Wanaongoza kipindi cha ITV cha Malumbano ya Hoja sina imani

Wanaongoza kipindi cha ITV cha Malumbano ya Hoja sina imani

Chadema hata mtu akimuuliza swali la kumchalenji katika hoja yake anaita ni kupingwa..... Hovyo kabisa.....

Mfano swala la bunge live, Kapalatu anamchalenji mtu kwamba mbona miaka ya 80 bunge halikuwa live na maendeleo yalikuwa yana patikana! Sasa mtu badala ya kutetea hoja kuonesha tofauti ya miaka hiyo na sasa ili mjadala uendelee kunoga yeye anakimbilia huku kwamba Kapalatu anapinga hoja zao.... Ujinga!
 
Wale ni moderators, lazima wasimamie kipindi kutokana na miongozo waliyopewa. Hawawezi kuruhusu kila mtu kuongea ansvyojisikia. Pia, lazima walinde ethics za kazi na ofisi yao.

Niliangalia kipindi jana, kuna watu wengi tu walikuwa wanaongea mambo mengi nje ya mada, je mlitaka waachwe waongee wanavyojisikia? Mfano yule diwani, he was horrible, yani unajiuliza hivi huyu alijiandaa na mada tajwa au amekurupushwa.

Kingine, mule watu wameingia na makundi yao, wanajipigia makofi na kujisifu ovyo. Kambaya na Kapalatu wanaongoza kipindi vizuri sana, ni lazima walinde ofisi na kazi zao.

Mwisho, kama mliangalia malumbano yaliyofanyika Morogoro, mtaona tofauti kubwa. Watu wa moro walijikita kwenye mada, waliongea points as compared to wanadarisalama. Watu wa Dar nao wamekuwa na vijembe kama wabunge.
 
Kweli mkuu uko sahihi,tatizo watanzania tumejijengea kutokufuta sheria kanuni na taratibu..Au wao walitaka waachwe waongee hata kama wako nje ya mada.
 
Kama yeye atakuwa zereoo wewe utakuwa muuza line za mtandao wa tigo.

povu limekutoka mkuu, pole sana lakini huo ndio ukweli kama huyo bonge ndio wewe basi jua kabisa unaharibu kipindi kwani hujui role yako kwenye hicho kipindi.
 
Chadema hata mtu akimuuliza swali la kumchalenji katika hoja yake anaita ni kupingwa..... Hovyo kabisa.....

Mfano swala la bunge live, Kapalatu anamchalenji mtu kwamba mbona miaka ya 80 bunge halikuwa live na maendeleo yalikuwa yana patikana! Sasa mtu badala ya kutetea hoja kuonesha tofauti ya miaka hiyo na sasa ili mjadala uendelee kunoga yeye anakimbilia huku kwamba Kapalatu anapinga hoja zao.... Ujinga!
Sio siri Kapalatu ni mzigo kwenye hicho kipindi, amekua kwanza akipoteza muda kuingilia mjadala.
 
huyu kambaya mi simwelewagi kabisa

Siyo wewe tu Mkuu, hata mimi hupata wakati mgumu sana kusikiliza maongezi ya huyu jamaa. Sasa jana kuna mahali aliropoka ' kama ikitokea watu wanapimwa akili timamu, na wakaja kwangu wakakuta ni timamu mpaka imepitiliza, blah blah'.

Hapohapo nikakwazika, maana inaonesha jamaa haelewi maana ya 'timamu'. Maana hata akili kupitiliza si timamu tena, kitu chote chema kikipitiliza kinapoteza heshima, ndiyo maana sasa hivi serikali inapambana na LUMBESA. Au amepitiwa na ule msemo wa wenzetu, 'too much of one thing is good for nothing'.

Kambaya popote ulipo jielimishe.
 
Muanzisha thread unaonesha dhahiri wewe ni CDM coz mnapenda sana kulalamika,mimi nimefuatilia vizur na nilichokiona hawa waongozaji wamehangaishwa sana na watu wasio na utambuzi kama wewe ambao tangu wanatoka nyumbani wamesahau agenda ya malumbano ya hoja wakaja na agenda ya bunge live hapa ndipo tatizo lilipo.
 
hawa jamaa kwa kweli wanazidi kungara kipindi wamekitendea haki bigg up kapalatu ,
 
Wadau, naangalia kipindi cha malumbano ya hoja ITV hivi sana. Mmoja wa wachokoza mada ni Dr. Avemaria Semakafu.
Dr. Avemaria anasema wabunge wanaacha kuongelea mambo ya majimbo yao badala yake wanaongelea mambo tofauti kama issue ya Lugumi.

Binafsi nimemshangaa huyu Dr. Avemaria. Hivi kama kweli kila mbunge akijishughulisha na mambo ya jimbo lake tu, nani atawatetea twiga wanaopandishwa ndege? Dr. Avemaria anasahau kuwa mojawapo ya kazi ya Bunge ni kuisimamia serikali. Au kama kila mbunge akisimamia jimbo lake nani ataihoji serikali kuhusu kashfa ya Lugumi? Kwakweli Daktari wa falsafa anaweza kuwa mvivu wa kufikiri kiasi hicho?
Samahani, huyo dokta ana PhD? Aisee haya mambo ya kuchumia tumbo ni mabaya sana, wasomi wetu wanajitoa ufahamu na kufumbia mambo ya wazi ili wamfurahishe mtu fulani na baadaye wanufaike. Yaani Dr. mzima hajui kazi za wabunge kikatiba? Kuwakilisha majombo yao ni mojawapo ya kazi na pia kusimamia serikali, kutunga sharia n.k. Sasa anashangaa nini? Hii ni aibu kwa Taifa letu. Pia anawaibisha wasomi wenzake.
 
Mkuu hayo ni maswali ya kuchalenji hoja na wala sio swali la kupinga....
Mkuu Idengenda ni kweli kabisa inawezekana alikuwa anataka kuchallenge hoja lakini ukimfuatilia hata ile body language yake na the wayalivyouliza utaona kabisa akuvutiwa na hoja iliyotolewa. Alafu nimefikia conclussion hii baada ya kumfuatilia vipindi kadhaa, ingawa pia vijana wa Chadema na CCM wanaoshiriki kipindi kile wanavuruga sana kile kipindi (Baadhi yao lakini)
 
Back
Top Bottom