Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

Kwanza kabisa naomba niweke wazi kuwa wengi wa wakosoaji wa viongozi wenye majina makubwa Tanzania ni watu wanaosaka umaarufu ingawaje nakubali kuwa wapo kweli wanaokosoa kwaajili ya kujenga taifa hivyo sio kila amkosoaye Nyerere ana hoja bali wengine wanataka umaarufu ingawa pia sishawishiki kuwa wakosoaji wa Nyerere wanafanya hivyo kwa maslahi ya taifa.

Kuhusu Nyerere kukosolewa hilo sina tatizo nalo ila mpaka leo hii hakuna hata kiumbe mmoja wa Tanzania hii aliyekuja na hoja mbadala ambazo zimezaa matunda nadhani wote mashahidi wa jinsi ubinafsishaji unavyoliuza taifa letu.

Mwalimu alitaja maadui watatu ujinga, maradhi na umasikini lakini miaka hamsini baada ya uhuru hakuna aliyepinga hili kwa hoja kuwa hawa ndiyo maadui wetu na mwishowe kinachonitia hofu ni jinsi wakosoaji hawa walivyoibuka kwa wingi baada ya Nyerere kufa, je walikuwa wanamwogopa? kwa maana aliacha urais tangu 1985 lakini hata 1995 wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi hawakumkosoa kiasi hiki ingawaje alishiriki kwenye kumpigia kampeni Benjamin Mkapa, hofu yangu ni kuwa tayari kuna fununu kuwa Nyerere anachafuliwa kwa makusudi tu.
Ni kweli kumezuka wimbi la wakosoaji wengi wa Nyerere siku za hivi karibuni. Mimipia naafiki kwamba Nyerere hakuwa malaika lakini bado naamini ni kiongozi aliyefanya kila awezalo kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wake. Nahisi kuna agenda ya siri ya kumchafua na inawezekana kabisa ni fitna za baadhi ya viongozi aliowaacha waliomsaliti na kusababisha chama na nchi kwenda arijojo.
 
