Wanaohusisha mkataba wa bandari na suala la udini wanafahamu kuwa ukosoaji haujaanza mwaka huu?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Tokea suala hilo liibuke, takriban miezi miwili sasa, kumetokea makundi makuu mawili.

Kundi la kwanza ni la wanounga mkono huo mkataba. Na kundi la pili ni la wanoupinga, wengi wao wakitaka baadhi ya vipengele virekebishwe.

Binafsi, nipo upande wa wanaotaka huo mkataba urekebishwe ili uweze kuwa na maslahi kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Kuuridhia ulivyo ni sawa na kuamua kujitumbukiza kwenye shimo lenye kina kirefu kisichojulikana urefu wake huku ukijua ni shimo hatari.

Wakati mjadala wa bandari ukiwa umepamba moto, kuna baadhi ya watu walioibuka na mtazamo kuwa wanoupinga wana mrengo wa kidini. Wanafikiri kuwa wanafanya hivyo kwa kuwa wawekezaji watarajiwa ni Waarabu, hisia ambazo hazina mashiko.

Sina uhakika kama wanaofikiria na kuamini hivyo wamefikia uamuzi huo kwa maamuzi yao binafsi au kuna wanasiasa waliowashawishi kufanya hivyo. Kama wameshawishiwa, watakuwa wameonesha udhaifu mkubwa mno kifikra. Na kama wayasemayo yanatoka mioyoni mwao, watakuwa wamesahau, pengine, kuwa hakuna utawala ambao haukuwahi kukosolewa.

Ukifuatilia Historia, hayati Nyerere, pamoja na "ukali" wake, bado alikosolewa na hata kutishiwa kupindiliwa zaidi ya mara moja.

Hata Mwinyi na Mkapa wdlikosolewa.

Nyerere mwenyewe, alipomwoma Mkapa anabinafsisha mashirika ya Umma, alijitokeza hadharani kulikosoa hilo.

Kuna wanaosema mkataba unapingwa kwa sababu Rais wa sasa ni Muislamu, lakini hilo haliwezi kuwa na ukweli hata kidogo. Labda wangesema mama Samia ni "mpole" kuliko mtangulizi wake wangeweza kueleweka, ay basi Mimi ningewaelewa. Kama watu siyo wasahaulifu, watakumbuka kuwa hata Magufuli alipingwa sana mpaka wengine wakatishiwa kupokonywa uraia wa Tanzania.

Labda nikumbushe baadhi ya viongozi waliowahi kuukosoa utawala wa hayati Dr. John Joseph Magufuli:.

1. Tundu Lissu
Japo alikuwa mkosoaji wa Serikali tokea utawala nafikiri, wa Mkapa, ni kipindi cha Magufuli ndiyo alionekana mkosoaji mwiba. Hata kushambuliwa kwake kwa risasi, wengine wamehusisha na misimamo yake dhidi ya Serikali ya JPM

2. Freeman Mbowe
Nini kilitokea kwenye baadhi ya biashara zake? Hazikufungwa? Kama angelikubaliana na utawala wa JPM, angepatwa na maswahibu aliyokutana nayo kipindi cha Serikali ya awamu ya tano?

3. Askofu Zakaria Kakobe
Soma JAMII FORU UZI usemao; Askofu Zakaria Kakobe: Tanzania siyo nchi ya cham kimoja. Amtaka Rais Magufuli atubu.

Nini kilichofuatia baada ya Kakobe kumtaka Magufuli katika mahubiri yake ya Disemba 2017 atubu kwa kuisigina katiba? TRA hawakumwandama? Uhamiaji hawakumsumbua?

4. Baraza la Maaskofu KATOLIKI TEC
Soma JAMII FORUM Uzi wa tarehe 09/02/2018 wenye kichwa, Waraka: Maaskofu KATOLIKI waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

5. K.K.K.T.
Soma JAMII FORUM uzi wenye kichwa, Maaskofu KKKT: Tunasikitishwa na matukio ya kupotezwa watu, kubanwa uhuru wa Mahakama, Bunge na Time ya Uchaguzi.

6. Askofu Severine Niwemugizi
Soma JAMII FORUM Uzi wa tarehe 13/12/2017 wenye kichwa kisemacho, Kuhojiwa kwa Askofu Severine Niwemugizi: Mtikisiko wa Kanisa na utawala wa Magufuli?

Wako na wengine wengi waliosimama kidete kukosoa pale walipoona Magufuli anakosea. Miongoni mwao ni pamoja na Bishop Dr. Augustine Mpemba, Bishop Dr. Benson Bagonza, Bishop Dr. Frederick Shoo, Bishop Dr. Stephen Munga, Dr. Charles Kitima, Zitto Kabwe, Bernard Membe, Mzee Kinana, Mzee Makamba, Balozi Hamisi Kagasheki, Godblesd Lema, Wenje, Mchungaji Msigwa, Askofu Emmaus Mwamakula, n.k.

Ukiangalia, Magufuli alikosolewa na Wakristo na Waislamu pia. Dini yake ya Ukristo haikumpa Kinga ya kutokukosolewa.

Alikosolewa kwa manufaa ya wengi. Ikiwa Serikali zilizotangulia zilikosolewa, ikiwemo ya awamu ya tano, kuna shida gani ya Sita ikikosolewa kwa manufaa ya wananchi? Ifahamike kuwa ukosoaji unaofanyika ubadukumwa na uzalendo.

Viongozi wa dini na wanasiasa wajihadhari wasije wakawagombanisha Watanzania kwa kutumia kivuli cha dini.

Kukosoa si kosa. Ukosoaji unaweza kuwa kichocheo cha maendeleo, endapo wahusika watakuwa na masikio sikivu. Wanasema, "Sharpen your idea on the grindstone of criticism"

Wakosoaji wa mkataba wa bandari wasituhumiwe kuwa ni wadini. Wana hoja za Msingi. Wasikilizwe kwa manufaa ya wengi.
 
Wachangiajij tu humu wanaonesha ishu sio TAIFA bali ni jinsia, dini ukanda na sio TANZANIA kiujumla.

Subiri waje upate ushuhuda wa wazi🙏🙏.
 
Back
Top Bottom