Miaka 3 ya kifo cha Magufuli: Haya ndiyo mabaya yake katika utawala wake

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Miaka 6 ya utawala wa Mwendazake ilikua ya Machozi, Jasho na Damu kwa Watanzania. Haya ni baadhi ya matukio niliyoyakumbuka kwa haraka, baadhi yalitokea nikiwa huko nyumbani na mengine yametokea nikiwa nimeshaondoka.

1. Alizika uhuru wa vyombo vya habari na kutia saini sheria kandamizi kwa vyombo vya habari. Vyombo vyote vililazimishwa kumuandika kwa kumsifu na kumpamba, kilichothubutu kumkosoa kilifungiwa.

2. Alitumia nguvu nyingi kupambana na upinzani na kutesa wanasiasa wa upinzani kwa kuwafungulia kesi za uongo mpaka leo bado wengi wapo jela kwa kesi za kisiasa za kubambikiziwa.

3. Aligawanya nchi kwa misingi ya ukabila, ukanda, uchama na udini na ubaguzi wa kijinsia. Serikali yake ilijaa watu wa kanda ya ziwa na 75% ya serikali yake ilijaa wasukuma watupu

4. Alikua na ubaguzi wa kijinsia na aliendekeza mfumo dume. Wanawake walikua 17% tu ya mawaziri katika serikali yake.

5. Alihakikisha wakuu wa vyombo vya ulinzi wanatoka kanda ya ziwa ili kumlinda likitokea lolote, CDF - Mara, IGP - Mara na CGP - Geita na CGF - Mwanza. Madikteta wote hufanya hivi maana wanajua watu wa kwao hawawezi kuwageuka.

6. Hakupandisha mishahara kwa wafanyakazi wa umma kwa miaka yote 6 ya utawala wake.

7. Hakutangaza ajira mpya katika kipindi chote cha utawala wake. Waalimu waliomaliza vyuo mwaka 2015 hadi leo wapo mtaaji jobless.

8. Aliua sekta binafsi kwa kutoza kodi kubwa, na kuharibu mazingira ya biashara. Hoteli nyingi za kitalii zimekufa kama vile Ngurdoto, Impala, Naura Spring na nyingine zimegeuka hostel za wanafunzi kama Landmark ya Ubungo.

9. Alipunguza mzunguko wa pesa mtaani na kuhakikisha matajiri wanaishi kama mashetani.

10. Katika utawala wake waliibuka watu wasiojulikana ambao waliteka, kujeruhi na kuua watu wasio na hatia. Watu hao walimpiga risasi Tundu Lissu mchana kweupe na mpaka leo hawajakamatwa.

11. Aliwapa nguvu baadhi ya viongozi kama vile Makonda na Sabaya kutesa na kuumiza wananchi kadri walivyojisikia. Makonda alishambulia kituo cha CMG kwa mitutu ya bunduki lakini hakuchukuliwa hatua yoyote. DC Sabaya majuzi kampiga diwani wa Sombetini nusura kifo.

12. Alifuta fao la kujitoa na kusababisha watumishi wengi wenye mikataba ya muda mfupi kuishi maisha magumu baada ya ajira zao kukoma.

13. Katika serikali yake Wapinzani walionekana maadui na sio watu wenye mawazo mbadala. Waliteswa na kufunguliwa kesi za uchochezi. Wengine walipotezwa na hata kuuawa. Alitamani upinzani ufe.

15. Katika utawala wake maiti 17 ziliokotwa ufukwe wa Coco na nyingine 6 ziliokotwa mto Ruvu kwa pamoja zikiwa zimefungwa kwenye sandarusi, na baadhi zikivuja damu.

16. Aliharibu mahusiano ya kidiplomasia na mataifa mengi ukimwenguni. Serikali yake ilichoma vifaranga vya kuku kutoka Kenya na kutaifisha ng'ombe waliovuka mpaka kuja Tanzania.

17. Alisababisha wanasiasa wa Tanzania wakimbie nchi na kuishi uhamisho kama wakimbizi wa kisiasa wakiwemo Ansbert Ngurumo, Tundu Lissu na Godbless Lema.

18. Alitumia mabavu kulazimisha ushindi kwenye uchaguzi wa 2020 na kuhakikisha CCM inashinda majimbo yote. Alipora ushindi wa upinzani kwenye majimbo mengi kwa mtutu wa bunduki.

