Wanaume mamwinyi

Wanaume mamwinyi

Huyo ni babaangu Baba Zurie ....amekaa karibu na friji na kabati la vyombo lakini atakuita wewe wa chumbani umuwekee maji ya kunywa. Umemuwekea chai ukasahau kijiko cha kuwekea sukari, anakiona kabatini lakini hawezi kukichukua bali atakuita umletee.

Mkewe akaamua kurahisisha maisha akaweka kikabati kidogo na friji chumbani kwao, yuko kitandani anamuita mama aliye nje aende kumpa juice. Hahahaahah...
Inabidi uolewe na MTU kama baba yako.
Manake kama course umehitimu
 
Ila humu kwenye ID za kujificha ndo mtujue wakinamama tulivyo. Tunacheka usoni moyoni majungu na majanga. Kutujua sisi kazi sana hasa tunapoweka maslahi yetu. Mbele.
 
Kuna wanaume wanapenda u-mwinyi bwana, yaani anaamka anaenda kuoga wakati anaoga unatandika kitanda na kuweka mazingira ya chumba vizuri. Unakwenda jikoni kuandaa chai, anatoka bafuni na taulo kiunoni anatafuta atavaa boxer na kama atakumbuka mafuta basi itakuwa kwenye viganja vya mikono. Taulo atakuachia juu ya kitanda si tatizo lake tena.

Mezani umeandaa chai na vitafunio hata kama chumvi haisikiki mfano kwenye mayai atakuita ukamchukulie jikoni hapo ni baada ya kukuita umletee maji ya kunawa na tissue ya kujikaushia.

Yaani ameshindwa kabisa kwenda kunawa jikoni au bafuni au kwenda jikoni kuchukua chumvi. Na akimaliza kula hataondoa hata kijiko mezani anaacha kila kitu pale anakwenda kukaa kwenye sofa anaangalia mpira, kusoma gazeti au anachat kwenye simu. Hiyo ni weekend.
Usijutie ni jukumu lako kama mke kufanya hivyo, vinginevyo kafanye bundumba nyumbani kwenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Nina muda mwache tu ntafanya ila nikikosa atajifanyia mwenyewe

Miaka ya nyuma kidogo, Mzee wangu na maza walirudi wote kutoka mihangaikoni midaa ya SAA tano usiku, msosi waliokuta dingi akadai kitunguu hakijaiva na akasusa kula, mama akamwambia hivi "baba Jane unaposusa kula hauwakomoi kina Jane unanikomoa Mimi maana siwez kula bila wewe kula, dingi kimya, maza akaingia jikoni hapo mida ya SAA sita akapika chakula kingine akamtengea Mzee, Mzee akala alipomaliza akajichekelesha na kwenda kulala. Asbh maza anatuadisia kiukweli niliumia ingawa huyu maza ni step maza Ila nilimuhurumia sana

invest what you are willing to lose
Basi bibie ukisikia mapenzi ndo hayo, mapenzi raha yake ni kwamba lazima mmoja aumie kwa upande wake na kwa wakati wake.

(Sorry kwa hii sentensi ifuatayo maana ni wazazi wetu) inawezekana mama yako alikuwa na hamu ya show sasa kama mzee asingekula usiku huo show asingepata. Ovaa
 
Ila humu kwenye ID za kujificha ndo mtujue wakinamama tulivyo. Tunacheka usoni moyoni majungu na majanga. Kutujua sisi kazi sana hasa tunapoweka maslahi yetu. Mbele.
All in all nyie mnaumuhimu Mkubwa sana kwetu.
 
Na ukiletewa chumvi unaitisha tooth pick
Tena inafaa nikiagiza toothpick washindane kwenda kuleta, nani wa kwanza kuifikia kopo.
Mila na desturi zetu haziruhusu eti mimi baba ninyanyuke na kitambi changu kuacha familia mezani na kufuata chochote jikoni.

Nashukuru Mungu kwa kunipa familia iliyotulia Kiafrika.
 
