Miss Natafuta
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 26,581
- 48,737
Inatokea binti ana rafiki wa kiume rafiki mzuri tu hata muda mwingine anakutongoza ila labda upo unamchunguza kama anafaa au vipi. Ikatokea siku ukakwama kifedha kama rafiki ukamuomba akukopeshe na rohoni mwako unajua kabisa utalipa
Kutoka hapo hata kukutongoza naaacha hata urafiki hataki tena kama huna sema huna sio unakimbia . Kwani ni lazima?
Naomba kuuliza wanaume ina maana kila mwanamke ni mchunaji? Ni kosa wewe kumsaidia rafiki wa kike? Kwani hatukwami sisi? hatuitaji msaada? Mbona mnakwama?? Nyie mbona mnakopa?
Kuna wanawake wengine mpaka akuombe hela kwanza ujue amekuheshimu sana na ukitoa ujue heshima yako inaongezeka mara dufu.
Tabia ya mwanamke hutoijua kwa kukuomba elf 20,au 30 ya kusukia . Anaweza asikuombe kumbe ndani ni mbwa mwitu. Mahusiano mangapi ya watoto wa kishua yapo vibaya? si wana hela wale hawana shida yoyote, Je hawasumbui? Mbona nao wanashindikana?
Kaka zangu rafiki yako akikuomba hela mara ya kwanza kama unayo wewe mpe tu kiroho safi . Usimjudge mtu kwa mambo ya dunia yasiyo na thamani utakuja kupishana na malaika mlangoni kwako kisa hela umkaribishe shetani kisa kuweka akiba isiyo na mlaji