Wanaopiga simu redioni kila siku wanatoa wapi fedha na muda?

Wanaopiga simu redioni kila siku wanatoa wapi fedha na muda?

Kuna hawa:
1. Fundi Hamis Full Migebuka
2. Sjiu Derva bajaji Masasi
3. Juma Dea..
Hawa kila kipindi clouds wamo
yaaani hao huwa wana sikiliza radio kutwa nzima....waweza kukuta huo ni ugonjwa ila hawajui tu
 
Huwa ni maigizo kama ya BIKO. Hakuna mwenye vocha au muda wa kuongea na DJ wakati ndani hamna chakula.
 
Kweli mkuu,na huyu wa dom namfaham pia anaitwa Imma Sadala hawa jamaa kama usemavyo mi mpaka DW nawasikiaga,
Juhudi tu mpk wamekuwa brand sasa. Majamaa wamejidedicate hatari kila radio wamo
 
Kuna wale ambao ujumbe wao BBC ndio uwa unasomwa tu pamoja na kwamba waliochangia kwenye habari husika ni wengi sana, sasa sijui uwa wanaselect ujumbe wao tu? Mmoja yuko Chunya, Kibaha, Muleba lazima uwasikie ujumbe wao unasomwa
Ukishakua nguli unazipata namba binafsi za watangazaji unamtumia straight, yupo mshkaji wangu anamtumiaga sms maulidi kitenge anasoma hewani.
 
Nimeshawai fanya hii mambo...

Kusikika kama clouds fm kuna muda wa kutuma sms mfano kila siku saa saba na dk 16 lazima itasomwa...

Ukipiga simu ukiona iko busy unakata haraka unapiga tena hivo hivo tena na tena mpaka utadaka line...

Unakuta mnafahamiana watu salamu mpaka simiyu uko ndani ndani hata redio zingine huzijui ila mnarushiana namba na kushtuana mtume sms ama kupiga simu wakati gani na mada inahusu nini....

Faida
Watuma salam na ma requester maarufu wanakua wanajulikana na wasanii na ma dj..
Mfano
Daudi wa kota
Young mreno wa ilala
Talavi talavencha
Mtoto wa vitoto
Brenda tesha
Rasi sanlee
Fundi khamis wa migebuka
Taita la mzumbe
Baba tovu mkali wa kuingiza vocha zilizotumika,
Mohamed jongo
Lawena nsonda
Amadi machaku
Ni wengi sana na wanajua ila faida ya kwanza

1:shoo nyingi wanaingia bure
2:wan
apata mda wa ku hang na wasanii mfano waziri dello na young mreno
3:unalipwa kuchagua nyimbo ili iendelee kuskika redion na ibaki top ten..kama ni cash, credit na bundle..

Baadhi ya wasanii waliokua wanafanya hii Belle 9, Hakeem five, stamina, kobba, stive rnb n.k

Enzi hizo kwa sasa sijui wanafaidikaje
 
Umri umepita sasa enzi za akina Muntala tala V tala vencha,squash girl,Daudi wa kota XXL hileeee.
haaa squash girl umenikumbusha mbari sana ni kasichana tu enzi hizo anakimbiza mpk wenzake wakawa wanalalamika anapendelewa hta O LEVER alikuwa ajamaliza wala umri haujaenda kivile
alikuwa ni best yangu sana ni mtoto wa VINGUNGUTI now anaishi mwananyamala
 
Back
Top Bottom