Wanaopiga simu redioni kila siku wanatoa wapi fedha na muda?

ARCHBISHOP

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
271
Reaction score
488
"Wanapata wapi muda na pesa?" Nijambo ambalo nimekuwa nikijiuliza tokea nikiwa mdogo.

Kuna watu walikuwa vinara wa kupiga simu redioni, leo wengine wamepotea, wengine wamepunguza, watu kama Suzzy Ngodoki, Pagija wa Pagija, Mwili Obale, n.k

Leo wameibuka wengine wanapiga simu kuchangia mada kila redio, utawasikia Clouds kila kipindi, RFA, Redio one, E fm.

Najiuliza hawa watu wanafanya kazi gani? Huu muda wanautoa wapi wakushinda wakitoa maoni redioni? Je, ni ushamba au ni ujanja?

Maoni kutolewa na watu wale wale kila siku, redio hazioni kuna dalili ya kufeli? Wengi wao hutoa maoni mepesi sana, unaweza dhani wanafanya mradi siku isipite bila kuchangia maoni redioni.

Wewe una mtazamo gani? Nani umemzoea kumsikia?
 
Matola ndo anawafahamu vizuri magwiji wa kupiga simu kwenye hizi radio.

Halafu hata kwenye kusalimiana wanasalimiana wenyewe kwa wenyewe.

Kuna jamaa mmoja huwa anapiga simu kwenye kipindi kinachoongozwa na somebody Mbogo, huyu jamaa akiwa anatoa hoja zake hadi mate huwa yanamtoka nadhani. Na hakosi kila nikisikiliza hiko kipindi.
 
Mkuu hizo ni hobby kama kuogelea na kwenda gym tu...
Mbona wadau wanaenda kuogelea na hela wanatoa beach??
Na yeye anapiga kwa kutumia vocha yake kama hobby..
Mh! Hatari
 
Kuanzia clouds, east africa radio, capital radio, radio one na zingine sikosagi kusikia jina la spora malisa khaa sijui huwa anaweka alarm? kwenye kutuma msg pia huwezi mkosa sikuhizi namsikia mpaka bbc swahili.
Hawa kuna kitu nyuma ya pazia sio bure
 
Matola ndo anawafahamu vizuri magwiji wa kupiga simu kwenye hizi radio.

Halafu hata kwenye kusalimiana wanasalimiana wenyewe kwa wenyewe.

Kuna jamaa mmoja huwa anapiga simu kwenye kipindi kinachoongozwa na somebody Mbogo, huyu jamaa akiwa anatoa hoja zake hadi mate huwa yanamtoka nadhani. Na hakosi kila nikisikiliza hiko kipindi.
Mzee unaona mate mpaka kwenye redio?
 
"Wanapata wapi muda na pesa?" Nijambo ambalo nimekuwa nikijiuliza tokea nikiwa mdogo.

Kuna watu walikuwa vinara wa kupiga simu redioni, leo wengine wamepotea, wengine wamepunguza, watu kama Suzzy Ngodoki, Pagija wa Pagija, Mwili Obale, n.k

Leo wameibuka wengine wanapiga simu kuchangia mada kila redio, utawasikia Clouds kila kipindi, RFA, Redio one, E fm.

Najiuliza hawa watu wanafanya kazi gani? Huu muda wanautoa wapi wakushinda wakitoa maoni redioni? Je, ni ushamba au ni ujanja?

Maoni kutolewa na watu wale wale kila siku, redio hazioni kuna dalili ya kufeli? Wengi wao hutoa maoni mepesi sana, unaweza dhani wanafanya mradi siku isipite bila kuchangia maoni redioni.

Wewe una mtazamo gani? Nani umemzoea kumsikia?

kila mtu na kazi yake, kama wewe ilivo kazi yako kufatilia maisha ya wengine na vitu visivokuhusu
 
Back
Top Bottom