Wanaume mmeyafanya mapenzi kuwa biashara

Wanaume mmeyafanya mapenzi kuwa biashara

roselyn2

Member
Joined
Jun 7, 2022
Posts
86
Reaction score
390
Labda ni kwa vile sikulifahamu hili kwa undani zaidi, ndio maana nikajikuta naumiza moyo wangu tu.

Kwa mwanaume wa sasa ukiwa na shida labda na elfu 30 ukampigia simu kumuomba, atakwambia njoo uijie nyumbani, na pindi unapofika kwake hakuna cha ziada mbali na kufanya nawe mapenzi kwanza ndipo akupe kiasi unachokitaka.

Kumbe siku hizi mapenzi hakuna? Hamjali utu, ndo maana wengi wenu mnaishia kulaumu kuwa tunawapiga vizinga kumbe tatizo ni ninyi.

Inafikia muda unakuwa na shida na pesa may be, akili yako inajiset kuwa ngoja nimtafute John nimuombe pesa, aniombe penzi, nitatue tatizo langu.

Wanaume kuweni na utu, achaneni na mapenzi biashara, upendo utoke moyoni, kwani bila kufanya nae mapenzi huwezi kumpatia pesa?
 
Wewe huna wazazi mpaka uanze kuomba wanaume pesa ambao hawajakuoa?

Ukianza kuomba hela mwanaume kwanza akilini anaona huna tofauti na Malaya...

Mwanaume akikupenda atakupa hela mwenyewe...

Sema nini tutunze watoto wetu wa kike.. tabia za kuomba wanaume hela ni sababu ya umaskini uliopo kwenye familia nyingi.
 
Kwani Huyo Mwanaume yeye kafanyaje akaipata hiyo Elfu 30 wewe ukashindwa kufanya Hicho kitu na wewe ukaipata hiyo elfu 30? Kujiepusha na Kulaumu watu humu

Je ulishamuomba Mwanamke Mwenzako hiyo elfu 30 akakujibuje.

Pesa hutafutwa ndugu haziombwi. Ukiomba Kubaliana na Masharti ya Uliyemuomba. Hata Nchi Yetu inaomba na Inapewa Masharti kibao na Inawezekana ingekuwa mwanamke basi Ingekuwa Malaya.

Kuwa na Chako uone kama utalaumu Wanaume.
 
Huna ndugu mpaka uombe watu Baki?

Mbona wanaume hawawaombi ninyi?

Acha kujidhalilisha na kuuvua utu wako na thamani yako kama mwanamke!

Muombe Mumeo pesa, omba wazazi pesa, omba ndugu zako pesa hasa mliozaliwa wote au ndugu za Baba au Mama yako.

Hakuna upendo kwenye kuomba omba watu Baki.

Mwanamke anayeomba pesa mtu asiye mume wake huwaga wanaume tunakuwa tunamchukulia Kwa namna ya kupekee
 
Mbona ni kanuni ya wazi ya maisha.

Ukiwa na shida na hela ya bure muombe baba yako ama kaka yako. Hao ndio wanaume ambao mko naturally bonded na they expect nothing from you zaidi ya upendo.

Mwanaume mwingine zaidi tofauti na hao hatoi pesa zake bure, hakuna kitu cha bure, ukitaka kula ukubali kuliwa.

Mwanaume anampatia msaada mwanamke ambae sio ndugu yake kwa mabadilishano, toa utamu nikupe pesa, hakuna kitu cha bure.

Kwani unadhani huyo mwanaume hana ndugu zake wanaohitaji ama wenye shida na hiyo 30k ama yeye hana shida nayo hiyo 30k? Wapo wengi tu ila anaamua kuchukua maamuzi magumu ya kukupa wewe na kuwanyima wao kwa sababu wewe kuna kitu unampa cha kumfariji angalau kupunguza machungu ya kutoa 30k yake.

Ukitaka kula lazima uliwe, hii ni natural law of life.
 
Back
Top Bottom