Wanaopiga simu redioni kila siku wanatoa wapi fedha na muda?

Wanaopiga simu redioni kila siku wanatoa wapi fedha na muda?

Kuna wale walikuwa wanaongea ki rasi rasi Radio Tanzania (RTD) Sana hasa kwenye maonesho ya sabasaba dar zamaaani.
 
Mbona wewe hukosi muda na bundle kuingia jamii forum? Ikipita siku sijatia timu humu, hata kusoma tu nahisi kuna information kibao zimenipita.

Kila mtu ana addiction fulani katika maisha yake, ili mradi humuumizi mtu kwa kile anachofanya.
[emoji109] haya ndio maisha.
 
Sasa kuna wale wanapiga simu usiku clouds fm kipindi cha Dj elly,huwa najiuliza wanalala saa ngapi?[emoji16]kuna mtu anaitwa mavugo,yaani ukilala ukishtuka yumo[emoji16][emoji16]
 
Hahahaha, sasa afadhali huku, kuna ile radio ABOOD ya Morogoro, tena usiku kuanzia saaa saba wanapiga simu na kutuma salam kwa watu watano. Sasa kitu ambacho hunichekesha ni kwamba huwa wanatajana walewale mfano ally anapiga simu atatuma salam za kwa, rais wa sabuni, muuza bamia maarufu dumira, abdul machips, kakakuona, inshu inakuja kwamba mfano rais wa sabuni akipiga simu atarudia majina hayohayo niliyoyataja.
Kubwa kuliko wakishamaliza kutaja majina kuna kule kutuma ujumbe, sas hapo ndio kwenye kioja kikubwa ujumbe unakuwa wa ajabu sna, eg mtu atasema "UKILALA KWENYE MATANGA USIWE NA DESTURI YA KUJIKUNA SEHEMU ZA SIRI"
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Umenichekesha sana, ujue hao wana umoja wao na kipindi cha nyuma sijui kwa sasa walikuwa wanakutana Mara moja kwa mwaka, wanachagua mkoa kwa ajili ya kufanya get together party na kufahamiana na kutengeneza network.

Sasa ukiona wanasalimiana wao kwa wao ujue wanafahamiana, na sio hao wa abood FM tu Bali wa redio zote.
Kinachonishangaza huwa wanalala muda gani? Maana kila ukifungulia redio wapo hewani.
 
Mimi huwa nachokaga wale wanachangia kule idhaa ya kiswahili BBC, DW, VoA n.k. kuwa e.g "wewe rais Trump acha ubabe wako wa kijinga kutuonea sisi mataifa maskini" sasa najiuliza Trump atamuelewe kweeli! Kwann labda asimfuate kwenye tweeter page yake amweleza!!
 
Titi shara, farida mpimbi,balozi wa kudumu wa e fm sapota ......walikuwepo akina Eido mtoto wa votrotroo in dj fety voice , wale sijui ni wahaa au wasukuma wana kuwa usiku mkali kweny kipindi cha Dj Elly wa clouds fm kuanzia saa saba hadi saa kumi afajir jamaaa wana tuma salamu za kuamshana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wale ni waha
 
Miaka ya nyuma enzi za RTD Kulikuwa na watuma salamu maarufu kwa njia ya kadi na baadaye simu zilipoanza bado walikuwemo. Waliokuwa maarufu sana enzi hizo ni wajad fundi wajad wa mahuta shimon, Jumanne Sebarua Tingisha, Hawa Hassan Kilongo "super white orijino", Lusian Lems Ndambo wa Iringa, Mbago mhamed Mbago wa duka la mbolea pale Mbeya, wakulima wa ming'oko toka lindi nk. Sijui watu hawa kama wapo siku hizi
Wajadi Fundi Wajadi Binadamu Mashaka na Sijui nani wa Mke wa Mtu wa Mauta Shimoni
 
Mimi huwa nachokaga wale wanachangia kule idhaa ya kiswahili BBC, DW, VoA n.k. kuwa e.g "wewe rais Trump acha ubabe wako wa kijinga kutuonea sisi mataifa maskini" sasa najiuliza Trump atamuelewe kweeli! Kwann labda asimfuate kwenye tweeter page yake amweleza!!
Hahaha leo tu kuna mtu kutika Bukoba kampongeza waziri mkuu wa Almenia kushinda nafasi hiyo, nilikuwa na wife kwenye gari kaangua kicheko, akauliza sasa huyo waziri anamsikia huyo?
 
Hahah,mngejua hao watu wanapewa posho,..yaan kuna hao,halaf kuna wale wanaochagua nyimbo,..inshort hao wanaochagua nyimbo wanalipwa na wasanii ili wachague nyimbo hzo,na ni wao tuu kila siku,..mmoja namfahamu vzur tuu hao.ndo alinambia michezo hyo..pia hata wale wa malumbano ya hoja,wale regular.wana posho,ili kipind kinoge,..pia kwenye radio kuna stor za kutunga nying,wale waandaaj wanatengeneza ili kipind kiwe hot,..hawana tofaut na kiki zile za wasanii za magazetin na mitandaon,zote ni planned na made up stories,..
 
Back
Top Bottom