Baadhi yetu wanaume tuna roho mbaya Sana

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,577
18,901
Habari zenu members

Nina rafiki yangu ana mke mmoja. Hii ndoa imekuwa na misukosuko kutokana na tabia ya rafiki yangu kumpiga mkewe karibia Kila wiki pamoja na kupenda michepuko lakini pia rafiki yangu amekuwa haachi matumizi badala yake inaenda kwa michepuko

Nakumbuka siku moja mkewe alinifuata Mimi Kama rafiki wa mumewe na kutaka niongee naye alinieleza mambo yote anayokutana nayo kwenye ndoa yake na kuniomba nimsaidie Jambo moja.

Tutengeneze Jambo la uongo Mimi nijifanye daktari halafu yeye amekuja hospital kwetu akiwa na mimba yenye miezi minne bahati mbaya ionekane mimba yake imeharibika na amekuja bila hela yoyote alafu akaniambia mumewe akituma hela atanitoa 50k ikiwa tayali alishafoji cheti Cha kliniki kinaonesha ana mimba .

Kiukwel ilikuwa ngumu kukubali kirahisi kwasababu sikuwahi kufanya Jambo Kama hili hapo kabla lakini kutokana na mapito anayopitia ninayoiona na mengine alivyonieleza nikabidi nimfanyie hili jambo

Tulifanikiwa na chakushangaza matibabu yote tuliitaji laki 3 lakini rafiki yangu alimtumia mkwewe laki 5 ni zaidi ya kile kiasi ambacho mkwewe alichoomba.

Ikabidi anipe 50k baada ya kazi alioniomba kuisha ila me nilimwambia asinipe ujue hakuna mtu asiyependa hela lakini sometime utangulize huruma na utu na usipende Sana hela mbele kwenye Kila Jambo ingawa nilikuwa Nina shida na hela ila matatizo aliyonayo huyu dada ni makubwa Sana so why nikaona nisichue hiyo hela.

Ingawa nilikuwa najua mchepuko wa rafiki yangu sikuweza kumwambia mkewe ila nilichofanya ni kumsaidia ndoa yao isitetereke.

Me binafsi ninajiuliza kiukwel mke wa rafiki yangu ni mzuri Sana kuliko hata mchepuko wa rafiki yangu na ni mwanamke anajitambua lakini pia anampenda Sana rafiki yangu kwa changamoto anayopitia ni wanawake wachache sana wanaweza kuvumilia unajiuliza kitu gani unakikosa kwa mkwewe mpaka uwende kwa michepuko?

Me nilichofanya nikabidi nichukue number ya mchepuko wa rafiki yangu na kweli nikafanikiwa sura ninaijua ila number ndo nilikuwa Sina nikampigia yule mchepuko wa rafiki yangu na tukapanga tukutane na tuliweza kukutana na nikabidi nimwambie ukweli kwamba rafiki yangu ana mke kitu ambacho niligundua hajui na nikamweleza yote.

Na ni kweli baada ya muda mfupi rafiki yangu akaachwa na yule mchepuko lakini pia sikuishia hapo nikabidi nikae na rafiki yangu pamoja na mkewe ili ni tatua tatizo la na kweli mazungumzo yaliendelea vizuri na kiasi Fulani yalimsaidia kumbadilisha tabia rafiki yangu.

NB: Wanaume hebu tujitahidi tuache tabia ya kupiga wake vibaya au kusahau kutimiza majukumu yetu Kama wanaume.
 
Ndoa INA mambo mengi sana mda mwingine kuelemewa na hisia za mapenzi kwa mchepuko inachangia sana haya pia kukengeuka pia na mengine mengi hongera kwa kuaaidia jahazi kutokuzama
Asante mkuu.
 
Huyo uliemtolea mfano mbona hana roho mbaya?. Mkewe kaomba laki 3 yeye kamtumia laki 5. Huo ni upendo kwa mke pia ni mfano mzuri wa kuigwa kwa sisi tunaotarajia kuoa
 
Unabahati sana hayo mambo huwa yanaingiliwa na wazazi na viongozi wa dini kiukweli mimi nisingevumilia kuwa na rafiki kama wewe
 
Huyo uliemtolea mfano mbona hana roho mbaya?. Mkewe kaomba laki 3 yeye kamtumia laki 5. Huo ni upendo kwa mke pia ni mfano mzuri wa kuigwa kwa sisi tunaotarajia kuoa
Kiufupi huyu jamaa sio mtu mwenye kutoa matumizi ya nyumbani ila mpaka mkewe atengeneze techinique ya uongo la tatizo ndo anatoa hela ila hiv hiv kutoa ni ngumu lakini pia anatabia ya kumpiga mkewe Sana sometime bila hata kosa Kuna kipindi alimpiga mkewe mpaka akavimba uso wote na kumchana na kiwembe kwenye paja lake na ukiachana na Hilo aliwahi kumfungia mkewe kwenye Banda la mbwa siku nzima.
 
kumpiga mwanamke haifai na ni kosa baya sana......ila wewe sio rafiki wa kweli.......
 
unaingilia mambo ya ndani... na kuna siku atajua....urafiki untaishia hapo........
ukwel unaweza kukuumiza lakini ukawa tiba baade na rafiki wa kweli ni yule anakuwepusha na mambo yasiofaa hata Kama njia anayotumia inaweza kukukwaza kuliko rafiki anayelea mambo yakijinga ya kwako.
 
Kiufupi huyu jamaa sio mtu mwenye kutoa matumizi ya nyumbani ila mpaka mkewe atengeneze techinique ya uongo la tatizo ndo anatoa hela ila hiv hiv kutoa ni ngumu lakini pia anatabia ya kumpiga mkewe Sana sometime bila hata kosa Kuna kipindi alimpiga mkewe mpaka akavimba uso wote na kumchana na kiwembe kwenye paja lake na ukiachana na Hilo aliwahi kumfungia mkewe kwenye Banda la mbwa siku nzima.

Huyo rafiki yako atakuwa na ukichaa
 
Back
Top Bottom