@Nguruvi3 kwenye red - spot on! & thank you!Yapata miaka kumi na moja sasa tangu kifo cha Mwl Nyerere na zaidi ya miaka 20 tangu aondoke madarakani. Kipindi chote hiki hakuna wakati 'ubaya' wa Nyerere umeongelewa kama sasa! Na mazungumzo au studies za ubaya wa Mwl (wengine Mzee) Nyerere umekuja mara baada ya wananchi kuanza kuuliza tunaelekea wapi kama nchi? (national leadership). How coincidental? Badala ya kutoa majibu ya maswali tunayouliza sisi wananchi, tunaandikiwa essays na kupewa lectures za ubaya, u-dikteta, udini, ukabila wa 'Mzee' Nyerere.Naomba nirudie mambo niliyondika huko nyuma:1. Mwl Nyerere anaweza akawa hajaacha burungutu la cash-Hazina, lakini hakuacha mashimo!2. Mwl Nyerere anaweza akawa hakujenga shule kila kata lakini alicha nchi ikiwa na literacy rate approx. 90%3. Mwl. Nyerere anaweza akawa hakujenga mfumo 'mzuri' wa kusamehe kodi ili kuwepo na EPZ madhubuti na kuvutia uwekezaji lakini aliacha Mwatex, Kiltex, Tanganyika Packers, Tanneries, General Tyres, Machine tools, Tanzania Fertilizers company (TFC), Coffee Curing, Tanzania Railway Company, Air Tanzania (with physical aircrafts), Ranchi za Taifa, Kiwanda cha kutengeza magunia, just to mention a few!4. Mwl Nyerere anaweza asiwe na nguvu za ziada (super-man) lakini alijenga bwawa la Mtera na kipindi chake mvua za kutosha zilinyesha na kujaza hilo bwawa! maajabu!5. Mwl Nyerere anaweza akawa anavaa miwani ya giza saa zote na hivyo kutowaona wezi wote, lakini hakuna mtu aliweza kuchota fedha toka central Bank kwa maana ya BOT! EPA, Kagoda hawakufurukuta!6. Mwl Nyerere anaweza asiwe amepiga picha na ma-celebrities i.e Boys II men, lakini alikuwa anacheza bao na watanzania huku mtaani.Pia alikuwa na mawasiliano ya karibu sana na Walter Sisulu, Samora Machel, Keneth Kaunda & Sam Nujoma.7.Mwl Nyerere hakutatua matatizo yetu yote lakini alitoa elimu bure (huku akiacha rasimali zote nzima kama alivyozikuwa) ili tuwe na uwezo wa kutatua wenyewe. Kwa maneno mengine he empowered Tanzania to solve thier solve thier problem.8. Mwl. Nyerere anaweza akanunua rada ya kizamani sana- pengine ya kuona ndege ikiwa umbali wa mita 3 tu! lakini ndege za kivita toka nchi nyingine hazikutuwa kwenye viwanja vyetu na kuchukua wanyama bila rada kuwaona!9.Mwl Nyerere anaweza akawa hakutembelea wakubwa mara kwa mara na pengine ndio sababu tulikuwa tunapanga foleni ya mawe kusubiri mgao wa chakula maana wakubwa hawakuleta misaada! lakini Mwl aliwaamini matatizo ya watanzania yatataliwa na watanzania wenyewe kupita ardhi, siasa safi, na uongozi bora.10.Mwisho. Mwl. Nyerere anaweza kuwa Dikteta in the strongest terms possible lakini hakuondelewa madarakani na NATO au kwa 'mazungumzo' ya amani!Mwl Julias Kambarage Nyerere - RIP.
Duh! Mkuu ASANTE SANA kwa ulichokiandika.Kitufe cha Thanks sikioni, ila nakupa hongera kwa kufanya summary nzuri sana khs utawala wa Mwl. Mpendwa wetu, Julius Kambarage Nyerere. Kwa kweli Mkuu, umenifanya nitake kuwa kama Mizengwe Iliyoanza Kupinda kwa kulialia, sijalia ila machozi yamenirengarenga kwa jinsi watu wanavyomkosea heshima Mwl. Nyerere kwa mema na mapenzi aliyojitolea kwa Nchi hii, hadi hawa Vilaza wa sasa hivi wanapata sehemu ya kutamba ''Kisiwa cha Amani''....wanafikiri kilijiweka tu kama walivyokuta rasilimali za nchi hii alizowahifadhia vizuri Mwl??? M...a...t...a...k...o....yao!!! MOD nisamehe ni hasira tu zimenijia kwa hawa jamaa wanao mchezea Nyerere! MTOA MADA ULICHOTAKA KUFAHAMU KHS NYERERE AMBACHO HATA MTOTO WA CHEKECHEA ANAWEZA KUKIONA NA KUKIELEWA ENZI HIZO ZA NYERERE ALICHOKIFANYA NDIO HICHO HAPO JUU JAMAA KAWAKILISHA. Achana na rongorongo za hawa WanaInterejensia Uchwara wanaojidai wanafahamu mengi ya Mwl yasiyoonekana!
 
