Wanaume anachofanya huyu mwenzenu ni sawa?

Wanaume anachofanya huyu mwenzenu ni sawa?

Najua mu wazima wa afya njema, mnaoumwa Mungu awafanyie wepesi mpone haraka.

Lengo la uzi huu ni kuomba ushauri kwenu na kueleweshwa Kama ni sahihi kwa mwanaume kuhitaji mpenzi wako akufanyie Kila kitu, unachotaka bila ya wewe kumjali?

Kumjali namaanisha hujui amekuja kwa nauli gani,mnawasiliana na hata ikitokea akisema Hana ata credit hawezi kukuwekea,wakati pesa unayo?

Yupo radhi akuonyeshe kiatu Cha laki mbili kwenye mtandao na anakuuliza Kama ni kizuri ili akinunue lakini sio kukujali hata kwa kidogo wewe mpenzi wake.

Sina maana kwamba ni wajibu wake,lakini anajua wakati ninaopitia Sasa kwa sababu kazi Sina lakini nipo kwenye mchakato wa kutafuta na ninaamini nitapata.

Kwa upande wangu sijazoea kuomba pesa kabisa kwa mwanaume ,najua yy anajua wajibu wake kwa mpenzi wake, lakini ninajiuliza kwa huyu mwanaume nilienae ikifikia hatua tumeingia kwenye ndoa ,ataweza kunihudumua kweli pamoja na familia?mwanaume ambae hwwezi kukupa ata senti yake?

Inafika muda natamani nifanye maamuzi magumu ya kumuacha lakini Nina nawaza labda atabadilika.

Je nitumie njia gani kumrekebisha Kama ipo?
Wewe ni kiburudisho Tu kwa huyo mwanamume, siku akipata mwanamke afaaye kuwa MKE wala hatahitaji kukumbushwa nini cha kufanya. Kwa sasa endelea kukata kiu yake ya ngono. Kusikia kwa kenge ni mpaka atokwe damu masikioni - sukuma proverb!!
 
Mnaingiaga mikenge Sana na watanashati..
Wengi wao very selfish..
Kiatu cha laki mbili halafu mpenzi hata nauli hampi?..

Atakua akukosha moyo na anavyo vaa na u handsome wake...ukimpost watsaap unajiona
Umepata ...huku unaumia kimyakimya..

Akija jamaa Sura personal..kiatu cha elfu kumi
Hata salam hupokei kumbe ana uwezo wa kukujali mara tano ya huyo
Umenichekesha saana aisee, sijawahi kumpost mwanaume wangu kwa social media,sema tu huyu ni mkono.wa birikaa
 
Kuna mwanaume ana uwezo wa kawaida sana ila ile care na mapenzi anayokuonyesha hata siku akikwama asipokupa chochote huwezi kucomplain sababu unamjua mtu wako vizuri.
Ila huyo anaonekana ni male version ya slay queens, be very careful.
Nakuelewa Sana Lenie🙏
 
Wewe ni kiburudisho Tu kwa huyo mwanamume, siku akipata mwanamke afaaye kuwa MKE wala hatahitaji kukumbushwa nini cha kufanya. Kwa sasa endelea kukata kiu yake ya ngono. Kusikia kwa kenge ni mpaka atokwe damu masikioni - sukuma proverb!!
Nilikua sijui hii methali ya kisukuma..
Kama unazo zingine za kisukuma share please
 
Zaidi ukimuaga anakuuliza uko vizur, sasa hapo umjibuje
na hapo keshakukaza au?????//// sio wako huyo...........kuhonga ni ASILI ya MWANAUME....... bado ni mvulana?.....hata soda ukimpa mwanamke/msichana ambae sio ndugu wa jamaa yako......UMEHONGA.......jiongeze bibie.......na WANAUME tukipata mdondo......hatuachi kamwe..
 
nikweli , sorry mdondo ndiyo Nini?naomba kuelewa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom