MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 305
- 728
Walimu Wana maswali mengi ambayo kwa muda Mrefu CWT wakiongozwa na Kiongozi wao Japhet Maganga hawataki kujibu na wala hawaoneshi jitihaza zozote kutetea haki za walimu:
i) Mapato yatokanayo na vitega uchumi vya chama mfano: Mwalimu house na ofisi za CWT kila mkoa (rent), je vinamnufaishaje mwalimu ambaye ni mchangiaji mkuu?
ii)Kwanini C.W.T wanakusanya michango kwa wanachama kila mwezi badala ya kukusanya mara moja kwa mwaka kama vyama vingine?
iii) Kwanini kuna tofauti katika makato ya kuchangia mfuko wa C.W.T wakati huduma ni sawa? Kuna nini kinachoongezeka kwa anayekatwa zaidi na nini kinachopungua kwa anayekatwa chini? Tofauti hizo zinaletwa na mfumo wa asilimia zilizowekwa na hivyo kuweka wachangiaji katika matabaka yasiyo na tija wakati huduma ni sawa.
Mfano mwalimu mwenye TGTS I yeye kwa Mwaka CWT huchukua 674,000 kwenye mshahara wake. Huyu anasaidiwaje zaidi tofauti na mwenye TGTS E ambaye hukatwa 225,000?. CWT wanakata Fedha nyingi Sana kwa Walimu na hakuna anayejali.
Malipo ya wanayopata ni T-shirt ambazo wamekuwa wakizilalamikia kila mwaka kutokana na kukosa ubora.
iv) Je kuna uhalali gani wa kiinua mgongo cha mwanachama anayestaafu kwa uwiano na alichochangia toka uanachama wake hadi kustaafu? Ikiwa kiinua mgongo kilichopangwa na C.W.T kwa sasa ni mabati ishirini (20) au laki tatu (300,000/=)
V) Je, C.W.T kwa mwaka inakusanya kiasi cha shilingi ngapi kwa waalimu wote Tanzania kwa makato ya asilimia mbili (2%) ya kila mshahara wa mwanachama ambayo pia inatofautiana kulingana na madaraja.
Vi) C.W.T inawafanyakazi wangapi kwa kila mkoa na taifa kwa ujumla na posho zao zikoje?
Vii) Kwa kuwa waalimu wamekua wakinyanyasika na kudharaulika na kutosikilizwa katika halmashauri, Je, C.W.T inafanya nini kurudisha hadhi ya mwalimu katika ngazi ya halmashauri ilihali mambo haya yanaendelea kumgandamiza na kumnyanyasa mwalimu?
Haya ni maswali muhimu Uongozi wa Japhet Maganga umeshidwa kujibu na hivyo basi anakosa sifa za kuendelea kuwa kiongozi ndani ya chama cha walimu