19. Alitumia sheria ya uhujumu uchumi kutesa wapinzani wake kisiasa na wafanyabiashara aliokua na kisasi kwa mfano Rugemala na Lema wa Elerai Construction.

20. Alipenda kuabudiwa, kutukuzwa na kuogopwa. Wote waliomnyenyekea aliwapa vyeo.

21. Aliamini mawazo yake ndio sahihi na hakutaka kushauriwa kwenye jambo lolote. Aliwahi kusema yeye hapangiwi cha kufanya.

22. Alipenda kuonekana mcha Mungu japo kiuhalisia ni dikteta katili aliyetisha. Inadaiwa alimpoteza Ben Saanane baada ya kuhoji kuhusu PHD yake.

23. Alitangaza kuwa Tanzania haina corona na akataka watu wasivae barakoa wala wasikubali chanjo kutoka nje ya nchi.

24. Alipeleka miradi mingi ya maendeleo kijijini kwake Chato kama uwanja wa ndege, hospitali ya rufaa, benkiz barabara za lami na mbuga ya wanyama ambayo haikua na wanyama ikabidi kuhamisha kutoka mbuza zingine.

25. Aliingilia mihimili yote ya dola ikiwemo mahakama na bunge. Aliwazawadia vyeo vya ujaji mahakimu waliowafunga wapinzani jela.

26. Aliigeuza Tanzania kama mali yake binafsi na katika kila mradi alipenda atajwe yeye. Aliamini akiondoka hakuna atakayeweza kuendeleza yale aliyofanya. Bunge liliwahi kupendekeza kumuongezea muda wa kutawala atakapomaliza mihula yake miwili, kumbe Mungu ana mipango yake hata hiyo miezi 4 hakumaliza ya kura alizoiba

1.Chato International Airport
2.Chato National Park
3.Trafic light Chato
4.3 star hotel Chato (TANAPA)
5.Bohari ya kanda madawa Chato
6.Hospital ya rufaa Chato
7.Stadium (proposa)
8.CRDB Chato

Jana usiku nilienda kumtembelea mzee mmoja ambaye ni mtu wangu wa karibu anae jihusisha na biashara ya madini,akinipa story fupi tu ya rafiki yake ambayo ilinihuzunisha sana.

Jamaa yake alikua na zaidi ya bilioni 7 kwenye account yake bank mwaka jana mwanzoni,alipigiwa simu na branch manager aende urgently na alipofika pale mida ya mchana akajulishwa kwamba account yake imepigwa spana na tra (task force). Ikabidi aende tra mkoa ili kufuatilia hiyo ishu.

Tra mkoani wakamwambia inabidi awasiliane na TRA makao makuu,ikapigwa sim akapewa appointment saa tatu asubuhi next day. Akapanda ndege jioni hiyo kuelekea huko, asubuhi kafika mapema kasechewa kweli kweli then akaingia ofisini kuzungumza na team roho mbaya.

Wewe ndio fulani? Ndio, inaonekana una pesa nyingi sana kwa account ila hulipi kodi. Jamaa akasema akasema kodi nalipa na ninapata tax clearance kila mwaka mbona sielewi? Wakamwambia ana option 2 TRA wachukue 5B wamuachie 2 au akalete vielelezo huku wakiendelea kuzuia hela zote. Vielelezo visipo jitosheleza watachukua hela zote pamoja na kesi ya uhujumu uchumi.

Pale ulikua huruhusiwi kwenda na mwanasheria wala accountant,jamaa akatoka nje kufikiria kwa muda akaona isiwe nongwa akawaachia 5B lakini pia akaambiwa arudi CCM kwa kujitangaza kwenye media kwa sababu alikua supporter mkubwa wa lowasa uchaguzi wa 2015.

Matajiri wengi wa mawe wameumizwa sana huko kanda ya kaskazini ila wamekaa kimya tu,bora huyu jamaa amekufa maana alikua anatupeleka shimoni/motoni kiuchumi na kijamii.