Mie naamini ukifika muda wa kuoa nitaoa Mke bora...na ubora wake ni pamoja na kuni hudumia sijuhi ndio kupika, kufua na kufanya usafi...
Pia najua Mke wangu hatojuta kuwa na Mimi ila nitamkera sehemu moja tuu...najua utakua na wivu sana.
Sasa hapo kazi IPO.
 
Na ukiletewa chumvi unaitisha tooth pick
Nishagundua una matatizo ya kupangilia nyumba yako

Niko meza ya chakula, toothpick, chumvi, tissue nk ndo mahala pake, sasa nisipoviona na hakuna maji ya kunawa nifanyeje? Niende kutafuta viliko? Na nikikuuliza unakunja mdomo na pua?

HAPANA labda uwe umenioa wewe
 
Mzazi wetu alihakikisha tunajua kila Kitu katika ukuaji wetu.
Hakuna ambacho kinafanyika ndani ya nyumba hakutufundisha.
Ila wanaume alituambia ametufundisha ili tuweze kujitegemea na kuwasaidia wake zetu wanapozidiwa.
Sio tupangiwe zamu.

Haya mawazo mliyonayo wadada wengi Ndio Maana mnaishia kututia hasara za kuchangia harusi aafu inavunjika Baada ya miezi miwili.
Kama unajijua unataka haki sawa usitafute mwanaume WA kiafrica.
Kaa tu kwenu uendelee kuzaa na waume za watu.
Hakuna mwanaume WA kiafrika wa 50/50. Hayupo. Hata baba yako kama unamfahamu hakuwa hivyo.
huwa mnakosea pale mnapofikiria mtaibadilisha jamii.
Yaani wewe utoke kwenu Uje kunikunja Mimi nikiwa mzee kabisa.!!
Kama mtu hajafundishwa kwao ndio imekula kwako hivo.
Hutaki kukubaliana, usiołewe!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujaelewa mada.
 
Basi bibie ukisikia mapenzi ndo hayo, mapenzi raha yake ni kwamba lazima mmoja aumie kwa upande wake na kwa wakati wake.

(Sorry kwa hii sentensi ifuatayo maana ni wazazi wetu) inawezekana mama yako alikuwa na hamu ya show sasa kama mzee asingekula usiku huo show asingepata. Ovaa
Wazee wangu washazeeka hawafanyi ujinga huo



invest what you are willing to lose
 
zamaaani niliwah mfanyia 'mlalamishi'mmoja tukio.....alikuja kuspend weekend home,tangu ijumaa mchana nilipika,vyombo nato naosha,nilifua(zangu na zake)...mwanzo alifikiri tu nabembeleza papa pale mwanzo,kufika jumapili asubuhi akaanza tena kulalamika eti naish kama hakuna mwanamke ndan!!HAMJAWAHI JIELEWA NYIE,inahitaji akili sana kuishi na wanawake!
 
Ile umeamka asubuhi ukawahi sehemu ukamuacha kalala ukirudi jioni hajatandika kitanda, hajaoga kalala kisa haukuwepo ukamuandalia maji utafikiri unaishi na chizi. Wanawake tuna tabu sana.
Ndo tatizo la wanawake ambao hamkufundwa hili,

Mwanamke aliyefundwa unyagoni, mtoto wa waungwana hawezi lalamika kwa mambo ya kipuuuzi kama haya,

Mama yako hamuwekeagi maji ya kuoga baba yako??!
 
Hayo mambo tushazoea kwenye ndoa we r Tanzanian hata usomeje mwanamke lazima mumeo umhudumie kila kitu wengi tunafundishwa hvyoo
Ni jambo la kawaida pia kwetu ukiona ananuna mke hajafundwa au uzungu mwingi

My own brand!!
Well said, tatizo vibinti vya siku hizi havifundwi, mambo ya unyago na makungwi siku hizi hakuna madam!!

Ndo mana vibinti vingi ndoa zinawashinda, akiolewa hata mwaka hamalizi kaachika!!

Hatari sana,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom