mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,767
- 7,116
Wana Jf
Nimefanya ziara ya kiutafiti wa sehemu inayoweza kustawisha zao la kibiashara kwa ubora wa juu. Nilishangazwa kukutana na maendeleo yaliyopo mkoa wa kagera. Hususani nyumba za kifahari ambazo ukikusanya unaweza kupata mji wa Arusha. Nlijiuliza kwanini wahaya hawajengi mji. Kumbe wana jambo Lao.
Jibu, wahaya wanapenda sana kula chakula cha asili, mjini ni kwa ajiri ya wageni, hivyo wameamua kujenga kijijini ili waweze kupumzika bila bughuza. Wahaya wengi wanamiliki wafanyakazi katika mashamba yao, hawana haja ya kuinvest mjini kwani hawapatumii. Anaposhuka uwanjawa ndege au kwenye mabasi, uwahi nyimbani kuchinja majogoo na mbuzi, mjini anaweza fika kununua samaki tu. Kwa sasa walioamua kuwekeza kwenye kilimo cha parachichi, kahawa, vanilla,alizeti ,viazi mviringo na magimbi hawana haja ya kukaa mjini kila siku ni kutoa hela tu, bali wanapenda kukaa vijijini kuhudumia mifugo.
Usije sema hawapendi kwao wao sio kama makabila mengine wanoogopa kujenga vijijini kwa visingizio vya kulogwa au kufanyiwa vibaya ,Nendeni mkaone mijumba yakufa mtu alafu mrudi na hoja nyepesi kuwa awapendi kwai. Bukoba wamenyimwa stand na serikali lakini badowakapigana kujenga vijiji bora. Wamenyimwa uwanja mkubwa wa ndege wakaubadirishia Chato wakati wapanda ndege wengi ni wahaya na wakanda.
Kilichokuwa kinawakwamisha ni ukabila sasa makabila mengi yameingia bukoba kulima na kufanya biashara. Wapo masai kibao wanalinda, wapo wasukuma wanalima mpunga, wapo wachaga wamejenga mabaa kibao, wapo wanyairamba wameajiliwa na wachaga kwenye mabaa. Kila kabila lipo acheni uoga mjooni bukoba kumenoga. Mimi nimetoka njombe kuja kulima vanila karagwe