faraja ya moyo
Member
- Apr 20, 2022
- 23
- 31
Umejibu vyema mkuu, niongezee tu hapo kuwa huyo mwanamke ana mahusiano gani na huyo mwanaume, kuna uhusiano wa kirafiki au ushkaji tu, na uhusiano wa mapenzi, sasa kumuomba mwanaume ambaye ni rafiki wa kawaida haina shida, lakini kama ni mpenzi hilo ni tatizo kubwa na linawakatisha wanaume wengu tamaa, ukweli ni kwamba wanaume wengi wanachukia tabia ya kuombwa ombwa hela na wanawake, inabore, kingine pia inategemea huyo anayeombwa hela urafiki/ uhusiano wenu una muda gani, sa unakuta mtu mmefahamiana tu wiki moja unaanza kumuomba hela, lazima ashtuke, maoni yangu hapa ni kwamba wanawake tuache hii tabia ya kuomba omba hela wanaume, tujitaidi kutafuta za kwetu, lakuni tatizo lingine tusiwe na matarajio sana ya kupata pesa kwa mwanaume unapomuomba, naye pia wakati mwingine anakosa, so kwa hili tujerekebishe, lakini kwa upande wa kiumeni, kama hauwezi kumsaidia mtu ni bora uache but sio kumsaidia kwa conditions, unless labda kama kalazimisha mwenyewe, ni bora umwambie sina kuliko umpe hela umuharibie utu na thamani yake.Kuomba wala sio tatizo ila tatizo liko hapa kama ulikuwa ni muombaji alafu ukamuomba mwanaume ukiwa unatatizo serious mwanaume lazima akushushe thamani na wala usihesabie huo ni upendo ataona nitabia yako ya upigaji vizinga lakini kama ulikuwa sio muombaji ikatokea ukawa una shida serious hiyo hamna shida hata mwanaume anaweza akakupa bure hata bila masharti na atachulia tatizo lako kiuzito sasa mtoa mada yupo kwenye kundi lipi nilizongumzia
Nashengena
Rosemary 255
Championship
Krait
Rebeca 83
mzabzab
