[QYAANI FIXED POINY UMEONGEA POINT,SIJUI NIKUPE ZAWADI,HEBU CHAGUA ZAWADIUOTE=Fixed Point;7288571]But all in all......
maisha ya watu wengi sana yakiharibika huwa tunaonewa sana wamama......
kuna kipindi pia huwa naingiaga huu mkenge, kuwa sisi ndo tunapaswa kushika control ya maisha ya familia zetu.
familia nyingi ambazo mama ana vision ya maendeleo huwa inafika mbali sana..... hata kama huyo mama hana kipato kikubwa.
Kuna watu wengi sana wa karibu nami ambao walikuwa na kipato kikubwa sana lakini wameishia kuwa na maisha mabaya sana sababu wake zao walikuwa hawaangalii sana future ya familia, wao ni kuvaa, kula, kunywa........ ananunua vitu vingine havina hata maana, sababu tu mume ana hela......
lakini pia kuna familia ambazo unaona kabisa hawana uwezo kiviiileeee, lakini mama kila siku anafanya juu chini angalau tu future ya familia iwe nzuri.
Naelewa kabisa kuna wababa ambao hawashauriki, hasa na wake zao. lakini mke ana uwezo wa kujua kabisa kuwa mume anapenda sana kusikiliza ushauri wa nani, anaweza kumtumia huyo mtu.
Kuna familia ambayo tunaichukulia kama wazazi wetu. ni watu wazima saana, wastaafu. lakini huyo mume anatusikiliza sana, kila tunachomshauri. Mke wake akitaka kufanya kitu chochote ambacho anajua mumewe ana uwezo nacho huwa anatuomba sisi tumshauri, ni kweli tukiongea naye tu anatoa hela faster, hata kama mkewe alishambishia saaana.
Huwa najifunza mambo mengi sana kwa kuwa karibu sana na watu wazima, haya maisha siyo kama tunavyoyaona kwa nje, kuna mengi yaliyojificha ndani ya nyumba.
usikute mzee wa watu (huyu tunayemjadili) hakuwa na starehe kihiiivyooooo, je alikuwa na mke mshauri?[/QUOTE]