Kuna jambo linamsumbua Shamu.Anasoma article nyingi sana katika internet, jambo zuri sana. Anavideo clip zinazoelezea madhila ya ujamaa, jambo jema kabisa.Asichokijua ni kitu kinaitwa 'school of thought' yaani kuna vyuo duniani haya mambo wanayajadili kila uchao, tofauti na Shamu wanaangalia mambo kwa mtazamo mpana bila hisia wala chuki.Nilishawahi kuona mwalimu wa University ameandika thesis yake marekani kuhusu viongozi wa Afrika akam cite Nyerere na Nkrumah kama mifano.Alifaulu vema tu, si kwasababu nyingine bali aliweza kueteta hoja zake kwa mantiki.Shamu, kuna article maelfu zinaelezea Nyerere kwa ujumla wake, nenda China, yaani ujamaa wa Nyerere unaonekana kama role model.Hizo article unazosoma zimeandikwa na watu kama wewe na hazikiji haja ya kuwa proof kama hazikuwa authenticated na documented.Video clip uliyoweka ni sawa na prof Jay akiweka video yake ya 'maisha magumu' basi wewe ukaichukulia kama proof ya maisha magumu TZ.Nina uhakika zipo document nyingi sana kuhusu mwalimu lakini umeamua kuchukua zile zinazokidhi haja ya ushindani wako, ni jambo zuri. Ubaya ni pale unapozibandika na huna mifano unayoijua wewe ya kweli kuthibitisha hayo.Matokeo yake unasema vijiji vya ujamaa wamekufa watu wengi, swali ni kuwa wengi ni wangapi, je 10 si wengi, 1000 si wengi.Umeshindwa kutetea neno dictator kama definition yake unabaki kusema alitisha watu. Mkapa aliposema tutawashughulikia wapinzani alikuwa dikteta? Kikwete aliposema serikali imeishiwa na uvumilivu na wapinzani naye dikteta. Kama tutaichukulia kauli yako basi hakuna kiongozi atakayekuwa salama. Obama amesema earmark ikutua mezani kwake ata veto, naye ni dikteta.Wanaomtetea Nyerere hawatumii majarida, wanakuambia hivi: Nyerere aliacha viwanda Mwatex, Tanganyika packers, Mutex, Urafiki, UFI n.k na waweza kukupa kiwanja namba. Wanasema kaacha hospitali ABC na wanakupa kiwanja zilipo. Wanasema kaacha viwanja vya ndege KIA, JNIA n.k. Watakwambia kaacha shule za kata na si wazo la Lowasa watakupa nyaraka zake mwenyewe (sio video za watu) na shule zilipo na fedha zilizotumika kujenga.Watakuambia ameacha Mtera na ukitaka watakuletea samaki wa kutoka katika bwawa hilo.Ninachotaka kusema ni kuwa usitoe nadharia za masimulizi, toa ushahidi kama huo. Hiyo video clip inaweza kutengenezwa na P.funky akaonyesha uzuri wa Nyerere, sijui utaiamini au unataka yenye lafudhi ya kizungu.Jaribu ku connect unachokijua na reality. Usijadili mada ukiongozwa na chuki na bias, inaondoa thamani ya kitu kinaitwa intellectual.Hivi hushangai kuna waganda wanamsifia Idd Amin leo na Wazimbabwe wanamsifia Mugabe!! Na kuna wamerekani wanamchukia JF.Hivi documentary unaweza kuitumia kama ushahidi hata katika mahakama ya mwanzo!!!!!!
Mkuu Asante Sana!
 
Kuna jambo linamsumbua Shamu.
Anasoma article nyingi sana katika internet, jambo zuri sana. Anavideo clip zinazoelezea madhila ya ujamaa, jambo jema kabisa.
Asichokijua ni kitu kinaitwa 'school of thought' yaani kuna vyuo duniani haya mambo wanayajadili kila uchao, tofauti na Shamu wanaangalia mambo kwa mtazamo mpana bila hisia wala chuki.

Nilishawahi kuona mwalimu wa University ameandika thesis yake marekani kuhusu viongozi wa Afrika akam cite Nyerere na Nkrumah kama mifano.
Alifaulu vema tu, si kwasababu nyingine bali aliweza kueteta hoja zake kwa mantiki.

Shamu, kuna article maelfu zinaelezea Nyerere kwa ujumla wake, nenda China, yaani ujamaa wa Nyerere unaonekana kama role model.
Hizo article unazosoma zimeandikwa na watu kama wewe na hazikiji haja ya kuwa proof kama hazikuwa authenticated na documented.
Video clip uliyoweka ni sawa na prof Jay akiweka video yake ya 'maisha magumu' basi wewe ukaichukulia kama proof ya maisha magumu TZ.

Nina uhakika zipo document nyingi sana kuhusu mwalimu lakini umeamua kuchukua zile zinazokidhi haja ya ushindani wako, ni jambo zuri. Ubaya ni pale unapozibandika na huna mifano unayoijua wewe ya kweli kuthibitisha hayo.
Matokeo yake unasema vijiji vya ujamaa wamekufa watu wengi, swali ni kuwa wengi ni wangapi, je 10 si wengi, 1000 si wengi.

Umeshindwa kutetea neno dictator kama definition yake unabaki kusema alitisha watu. Mkapa aliposema tutawashughulikia wapinzani alikuwa dikteta? Kikwete aliposema serikali imeishiwa na uvumilivu na wapinzani naye dikteta. Kama tutaichukulia kauli yako basi hakuna kiongozi atakayekuwa salama. Obama amesema earmark ikutua mezani kwake ata veto, naye ni dikteta.

Wanaomtetea Nyerere hawatumii majarida, wanakuambia hivi: Nyerere aliacha viwanda Mwatex, Tanganyika packers, Mutex, Urafiki, UFI n.k na waweza kukupa kiwanja namba. Wanasema kaacha hospitali ABC na wanakupa kiwanja zilipo. Wanasema kaacha viwanja vya ndege KIA, JNIA n.k. Watakwambia kaacha shule za kata na si wazo la Lowasa watakupa nyaraka zake mwenyewe (sio video za watu) na shule zilipo na fedha zilizotumika kujenga.
Watakuambia ameacha Mtera na ukitaka watakuletea samaki wa kutoka katika bwawa hilo.
Ninachotaka kusema ni kuwa usitoe nadharia za masimulizi, toa ushahidi kama huo. Hiyo video clip inaweza kutengenezwa na P.funky akaonyesha uzuri wa Nyerere, sijui utaiamini au unataka yenye lafudhi ya kizungu.

Jaribu ku connect unachokijua na reality. Usijadili mada ukiongozwa na chuki na bias, inaondoa thamani ya kitu kinaitwa intellectual.
Hivi hushangai kuna waganda wanamsifia Idd Amin leo na Wazimbabwe wanamsifia Mugabe!! Na kuna wamerekani wanamchukia JF.
Hivi documentary unaweza kuitumia kama ushahidi hata katika mahakama ya mwanzo!!!!!!


Unapozungumzia "school of taught" unazungumzia schools of economic thought? Socialism vs. free enterprises? Unajua kabisa nani mshindi, I hope.
Socialism-Ujamaa system ambao Nyerere alikuwa ana practice unajua kabisa ilifeli kwa sababu ya matatizo gani. Tunachozungumzia hapa ni jinsi Nyerere alivyoshindwa kuimplemet hizo fundamentals principles za uchumi kwa makusudi kwa sababu ya Udictator wake.

Unapouliza definition ya Udictator, na kama Nyerere aliqualify kuwa Dictator; jibu Yes, Nyerere alikuwa Dictator. Mfano, na ushahidi ni Azimio la Arusha. Nyerere kwa nguvu alitumia kuwahamisha watu na kuwapeleka vijijini kwa nguvu. Tatizo kubwa lilotokea ni mauaji yaliyotokea ni kwamba WTZ walikuwa wanakufa kwa njaa, maradhi huko vijijini. Utawahamisha vipi WTZ kutoka ktk sehemu zao na kuwapeleka vijijini kulima, bila ya kuwa na mahitaji muhimu kama maji, hospital? Hayo ni mauaji. Nyerere alifanya hayo kutekeleza Azimio la Arusha. Huo ni Udictator.

Unazungumzia kuhusu video documentary. Hii video clip in MANENO yake mwenyewe Nyerere, na ANAKUBALI ALIKUWA DICTATOR. Angalia hii clip ili usikilize na umuone Nyerere mwenyewe anasema maneno hayo, please.
Films On Demand - View Playlist#
 
