Je, wabunge watakaoshinda kupitia CHADEMA 2025 watagomea mshahara wa Milioni 18 kwa mwezi?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
16,907
25,677
Salaam, Shalom!

Mimi ni MMOJA wa wananchi anayepinga wabunge kulipwa zaidi ya milioni 5 tano, Kwa mwezi kutokana na Pato kiduchu linalokusanywa maana ubunge ni KAZI ya kujitolea, ni seasonal job!!

Inakadiriwa, makusanyo ya Serikali kupitia Kodi na vyanzo vingine vya mapato havizidi bil 900 Kwa mwezi, Kwa mshahara wa wabunge 399 kulipwa ml 18 Kwa mwezi, Serikali italipa Billion takriban 7 Kwa mwezi, hao ni wabunge pekee,

Tukilipa watumishi wote wa Serikali mishahara na stahiki zao Kwa mwezi, ni dhahiri kulingana na makusanyo madogo, italazimika Serikali kukopa pesa Ili kujazia ulipaji wa watumishi wa Serikali,pesa za ndani haxitatosha kulipa mishahara.

CHADEMA ilikuwa na wabunge wengi tu tangu 2000, 2005,2010, 2015 na wakapungua Hadi mbunge mmoja 2020.

CHADEMA ilipokuwa bungeni tangu awali, hawakuwahi hata siku moja kugomea posho na mishahara ya wabunge wao bungeni zaidi ya kusema mishahara na marupurupu hayo ni kiduchu kulingana na hadhi ya mbunge.

Sasa Kwa kuwa Mwenyekiti Mbowe ameamka Kutoka usingizini na kuonyesha kukerwa na wabunge kuongezewa posho na marupurupu Yao Kutoka ml 13 Hadi ml 18 Kwa mwezi, naungana naye kupinga ubadilifu mkubwa wa Kodi za wananchi,

Na Kwa kuwa CHADEMA imetoa kauli kuwa itashiriki uchaguzi 2025, na Kwa kuwa itasimamisha wagombea ubunge Nchi nzima,

Na Kwa kuwa CHADEMA Ina uwezekano wa kushinda ubunge katika majimbo kadhaa nchini,

Je, wabunge watakaoshinda ubunge kupitia tiketi ya CHADEMA 2025 watagomea kupokea posho na marupurupu yanayofikia 18 ml Kwa mwezi?

NB: Vyama, viwekwe pembeni, walipakodi tujadili kwanza maslah ya nchi, Hasa matumizi mazuri ya Kodi zetu,

Swali: Upi Hasa uwe mshahara na marupurupu ya mbunge Kwa mwezi kulingana na makusanyo yetu kupitia Kodi?

ANGALIZO: Ni muhimu wananchi Kwa UMOJA wetu tupambanie KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote, vyama vya siasa na wanasiasa hawaaminiki.

Karibuni🙏

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Mungu ibariki CHADEMA.

Amen
 
Ukitaka kupotea msikilize Mbowe,alipokua KUB hakutuambia alikua anapokea mshahara kiasi gani na posho kiasi gani alikua akikunja zote na vyama vingine alivichinjia baharini!
CHADEMA kama chama kikuu, chama mbadala,

Itoke na kusema wazi,

Upi Hasa unatakiwa kuwa mshahara wa mbunge,

Mimi nionavyo,

Mbunge hapasi kulipwa zaidi ya ml 3,
 
Usikute kipara kipya nae ni mbunge nchi hii comedy kibao bunge limekanusha lakini halikusema wanajilipa ngapi Kisha tuione UONGO wa MH mbowe vinginevyo tutaendelea kuamini kuwa nikweli wanajilipa 18 ml
 
Usikute kipara kipya nae ni mbunge nchi hii comedy kibao bunge limekanusha lakini halikusema wanajilipa ngapi Kisha tuione UONGO wa MH mbowe vinginevyo tutaendelea kuamini kuwa nikweli wanajilipa 18 ml
HOJA hapa ni hii,

Kwa kuwa Mh Mbowe ameamka Kutoka usingizini, ameonyesha kusimama upande wa wananchi kuchukizwa na Mzigo mkubwa tunaobebeshwa wananchi,

Ni vyema CHADEMA ikaweka msimamo, mbunge alipwe pesa isiyozidi ml 3 pekee.

Na itoe msimamo wazi wa kugomea wabunge wake 2025 kulipwa ml 18 Kwa mwezi.

🙏JF, where we dare to talk openly!!
 
Kipara bila akili
Kipara kipya huyo!
20240317_220208.jpg
 
Back
Top Bottom