Wanaongoza kipindi cha ITV cha Malumbano ya Hoja sina imani

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,691
149,909
Kipindi cha Malumbano ya Hoja kinaendelea hivi sasa ITV na mada ikiwa inasema : "MWENENDO WA BUNGE LA 11.JE,LINA AGENDA ZINAZOLIUNGANISHA KATIKA KUSIMAMIIA SERIKALI YA AWAMU YA TANO?"

Binafsi naona watangazaji wanaoongoza hiki kipindi hawako nuetral na nimepoteza imani nao.

Naomba mwenye nafasi ya kufuatilia nae afuatikie alafu awapime.
 
Huyo jamaa mwenye tai sijui kuna cheo anavizia yani mwanahabari mzima anatetea bunge kutokua live
 
Kipindi ni kizuri tatizo nikuwa wanajitahidi watu waseme wanayoyapenda kama kutokuikosoa serikali. Waache serikali isemwe ili nchi isonge mbele.
 
Hawana uwezo wa kuongoza kipindi hiki, kwanza wanatumia muda wa watu, wanauliza maswali ya kitoto kwa wazungumzaji na pia hawaelewi wao ni akina nani
 
Wadau, naangalia kipindi cha malumbano ya hoja ITV hivi sana. Mmoja wa wachokoza mada ni Dr. Avemaria Semakafu.
Dr. Avemaria anasema wabunge wanaacha kuongelea mambo ya majimbo yao badala yake wanaongelea mambo tofauti kama issue ya Lugumi.

Binafsi nimemshangaa huyu Dr. Avemaria. Hivi kama kweli kila mbunge akijishughulisha na mambo ya jimbo lake tu, nani atawatetea twiga wanaopandishwa ndege? Dr. Avemaria anasahau kuwa mojawapo ya kazi ya Bunge ni kuisimamia serikali. Au kama kila mbunge akisimamia jimbo lake nani ataihoji serikali kuhusu kashfa ya Lugumi? Kwakweli Daktari wa falsafa anaweza kuwa mvivu wa kufikiri kiasi hicho?
 
Back
Top Bottom