Nimesoma mara tano hoja zako nikijaribu kuelewa na kufikiri kwa undani juu ya ulichoandika naomba nirejee mambo kadhaa ambayo naamini yatatufanya tujadili kwa mapana zaidi. Kwanza kabisa nitatumia mfano huu rahisi wa wanafunzi wa shule ya boarding ambao wanavaa sare tufanye shati jeupe na suruali nyeusi, kwa mazingira haya iwapo mmoja wapo anatafuta umaarufu kwa njia rahisi kabisa anachofanya ni kujitahidi kuwa unique/ wa pekee mfano yeye atavaa bukta na shati la kijani, mara moja atajikuta yeye ndiyo anatazamwa sana kutokana na utofauti wake na wenzake. Halikadhalika tuchukulie mfano wa mapadre wa kanisa katoliki hawaoi ila akitokea mmoja akaoa anajenga umaarufu na anatamkwa sana na watu kutokana na kitendo chake hiko mfano Askofu Emanuel Milingo wa Lusaka Zambia, na labda niweke hoja yangu clear kwa kusema kuwa umaarufu wa hapa siyo tu wa kupongezwa bali wa ushujaa hata ikiwa anakosea mifano ni tabia ya baadhi ya wasanii wa kizazi kipya kutafuta skendo ilimradi wapambe kurasa za magazeti. Sasa kuhusu NYERERE tayari ipo wazi kuwa watanzania wengi wanamheshimu, sasakumheshimu Nyerere imekuwa common haishangazi lakini anapoibuka mtu ambaye anamkosoa hali inakuwa tofauti mfano anaweza kuonekana shujaa au jasiri huu ndiyo umaarufu ninaosema wanautafuta. Sasa kuna tatizo pia kuhusu 1995 ambapo Nyerere hakukosolewa hivi mimi siamini kuwa watu wote walimwogopa, nasema hapana hata kidogo hapa tunapaswa tujihoji mara mbili labda nitoe wazo tulifikirie kwa mantiki, mimi nadhani 2005 wakati kikwete anaingia kwa mbwembwe kuna baadhi ya waandishi na wachambuzi mahiri wenye majina makubwa walilewa mbwembwe zake nao wakamuunga mkono sasa kawaangusha sana kiasi kwamba maandiko yao yanawasuta sasa wanaamua kutumia udhaifu wa NYERERE kumjenga kikwete eti wanadai Nyerere ndiyo kaweka misingi mibovu? how? hata huyo KIKWETE si kasoma bure kutokana na sera nzuri za kufuta ujinga za Nyerere sasa mbona yeye katujengea mitambo ya kuzalisha sifuri? hizi shule za kata na bado kuna watu wanamuunga mkono? kuna nini hapa?
Asante sana Mkuu kwa ulichoandika, ongezea na hii: Ukitaka kuona kirahisi kwamba Mwl. Nyerere bado anahitajika sana ktk nchi hii, angalia baadhi ya watu wanavyosema kuhusu viongozi wanaofanya mabaya utasikia ''Mwl angekuwepo angewachalaza viboko'' kama hiyo haitoshi, utakumbuka Mrema kipindi kile alivyojipatia umaarufu hadi akawa anatembea na kitabu cha Mwl na watu walijitokeza kwa wingi kumsikilizia, hata Kikwete ukiuliza alichofanya hadi watu wakampenda ni kipi ktk uchaguzi wake wa kwanza?? Kama utakumbuka watu wengi walivutika kutokana na hisia kwamba ana dalili za kufuata hatua za Mwl, tena kulikua na tetesi zimezagaa kwamba kakataa nyumba za mgao wa bure wa serikali, wananchi wengi waliguswa na kumpa matumaini yao ya ukombozi wakiamini angerejesha heshima serikalini baada ya Mkapa kuonekana kama kawaachia Viongozi wa serikali wajimwaemwae wanavyotaka kwenye matumizi ya mali za uma. Ninacho sisitiza hapa, Watanzania bado wanamwitaji sana Nyerere hivyo hata akitokea Kiongozi mwenye dalili za kufuata nyayo zake...lazima atafanikiwa. Baadhi yao aliojivika ngozi ya Mwl kumbe ni Matapeli ni hawa kwa uchache: Mrema, Kikwete, Pinda, Sita, Mwakyembe, etc. Wako wengi!
 
Kauli zote za kumhujumu Mwalimu zitachuja na hazitawafanya watanzania wamchukie. Ni nyie wachache mliofilisika kifikra. Fikra mbovu. Upuuzi uliokubuhu. Toka lini gunia la mchanga likawa sawa kwa uzito na gunia la pumba? Acha hizo pumba. Jua namna ya kuweza kumridhisha mke uliyemwoa. Maana watu wa jamii hii ni hatari kwa taifa hili. Ni hesabu rahisi, kama huioni, ni watanzania wangapi ambao hawajui mazuri na mabaya ya mwalimu? Iweje watanzania hao hao ndio wanaomwenzi mwalimu. Bora hata wakristu wangekuwa wanamlaani kuliko waislamu maana alitaifisha shule za kikisto kuwa mali ya serikali yake ili pamoja na wengine watoto wa kiislamu nao wasome.