Akasema nyumba za kimara zibomolewe lakini za mwanza zisibomolewe maana ni wapiga kura wake....Maiti zilikua zinaokotwa baharini enz za mwendazake

Nitamkumbua Magufuli kwa ukatili wake wa kutisha

1. Kuvunja nyumba za wananchi wa Kimara - Mbezi bila chembe ya huruma ila wale wa mwanza aliwaachia

2.Kupora Korosho za wananchi wa mikoa ya kusini kwa mtutu wa bunduki, hii hali iiwatia wananchi umasikini

3. Bila kujali kuwa watu wameshahudumu serikalini kwa muda mrefu na wanategemea kustaafu, akapitisha hoja ya uhakiki na kuwafukuza maelfu ya watu hao Huku akiwaacha bila kuwagusa wanasiasa na wateule wake katika hilo zoezi

4. Kubabikizia watu kesi za uhujumu uchumi, kuwatesa kupitia mfumo wa mashitaka na kuzisababishia familia zao maumivu makubwa na hali ngumu

5. Kuendelea kuwashikilia mamia ya masheikh walioko jela huku akisamehe wabakaji akina Babu Seya

6. Kukataa kuwapa watumishi wa serikai stahiki zao kwa wakati, ikiwemo kupandishwa madaraja na nyongeza za ishahara

7. Kuharibu chaguzi zote zilizofanyika chini ya serikali yake, kuanzia zile za marudio, serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, Alidhuluu haki ya wananchi kuchagua viongozi wao

8. Magufuli alitunga sheria kandamizi, na kuvuruga misingi ya katiba. Kafanya kia jitihada kulifanya bunge liwe butu, kuiweka mahakama mfukoni etc

9. Magufuli alikuwa na kauli mbaya zisizo na staha mfano "sisomeshi wazazi, serikali siyo iliyoleta tetemeko, baki na mavi yako nyumbani, nitapiga mashangazi.. etc"

10. Alikuwa na miradi kadhaa au mpango wa miradi kadhaa ambayo ni white elephant mfano, uwanja wa ndege Chato, Midege,Mpango wa Uwanja wa mpira Chato

11..Magufuli alikuwa mkabila, huhitaji kuwa mwanasayansi wa elimu ya jamii kuona kuwa teuzi zake ziliaia sana watu wa kanda na kabila lake.

12. Magufuli alikuwa haheshimu katiba waa sheria pale zinapokinzana na anachokitaka yeye, mfano haki ya kufanya siasa kwa vyama vya siasa iliyokuwepo kikatiba hakuiheshimu

13. Magufulu hakuthubutu na wala hakujali kufanya uchunguzi juu ya kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda, Kanguye na waliompiga risasi Lissu

Kwa hiyo mimi nakichukulia kifo cha Magufuli kama nafasi muhimu ili Taifa letu lipone.

Na sisi kama Taifa, tumeona kwa macho yetu namna katiba ya sasa ilivyokuwa hatari kama tunampata mtu mmoja asiyejali, ambaye ana element za udikteta, basi tuitumie nafasi hii kuliponya Taifa

Tangulia Magufuli, uwongo mbaya sitokumiss na sijawahi kukupenda kwa style ya uongozi wako, ninatamani Taifa lisipate Kiongozi mwenye mapungufu ya aina yako, ni mapungufu hatari kabisa

UPDATE

Ndugu yangu mmoja alishtakiwa kwa uhujumu uchumi akituhumiwa kukwepa kodi kwenye biashara zake. Lakini yeye anadai ni kesi ya kisiasa. Mwaka 2015 aliombwa kusupport kampeni za CCM akakataa lakini alifadhili kampeni za UKAWA. Anaamini hiki ndicho kilichomponza.

Mwaka 2018 alikamatwa na baadhi ya biashara zake kufungwa, na nyingine zikashindwa kujiendesha kutokana na makadirio makubwa ya kodi.

Baada ya kukaa gerezani miaka miwili akaona bora akiri ili atoke (the lesser evil). Wakati wa majadiliano na DPP akatakiwa kulipa zaidi ya 200M. Akakubali kufilisi biashara zake chache zilizobakia ili "kununua" uhuru wake.

Mwaka jana tulimtembelea gerezani mimi na Dr.Cyrilo. Tukamuuliza kwanini umeamua kukiri? Huoni itakuwekea doa? Kuna nchi utazuiwa kwenda kwa sababu ya "criminal record" ya uhujumu uchumi. Kuna fursa za biashara utashindwa kupata. Kwanini usingepambana ushinde badala ya kukiri.

