Mwl Philemon
Member
- Nov 29, 2018
- 61
- 67
WANAOFAIDI KEKI YA TAIFA
Na Thadei Ole Mushi.
Kwa Mwezi anapokea Milioni 11,000,000
Kwa mwaka atapokea 132,000,000
Kwa miaka mitano atapokea Jumla 660,0000
Huu ni mshahara tu hujaweka kiinua Mgongo, bado Sitting allowance, bado Posho mbalimbali nk. Tuachane na mawaziri na manaibu waziri ambao fedha hii inaongezeka.
Mshahara huu uliingia Moja kwa moja kwenye account Ina maana labda ulikuwa na Makato ya kodi nk au Hauna hayo Makato lakini take home yake ni hiyo iliyoingia kwenye Simu.
Kazi yake kubwa Bungeni Ni kupiga makofi meza, kuitikia ndio au hapana Bungeni.
Huyu mbunge Sifa zake kitaaluma anatakiwa kujua kusoma na kuandika tu.
Njoo kwa Mwalimu anayeajiriwa na Degree moja.
Anaanza na msahahara wa TGTS D1 mshahara wake Ni 733,000 akikatwa Kodi, bima, NSSF, CWT, Loan Board, anabakiwa na shilingi 500,000 plus kwa Mwezi.
Kwa mwaka atachukua 6,000,000 huu mshara wa mwaka haujafikia mshahara wa Mbunge kwa Mwezi mmoja.
Kwa miaka mitano atachukua Milioni 30 plus huku mmbunge akichukua Milioni 660,000, 000.
Majukumu ya huyu mwalimu Sitaki kuyataja kwani ni Mengi mno.
Daktari anayeanza na Degree Moja.
Huyu analipwa 1,400,000 bila makato Kama akikatwa vikorokoro vyote anabakiwa na 900,000 kwa Mwezi.
Kwa mwaka atachukua 10,800,000 bado hajafikia mshahara wa Mbunge.
Kwa miaka mitano atachukua Milioni 54,000,000 huku Mbunge akichukua Milioni 660,000,000.
Majukumu ya Daktari unayajua hatuna haja ya kuyataja.
Ole Mushi
0712702602
Viva
Ambakisye Mwakisyala Mlima
Msemakweli Daima