Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,620
- 34,820
Shamu sasa mkuu wangu unaenda kusiko hata kidogo. Nani alosema demokrasia ni freedom ya msingi ambayo kila mtu anatakiwa kuwa nayo, umeipata wapi hii na inatumika wapi. hao Wafaransa wagwiji wa demokrasia wamekataza wanawake wa kiislaam kutovaa veil na sheria imewekwa wakati wakijua fika kwamba waislaam hawana idadi tosha ya kuweza kuwakilisha haki ya wanawake wao. Na ukienda Arabuni wazungu wanalazimishwa pia kutovaa nguo zao wote wakilalamika kwa jina la demokrasia.
Huko Marekani, waislaam hawaruhusiwi kuoa wake zaidi ya mmoja na vile vile dini za kiasili zinapigwa marufuku kufanya mambo yao ya misukule na kadhalika hii demokrasia inayozungumwa ni ipi mbona sheria zote ktk kila nchi zinafuata tamaduni za wenyeji na kusisitiza kwamba Ukiwa Rome fanya kama waroma wanavyoishi, ina maana mnalazimishwa kuishi kama Waroma na sheria zote zinalenga tamaduni zao..
Hakuna nchi hata moja labda niseme hakuna utawala wowote ulofanikiwa kusimamisha malengo yake pasipo sheria ambazo zinawafunga watu wengine kutofanya majambo fulani hata kama wanayatazama kinyume. na hii inatokana na malengo waliyoweka, hivyo kama unataka kusimamisha Ujamaa lazima utumie Udikteta fulani..Hakuna nchi hata moja ilopiga kura kuchagua Ujamaa au Ubepari bali viongozi wake ndio waliamua kuchukua mwelekeo huo. nakumbuka vizuri wakati wa vita baridi, ulikuwa huwezi kuingia Marekani na gazeti la Kichina wala kirusi acha mbali kuwa na visa inayoonyesha umepitia huko. Yaani unavyoona vita ya Magaidi inavyoendeshwa leo ndivyo ilikuwa kwa mtu yeyote mwenye mtazamo wa Kijamaa na hawa ndio waliokuwa wakitangaza demokrasia muda wote kama vile demokrasia inakwenda sambamba na Ubepari..
Kwa nini tunamsifia mwalimu ma kumwona kiongozi bora! - bila shaka alikuwa na msimamo, aliweza kuongoza watu akitumia dira ya kitaifa hata kama kuna watu hawakuipenda lakini walifuata na leo hii wewe ni mmoja wa matunda ya mwalimu. Kwa hiyo kila unachoandika iwe kwa kutofurahia malezi ya mwalimu bado unashindwa kujenga hoja ya uongozi bora kwani hata ktk kupima mzazi bora hakuna Principal zaidi ya kufuata taratibu zinazopelekea kufikia malengo ulokusudia. Na hakika hii imani nma utulivu ni matunda ya mwalimu pamoja na kwamba sasa hivi mnataka kuyaharibu kwani kama ulivyosema watanzania hawakuwa wajinga..
Tanzania baada ya Uhuru ni sawa na mtoto alozaliwa, lazima atunzwe kwa malezi yenye sheria na uangalifu mkubwa kiasi kwamba hizo sheria zitaonekana ni Udikteta lakini ni muhimu zaidi kwa mtoto mdogo. Tanzania tumekua kiumri ingawa bado maisha yetu ni ya kimaskini na haiwezekani kuendelea kumlaumu mzazi wakati tumefika umri wa kujitegemea wenyewe, kufanya maamuzi kwa ajili ya maendeleo yetu na sii kuweka visingizo vya sheria zilizokuwepo wakati wa mwalimu. Na amini maneno yangu mkuu wangu kila nyumba (nchi utakayo kwenda utakuta sheria ambazo wewe hukubaliani nazo tena basi ukirudi ktk historia yao utakuta ni mbaya kuliko unavyofikiria! Kila nchi hata hiyo Marekani wamepitia kipindi cha kula sembe na kupanga foleni inategemea sababu zipi tena basi wenzetu kwa kufanya hivyo waliita ni uzalendo!
Mkandara nimetafuta thanks haipo, likes haipo nakupa hii Thank you sir!
kilichonifurahisha ni kuwa umempa mifano inayolenga kumtibu Shamu ugonjwa wa chuki aliofundishwa na kukariri bila kujua kuwa yale anayosema yanaisuta nafsi yake na yanamhukumu. Ndiyo maana nasema ni vema kuelewa kuliko kukariri.
Shamu soma between the lines alichosema mkuu Mkandara, halafu jiulize kama Nyerere hakuwa na demokrasi, je kule UN kwenye kura ya VETO kuna demokrasi! Kama Nyerere hakuwa na demokrasi je ipo Vatican au Saudia arabia?