa kama huyu bi mkubwa hapo pembeni ya muzee..unyonge pembeni kuanzia sasa..mama kaonyesha njia sahihi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom