"Wanapata wapi muda na pesa?" Nijambo ambalo nimekuwa nikijiuliza tokea nikiwa mdogo.
Kuna watu walikuwa vinara wa kupiga simu redioni, leo wengine wamepotea, wengine wamepunguza, watu kama Suzzy Ngodoki, Pagija wa Pagija, Mwili Obale, n.k
Leo wameibuka wengine wanapiga simu kuchangia mada kila redio, utawasikia Clouds kila kipindi, RFA, Redio one, E fm.
Najiuliza hawa watu wanafanya kazi gani? Huu muda wanautoa wapi wakushinda wakitoa maoni redioni? Je, ni ushamba au ni ujanja?
Maoni kutolewa na watu wale wale kila siku, redio hazioni kuna dalili ya kufeli? Wengi wao hutoa maoni mepesi sana, unaweza dhani wanafanya mradi siku isipite bila kuchangia maoni redioni.
Wewe una mtazamo gani? Nani umemzoea kumsikia?