Na ni waislamu hao hao waliokuwa wanamchenga mwalimu na kuwaelekeza watoto wao kuzingatia elimu ya madrasa. Leo mwalimu anaonekana mtu ovyo kwa hao hao. Mfano wangekuwa wanachukulia maanani jinsi mwalimu alivokuwa akiwapigania kielimu wangekuwa mbali. Lkn wapi. Leo hii mna watu kama kiwete, magamba,nk nk waliokuwa wanasoma shule za misheni , leo huyu kiwete angekuwa anauza mabumunda. Acheni upuuzi, ushenzi, ukoram, upumbavu, ufuska wa kimawazo. Kaa na wake zenu; wawafunze: maana mama zenu walishindwa.
 
Films On Demand - View Playlist[/URL]#

Shamu, kama umeisikiliza hiyo video nakusikiliza maneno ya sekunde tano tena yanayoeleweka vizuri na bado hukuelewa!! I am so sorry for you! It's too low. Duh! Huyo amini hakuweza kusema yeye ni dikteta seuse Nyerere!! pick up one word and make your own phrase. Being a hater for nothing is not good for your health, it may complicate to serious problem in future dude!
Naomba mtu mwingine asipoteze muda kusikiliza huo 'ushahidi' maana ni tatizo la chuki la mtu mmoja.
 
Unapozungumzia "school of taught" unazungumzia schools of economic thought? Socialism vs. free enterprises?
School of thought definition:
A collection or group of people who share common characteristics of opinion or outlook of philosophy,discipline,belief, social movement,cultural movement or art movement

It doesn't mean 'economy' Shamu!
 
Nyerere alikuwa "dikteta" ndiyo. Swali ni vigezo vya nani? Maana ukweli ni kwamba asilimia 99 ya mababa na mamama waliyo viongozi (hata wale wa kifamilia) katika jamii ya Tanzania leo hii wana-qualify kuitwa "madikteta" kwa vigezo vya Wazungu. Machifu wa Kiafrika walikuwa madikteta. Na Wafalme na Ma-Emir kwenye nchi za Kimanga na Kiislamu kama Saudi Arabia, Oman, Kuwait, Brunei etc nao wote ni madikteta. JK ni dikteta pia, tena dikteta mkubwa sana.

wow! you can say it again!

ukisoma african societies unaweza kumtetea Nyerere many ways, kitu ambacho sijakiona kwa Nyerere defenders! nasoma. I will be one to my own kids...is natural!
 
Nimesoma Raia Mwema nadhani kuna watu watarudi post zangu za mwanzo, kukubaliana na mimi kuwa Nyerere atajitetea

Raia Mwema

mwandishi yuko shallow kidogo, article haijashiba, HASA SWALA LA POSHO, NA WAISLAMU HALIJASHIBA

Ni ukweli Nyerere alivunja shirikisho la east africa la waislamu, lakini ni ukweli usiopingika ni yeye pia alivunja Assemblies of God vipande viwili!! ka kutaka dini zisiwa na nguvu, na kipindi hicho Aseemblies of God church lilikuwa na nguvu na lilihisiwa kupokea misaada kutoka Marekani

waandishi issue za dini kwa Nyerere mzi-balance, sioni tatio la udini

Nyerere hakuwa mdini!! UGONJWA WAKE MKUBWA ULIKUWA ALITAKA UJAMAA na katika jitihanda hizo aliharibu hapa na pale
 
Ndugu kambota: Unajua katika kipindi chake Nyerere vijana wengi wa low income erners families na son and doughters of peasants walikuwa wanarudia darasa la saba mara kumi hata kumi na mbili kwa kiu ya kupata elimu ya secondari. Yeye nyerere hakuona hilo ni kama tatizo. Makweta mwaka 1983 alifanya tume ya kuboresha elimu na alikuja na ripoti ya kwamba tanzania tupo nyuma sana ki elimu ni lazima serikali ijenge secondari mpaka ngazi ya kata. Lakini Nyerere alikataa kwa kujibu eti wewe unataka kuimarisha paa badala ya msingi, kimya. Alipotoka madarakani alikuwa napeleka wanafunzi 900 kwa mwaka chuo kikuu lakini mkapa alipotoka madarakani alikuwa anapeleka wanafunzi 40,000.00! Mazuri ya nyerere mimi nimemtetea sana ila mabaya yake ni lazima yuyaweke wazi pia ili viongozi wetu wasije wakaiga bure. Katika utawala wake aliondoa hati miliki kwa wanamuziki hivyo kuwafanya wanamuziki wengi kufa masikini. Lakini walioona hilo pungufu wamerudisha hati miliki kwa wanamuziki wa Tanzania , ona sasa wanamuziki wetu wanavyo ishi maisha ya mboga saba mezani! Ona sasa Kikwetae alivyo boresha maisha ya vijana wetu wenye kipaji cha soka na muziki. Jiulize kwa nini watanzania hawapati kazi Kenya na Uganda ila waganda na wakenya wanapata kazi kirahisi Tanzania? Hayo yote tumtwishe nani lawama? Watu walikaa na jazba moyoni kwa kuogopa utawala wake ,ila sasa wanatoa jazaba yao.
 
lakini ni ukweli usiopingika ni yeye pia alivunja Assemblies of God vipande viwili!! ka kutaka dini zisiwa na nguvu, na kipindi hicho Aseemblies of God church lilikuwa na nguvu na lilihisiwa kupokea misaada kutoka Marekani

Naomba utufill details za hili; maana so far Nyerere kalaumiwa sana kwa kuanzisha BAKWATA na kuwagawa Waislamu. Ilikuwaje katika hili la kuivunja Assemblies of God?
 
School of thought definition:
A collection or group of people who share common characteristics of opinion or outlook of philosophy,discipline,belief, social movement,cultural movement or art movement

It doesn't mean 'economy' Shamu!


Umemiss point here. Tunapozungumzia "school of thought" lazima ujue unazungumzia kuhusu point gani. Kwa Nyerere, ni philosophy katika school of economic thought. Hiyo uliyotoa ni definition ya school of thought. Ukienda kwenye share common hapo inabidi uzungumzie philosophy ya Nyerere ambayo ni Ujamaa. Sasa unapozungumzia "school of thought" lazima uelezee ni school of thought ipi? Ujamaa, au free market economy.
 
Shamu, kama umeisikiliza hiyo video nakusikiliza maneno ya sekunde tano tena yanayoeleweka vizuri na bado hukuelewa!! I am so sorry for you! It's too low. Duh! Huyo amini hakuweza kusema yeye ni dikteta seuse Nyerere!! pick up one word and make your own phrase. Being a hater for nothing is not good for your health, it may complicate to serious problem in future dude!
Naomba mtu mwingine asipoteze muda kusikiliza huo 'ushahidi' maana ni tatizo la chuki la mtu mmoja.


Walioiweka hiyo video wanajua zaidi kile wanachozungumza. Wametumia kauli ya Nyerere kucite ushahidi wa maneno waliyotoa. Sasa wewe kama unasema Wazungu pia hawajui maana ya lugha yao, itakuwa ni ubishi wa ligi usioisha. Fuatilia vizuri hiyo video clip ili ujue ukweli.
 
Umemiss point here. Tunapozungumzia "school of thought" lazima ujue unazungumzia kuhusu point gani. Kwa Nyerere, ni philosophy katika school of economic thought. Hiyo uliyotoa ni definition ya school of thought. Ukienda kwenye share common hapo inabidi uzungumzie philosophy ya Nyerere ambayo ni Ujamaa. Sasa unapozungumzia "school of thought" lazima uelezee ni school of thought ipi? Ujamaa, au free market economy.
Nguruvi3;2178484]Asichokijua ni kitu kinaitwa 'school of thought' yaani kuna vyuo duniani haya mambo wanayajadili kila uchao, tofauti na Shamu wanaangalia mambo kwa mtazamo mpana bila hisia wala chuki
Nilisema kujadili mambo kwa ujumla bila ya hisia au chuki iwe ya kisiasa, kiuchumi au kiutamaduni. Kauli yangu ni general na haikutaja mahali kuhusu Nyerere au ujamaa. Hayo umepandikiza wewe kwa kuongozwa na chuki na hisia, nadhani unaona hatari yake. Often unakuwa off point.
 
Nadhani kukosolewa ni jambo la kawaida kwa kila mtu. Ata wale wale manabii na makuani walikuwa na makosa yao kama wanadamu.
 
nani anaweza kutuwekea tafsiri hasa ya neno DIKTETA? hapa kuna tatizo, nyerere aliongoza kwa kufuata sheria zilzokuwepo, hizo sheria ndo tuite kuwa zilikuwa katika mfumo wa kidikteta, tofauti na sheria za sasa, hizi za leo ni zakidikteta zaidi tena udikteta wa kimfumo hasa.
 
Tango73;2178666: Unajua katika kipindi chake Nyerere vijana wengi wa low income erners families na son and doughters of peasants walikuwa wanarudia darasa la saba mara kumi hata kumi na mbili kwa kiu ya kupata elimu ya secondari.
Yeye nyerere hakuona hilo ni kama tatizo. Makweta mwaka 1983 alifanya tume ya kuboresha elimu na alikuja na ripoti ya kwamba tanzania tupo nyuma sana ki elimu ni lazima serikali ijenge secondari mpaka ngazi ya kata. Lakini Nyerere alikataa kwa kujibu eti wewe unataka kuimarisha paa badala ya msingi, kimya.
Uliusoma vizuri mpango wa maendeleo wa Nyerere wa mwaka 1963? Unaweza kunithibitishia kuwa suala la sekondari za 'kata' halikuwepo? Unaamini kuwa Makweta na Lowasa ndio walioanzisha mpango huo? Je Mwalimu alikuta sekondari ngapi alipochukua nchi. Kama angeendeleza sekondari huduma za afya alizopata baba au mama yako zingetoka wapi?
Alipotoka madarakani alikuwa napeleka wanafunzi 900 kwa mwaka chuo kikuu lakini mkapa alipotoka madarakani alikuwa anapeleka wanafunzi 40,000.00!
Alipoingia madarakani alikuta wanafunzi wangapi wa chuo kikuu? Je kulikuwa na chuo kikuu Tanganyika. Hao walimu waliofundisha 40,000 ya Mkapa walizaliwa siku moja na kuwa walimu(maprofesa). Je ubora wa 40,000 unawezaje kuuweka katika mizani na 900 wa mwalimu?Mkapa alijenga vyuo vikuu vingapi?
Katika utawala wake aliondoa hati miliki kwa wanamuziki hivyo kuwafanya wanamuziki wengi kufa masikini. Lakini walioona hilo pungufu wamerudisha hati miliki kwa wanamuziki wa Tanzania , ona sasa wanamuziki wetu wanavyo ishi maisha ya mboga saba mezani! Ona sasa Kikwetae alivyo boresha maisha ya vijana wetu wenye kipaji cha soka na muziki
Na ona sasa mamilioni ya wahitimu wasivyokuwa na kazi achilia mbali mamilioni wanaoteseka bila hata kumaliza shule. Hao wa mboga saba wanaweza kuzidi 20 labda! nisaidie kwa hili
Jiulize kwa nini watanzania hawapati kazi Kenya na Uganda ila waganda na wakenya wanapata kazi kirahisi Tanzania? Hayo yote tumtwishe nani lawama? Watu walikaa na jazba moyoni kwa kuogopa utawala wake ,ila sasa wanatoa jazaba yao
Nyerere amezuia watu kupata kazi duniani? Kama huna elimu au hujui kujieleza kupata kazi Nyerere angetakiwa aje kukusaidia Interview.
 
Back
Top Bottom