Huku akilengwalengwa na machozi akajibu, nachotaka kwa sasa ni kuwa huru tu. Nikishatoka hiyo "criminal record" anaweza kuja Rais mwingine akaifuta, huwezi jua. Tukaagana, akarudi zake nyuma ya nondo.

Licha ya kukiri na kuwa tayari kulipa (plea burgaining) lakini bado hakuachiwa. Aliambiwa jalada bado lipo kwa DPP.

Wiki iliyopita amefutiwa mashtaka yote na kuachiwa huru, bila kulipa chochote. Siku anaachiwa wala hakujua kama angeachiwa. Ilitumwa "remove order" gerezani, akaenda mahakani bila kubeba chochote maana haikua siku ya kesi. Hata wakili wake hakuwepo.

Miguuni alivaa kandambili. Alipofika mahakamani akaambiwa, Jamhuri imekufutia mashtka yote na haina nia ya kuendelea na kesi. Akadhani ni mtego ili wamkamate tena. Akajaribu kutoka nje ya mahakama, lakini hakuna mtu aliyehangaika nae.

Akaita taxi, ikampeleka nyumbani. Mkewe akapata suprise ambayo hakuitegemea. Akaanguka, alipoamka akaanza kulia. Watoto walipomuona baba yao nao wakalia. Majirani wakaja na kumkumbatia, wakilia. Nyumba ikatawala machozi.

Hii nchi imepitia kipindi kigumu sana. Kuna jinsi Mungu anamtumia mama Samia kuponya majeraha na kuokoa mioyo iliyopondeka. Biblia inasema Haki huinua taifa bali dhambi ni aibu ya watu wowote (Mithali 14:34).!

Mtu ambaye aliweza kushirikiana na mpwa wake na kijana mmoja wa Mwanza diaspora (Dick mpemba) ambaye amefariki mwaka jana kutorosha mabilioni kuyaficha Canada mtu huyo anaweza kuwa vipi kiongozi wa wanyonge?

Ni kichaa tu anayeweza kudhani eti mwendazake hakua fisadi alikua fisadi papa

Hakuna mtu anaweza mzidi kwa ukwapuaji jamaa alijipimia haswa huko Canada ni mabilioni kwa mabilioni karibia bilioni 500 alizificha huko halafu kuna watu wanasema hakua mbadhirifu alikua mkwapuaji mkubwa sana

Mtu kaacha majumba huko Canada, kanunua hadi supermarkets za kutosha huko eti alikua baba wa wanyonge, Ripoti ya Assad ilisema ni trilioni 4 zilichotwa lakini muulizeni na naamini ipo siku atasema maana siku kadhaa kabla ya ripoti alifatwa na "Wasiojulikana" zaidi ya mara 3 siku ya kwanza wakimvamia garini akitoka sheli jioni kujaza mafuta ilimbidi mwishowe akakaa na wakaguzi wengine akapunguza baada ya vitisho hadi vya kufuatwa ofisini....Ndo maana Assad huwa hamsifii mwendazake hata chembe Prof Assad akiwa anazungumzia changamoto alizopitia katika utumishi wake

Anasema alikwenda kukagua wizara moja, akauliza kuhusu matumizi ya Pesa fulani akaambiwa usikague matumizi haya,

Akauliza kwanini asikague matumizi ya fedha zile akajibiwa kuwa matumizi yake inajua Ikulu!

Bado mamia ya mahekta aliyojipimia huko kwenye hifadhi za taifa na mapori....Mtu ambaye aliamuru bilioni 900 zitolewe hazina zikafanye kazi ya kununua wabunge na madiwani huyo si fisadi papa?

Bado alifanya ufisadi mkubwa kwenye manunuzi ya ndege alileta ndege used huku akihakikisha kila ndege anapiga

Mtu ambaye alificha zaidi ya trilioni 1.2 kwenye accounts za siri za benk huko Malaysia na Uchina anaweza vipi kusema alikua Msafi?
Serikali yake ilijaa wizi na ufisadi, Wizara ya mambo ya ndani waliingia mkataba wa trilioni 1 kununua sare za polisi huku yeye mwendazake akichukua mgao wa bilioni 650 muulizeni kangi Lugola.

Msisahau hata siku ya msiba wake kule Chato inadaiwa hata mrithi wake analijua hili, vilikutwa viroba vimejaa pesa nyingine ziliwekwa hadi kwenye majaba halafu ni dola za kimarekani huku tukipumbazwa kwamba mabeberu ni watu wa ajabu na ni wabaya lakini yeye alificha dola za kimarekani ndani mwake.

Kwani kilichomuua Lwajabe ninini??

Jinsi Leopold Lwajabe walivyomuua.

Hii kwanza isichukuliwe kama kitu cha bahati mbaya ama kufumbia macho na kujaribu kuzunguka mbuyu. Muuaji wa huyu Injinia ni hayati lazima tumnyooshee kidole bila kuweka shaka wala kufanya unafiki kwanza alifatwa na watu wa Intel HQ, walioagizwa kudeal nae, walitumia simu ya mmoja wa hao jamaa wa Intel kumpigia mida ya saa tatu asubuhi akiwa ofisini kwake kisha wakaondoka nae wakakaa siku mbili wakimuhoji na kumtishia uhai wake, tar 18 wakamwambia asiseme lolote wakimuachia arudi uraiani, wakamchukua mpaka karibu na kwake wakamuacha hapo. Na kumpa masharti ya asiripoti popote kwamba alichukuliwa na watu wa serikali kikosi maalumu.

Hao wakamwambia ila wakutane nae Mburahati kituo cha Polisi kwa mahojiano zaidi siku watakapomuhitaji, ila asiseme kwa mtu yeyote waliyomuhoji wala mtendea. Badala yake wakambrain wash aje aseme alichanganyikiwa tu akajikuta katoweka.

Wiki moja mbele akapigiwa simu na watu wale wale kwamba aende kituo cha Polisi Mburahati kwa mahojiano zaidi, akafanya hilo akaaga Ofisini kwake na kuanza safari jamaa walimsubiria Mburahati wakahojiana nae kwa sehemu kisha, wakamwambia anatakiwa na wakuu kwa mahojiano zaidi, wakampakia kwenye gari private kisha wakaanza nae safari kumpelaka walikojua wao na simu zake zote wakazima.

Moja ya mambo ambayo wanamtuhumu ni kwamba anashirikiana na mabeberu wa EU kumuhujumu Mh Rais. Kumbukeni nani anaejinadi kupoteza watu watakao bainika kumkosoa ama kua kikwazo kwa Rais. Leopold kosa lake kubwa ni kumkatalia mwendazake na genge lake kuchota mabilioni kwenye kitengo cha EU alichokua akikisimamia. Wakamuona kama msaliti kwanini anasema kwa wenyepesa kwamba kuna pesa inatakiwa itoke bila yeye kuambiwa aseme nini kwa hao wazungu.

Walitaka watoe bilioni 500 wazipeleke nje kupitia doto james ambaye mkabidhiwa ni dick mpemba yule mratibu wa vuguvugu la Mwanza ambalo lilikua na kauli mbiu ya kuhakikisha wakuja wote wanaangushwa kwenye majimbo kanda ya ziwa huku wasukuma pekee wakichukuwa majimbo (Nitaleta huu ushahidi hapa Jf soon na jinsi mwendazake alivyokua na mpango wa kuunda himaya ya kikabila na mratibu alikua ni huyu Dick na hata Gwajiboy alikua anaujua huu mpango nitakuja kuleta ushahidi)
Tuendelee na ishu ya Lwajabe

Kuna taarifa mbovu sana sana ya uchotwaji wa pesa kwenye hicho kitengo alichokua akisimamia. Na yeye ndio alikua anajua na muaandaaji wa report na report alizozituma kwa wenye pesa EU ndani yake aliainisha matuzi ambayo hayakukusudiwa na EU lakini pesa zilichukuliwa kwenye fungu lao. Hicho kikaonekana kama yeye kasaliti usiri wa uchotaji huo wa pesa na ili kuficha maovu yoote ya upigaji basi wameamua kumuua kuficha uchafu wote.

alimchukua mpaka mapori ya huko Mkuranga na wamkamlawiti kwa zamu huku wakimrekodi kisha kummaliza.Rejea Kifo cha Leopold Lwajabe dhidi ya uongo wa Mambosasa: Aibu dunia nzima "skunk of the world"

Ukiachana na hiyo 1.5 trilioni kuna ishu nyingine ya trilioni 1.6 ambazo zilitumika juu kwa juu na ikulu bila kupita mfuko mkuu wa Hazina akadai zilikwenda kwenye miradi lakini inadaiwa ziliingizwa kwenye account zake mbili ambazo zilikuwa zinasimamiwa na Mpwa wake dotto James!!!

Ndo maana aliamuru serikali yake ijitoe kwenye mfumo wa kujiendesha kwa uwazi mwaka 2017 kwasababu alifahamu ufisadi wake na ili aendelee kupiga mabilioni kwa matrilioni na baada ya hapo ndo report za kutisha za wakaguzi zikaanza kutikisa taifa kwa ufisadi aliokua anafanya rejea Tanzania yajitoa rasmi katika mpango wa uendeshaji Serikali kwa Uwazi (OGP)

Taifa lilipitia magumu mazito sana kwa miaka 6 ya yule jamaa huwa najiuliza ilikuaje akawa Rais?Hakua na utu hata kidogo alikua katili kuwahi kutokea haya tunayoyaandika yalionekana kwa macho vipi madudu mengi ambayo aliyafanya bila kufichuka?Tumshukuru Mungu kwa kila jambo ila kwa mateso nchi iliyopitia sijui kama itakua ni rahisi kwa watanzania kupona majeraha ya yule bwana.
 
Alipojua anakufa hakutaka kumpigia Simu Mama Samia ili kumpa siri za kuendeleza mapambano (Succesion Plan) bali alikimbilia kutubu na kuomba mapadre wambariki kuiokoa nafsi yake! Mungu aMrehemu.
 
Ndiyo maana Chadema ni mazwazwa mnapinga hadi ujenzi wa bwawa la umeme ambao ni kwa ajili yenu wenyewe.

Kucha kuombaomba tu walichofanyia kazi wanaume wenzenu,
. Lema na Lisu Familia zao wanalishwa na wazungu.
 
Na mazuri yake yako wapi? Mbona jina lake linagoma kuzikwa? Mambo yake yanajieleza yenyewe? Tuwe balanced kidogo.
JPM jina lake litaendelea kukaa kaa kwa sababu kadhaa. Msipozijua hizo sababu, mtapata tabu sana
 
Aligawanya nchi kwa misingi ya ukabila, ukanda, uchama na udini na ubaguzi wa kijinsia. Serikali yake ilijaa watu wa kanda ya ziwa na 75% ya serikali yake ilijaa wasukuma watupu
Sio kweli hata kidogo.

Nchi hii hata kabla ya Hayat Rais kuwa Raisi ilikuwa na wasukuma maofisni kushinda makabila yote.

Na sababu zake zinajulikana, Ni waadilidlfu, wapo very smart, ni wajasiriamali, wasomi, itoshe ndio Kabila kubwa Tanzania. Bila kusahau walitoa mchango mkubwa sana kuwasambaratisha wakoloni!

Kwa msingi huo ,uwepo wao makazini haukuletwa na Magufuli, ila walijitokeza kwa kuwa na Pride ya kuwa na Raisi anayetoka kabila lao. Sawa tu na wa Irish wanavyofurahia President Biden kuwa raisi wa Marekani ama Baraka Obama kwa Wajaluo na wakenya na waafrika wote kwa kuwa Raisi wa Marekani.
 
Kaka kumtoa mu Africa katika umasikini na ujinga siyo kazi rahisi, kama tu hao wachina, wa Vietnam, wa Thai n.k walistruggle kweli kweli sembuse sisi? Kila uongozi hutakosa mabaya yake, nilichojifunza ni ngumu mno kuendelea kwa jamii yenye asili ya kiafrika rejea tu HAITI.
 
Mazuri ya Jiwe > Ukatili wake.

WaTz kwa tulipofika tulihitaji kuburuzwa na sio kubembelezwa.

Nyingi ulizotoa ni allegations. Fulani alisema hiki, fulani alisema kile.

Miaka mitatu Jiwe limelala, tuangalie mbele.
 
Mimi namkubali magu leo na kesho ila swala la kuumiza wafanyabiashara linahitaji uthibitisho mkubwa na kama ni kweli basi alikosea.

Nina hofu isijeikawa ni propaganda sabab kila anaesema jpm alifanya umafia kwa wafanyabiashara anaishia kusema maneno matupu.
 
Upinzani wa ukweli kabisa na pamoja ya hamasa ya wananchi juu ya demokrasia ilikufa baada ya October 2015. Mpaka leo neno demokrasia limekufa kwenye kamusi ya wananchi wengi
 
Back
Top Bottom