🤣🤣😂 Ila kupitia huu Uzi wanawake tushushe kiranga cha 50/50, tuelewe kuna Haki Sawa na mfanano wa Haki......mfano Kama kuna watu wawili mmoja ana umri wa miaka 40, mwingine ana miaka 2 na wote Wana njaa, ukiwapa Kwa Haki Sawa utawapa wote mtori nusu bakuli au wali kilo moja moja....hapo umezungumzia Haki Sawa ambapo either mmoja atapunjika au atafaidi zaidi.
Lakini kwenye mfanano wa Haki kila mtu atapata anachostahili, wa mtori ale mtori wa wali ale wali.
So wanawake wenzangu, we can't beat nature, tulilie mfanano wa Haki, nature inataka tuhudumiwe, tuna Haki ya kuhudumiwa....Ila Haki huambatana na wajibu, ni wajibu wetu kuwa submissive Kwa hawa wanaume watafutaji.....ukiambiwa njoo uifate getto nendaaaa😂😂😂😂 tena Nenda Kwa adabu, toa yoteee!🤸🏿♀️
Tena muulize Kama anataka tena, hakuna mwanaume mgumu Kwa mwanamke mnyenyekevu.
Shida tunajifanya ngangari, tunahubiri 50/50 huku pesa zao tunazitaka😂