Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,341
- 51,904
KWA NINI KUUPINGA MKATABA WA BANDARI INAITWA "UDINI" LAKINI KUUNGA MKONO SIO UDINI? MSIWE WAPUMBAVU.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Wanasiasa moja ya mambo yanayowashushia heshima ni kigeugeu na unafiki wao. Wanasiasa wakisifiwa na viongozi wa dini hawasemi dini imeingizwa kwenye Siasa lakini wakikosolewe hapo utasikia Dini imeingizwa kwenye Siasa.
Wanasiasa wakitaka kuombewa na viongozi wa dini hiyo hawaiti dini imeingizwa kwenye Siasa. Wao wanataka tuu Sifa na utukufu Kutoka Kwa dini lakini wakikosolewa na kupondwa hapo wanaleta shida.
Tabia hiyo ya hovyo na kinafiki imekomaa Sana katika Nchi yetu. Na sasa tupo kwenye sakata la mkataba WA Bandari.
Viongozi wa dini waliosifia mkataba huu wao hawaambiwi kuwa ni UDINI. Lakini wanaoukosoa wanaambiwa ni udini. Hivi tutaacha lini huo upumbavu.
Kwa nini tusiangalie hoja ya msingi. Huo mkataba kama ni mbovu Kwa nini usibadilishwe? Kama kweli nia ni yakweli ya kutetea maslahi ya nchi. Kwa nini huo mkataba usiboreshwe vifungu vyenye utata?
Kujitetea kwa kujificha kwenye kichaka cha udini hakutabadili Jambo lolote.
Hekima na busara zitumike, kama kweli lengo ni kulinda maslahi ya Taifa letu na maslahi ya Watu wetu na rasilimali zetu. Mtu akipinga Jambo kama anahoja ya msingi lazima asikilizwe.
Kwanza hizo dini zenyewe tumeletewa. Pili, tupo watanzania wengi ambao hatuamini Kati hizo dini zenu za kigeni. Ingawaje tunawatambua na kuheshimu wanaoziamini. Sasa msitake kuzifanya hizo dini zenu zinaumuhimu kuliko taifa letu.
Mnapojadiliana ishu za taifa msijifanye mnajificha kwenye udini. Oooh! Yule Mkristo ndio maana anakosoa. Lakini akisifia huwezi sikia Jambo Hilo. Angalieni kinachokosolewa, je kina uhalali wa kukosolewa? Kama jibu ni ndio,basi fanyieni maboresho.
Uwe Mkristo au muislam, uwe wakabila gani, uwe Mtibeli kama Mimi au mpagani. Kwetu haina maana yoyote Ile. Tunachotaka ni kulinda maslahi ya nchi yetu na sio genge Fulani la Watu. Ni lazima tuangalie kizazi chetu kilichopo na kinachokuja.
Dini yako, au Cheo chako au mamlaka yako haina maana yoyote kwetu ikiwa unataka kuliingiza taifa katika hasara na ubinafsi wa hovyo.
Acheni upumbavu! Mtu akitoa hoja isikilizwe hoja yake na sio ni wadini gani. Kama mkataba haufai, urekebishwe. Hiyo ndio hoja. Mambo ya sijui Amani, sijui mgawanyiko, hayo yote yataletwa na watu wabinafsi na wasiotaka kusikiliza wengine.
Mgawanyiko ni muhimu ikiwa tunatofautiana. Hiyo iwekwe wazi. Kama Watu hawataki wawe wamoja, kujaribu kuwaunganisha Watu wasiofanana ndio ukosefu wa Amani, mitafaruku, unyanyasaji na ukatili. Hatuwezi lazimisha umoja wa kinyonyaji, umoja wa wengine wanafaidi wengine wanasota, huo umoja haupogo labda kinafiki.
Nisikilizeni, umoja unaletwa Kwa kuangalia wengi wanasema nini, lakini pia Kwa kuzingatia maslahi ya taifa na kizazi kijacho.
Upendo, Haki, Ukweli na Akili hiyo ndio namna ya kuwaweka Watu pamoja. Utibeli.
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam