my house.... My rules.......
Muishi na ndugu mwenye uhitaji haswa na awe na shughuli ya kufanya. Ukiishi na ndugu ambaye yupo yupo tu mtaishia kugombana.
Akifika mkae na mumeo mumpe abc utaratibu wa nyumba yenu hawezi mwambieni wazi milango iko wazi
kama ana ugonjwa unaohitaji attention au masharti fulani aseme siku ya kwanza kabisa msije kwazana mbeleni
unajua ndugu zako mwanamke ni rahisi kuwakemea na kuwapiga biti sasa ndugu wa mwenzio wanaweza wakuone una roho mbaya
pia mke jifunze kuchukulia easy baadhi ya vitu na kumbuka hao ni wapitaji tu
mwisho watendee vile wewe ungependa kutendewa
Hahahahah, hivi unajua kuwa ukiwaeleza ndugu kwamba huna hawakuamini?
Ushauri wangu ni kwamba wanandoa wakubaliane jinsi ya kusaidia ndugu wa pande zote. Sisi baada ya majaribio ya zaidi ya miaka 20, tumeshaamua kutoka hi na mtu zaidi ya mfanyakazi. Na huko mbele ya safari tunaweza kuishi peke yetu pale watoto wakishapata makazi yao.
Inconvinience za ndugu hazivumiliki.
Kuna ndugu wanakera balaa.
Anakula vitu ovyo kwenye friji, viguu anaweka juu ya sofa, haflash choo wala nini.
Mtambuzi nimekusoma kaka na michango mingine
Wengi kama unavosema tumesaidiwa na ndugu kufikia hapa tulipo
Lakini pia hatukuendelea kukaa kwao pale tulipojiweza
Tatizo apa ninkwamba kuna ndugu wanakuja hawana plan na ukiwapa hawaitaki maadam wanakula wanalala basi apo ndo wameweka kambi..hao ndio wanaoibua masimango..kabila letu hatuna utamaduni wa kupiga kambi..siku mbili tatu umeondoka tena usipoangalia wazee wako kuwaomba waje kukutembelea ni mtihan maana wana majukumu pia mengi na wanaheshim privacy..watakuja kwa lets matibabu na kutimua
Kuna makabila mengine anaenda na magarage na mahindi kilo tatu na watoto 3 anakaa miezi mitatu!
Mkuu mangatara naomba unitake radhi, mwenzio mie bado anda eitin, hata harufu ya ndoa bado sijaanza kuisikia.
Nimeyaona hayo kwa marafiki zangu ndio maana nikalileta hapa ili tuhadili tatizibhuwa ni nini??
Kwa upande wangu hata mie nimelelewa kwenye extended family, tuliishi vizuri na ndugu wa kwao baba yangu na wa kwao mama yangu. Nina imani hata mie nitakuja kuishi vizuri na ndugu wa mume mtarajiwa.
binafsi nimekulia kwenye extended family, ndugu wa pande zote mbili na watu wengine baki wasiopungua wanne, lakini wote ilikuwa sheria moja, shuleshule, kazikazi, kilizo kijijini kusaidia kulima, wote tulikuwa respect na hakuna muda wa kupiga pelepete zisizo na msingi. kwangu mimi extended family haiepukiki, kikubwa ni misingi tu, hakuna upendelleo wa ndugu wa upande wowote, wote ni sawa, na mwanamke anatakiwa ajue hilo.
Well said,kabila gani hilo unalolisemea hawaweki kambi?
ugomvi wote huu ktk familia ni chakula!!! cjui kwa nn wanawake kwao chakula wanaona dili sana!!! alafu mbaya sana ndugu wa mwanamke akija kunakuaga hakuna shida ataishi na hata atasomeshwa fresh tu lakini ngoja aje ndugu wa mwanaume tabu mtindo mmoja!!!
Kuna ukweli kuna ndugu ni visirani balaa asione kaka yake kaja na kimfuko,utasikia"anamdekeza sana mkewe,mwanamke mwenyewe sura kama kiazi kitamu sijui alikua kafumba macho"
na upande wa pili mke/mume anaweza akawa ndiye mbaya.
Changamoto ni kubwa kama kuibuka chuki na maneno ya ugomvi kati ya ndugu na mwanandoa mmojawapo.
Nilikuja kujua kumbe kweli Mdigo Mzigo shemeji yangu alipokuja kuishi nasi pamoja na mke na watoto wanne.Mie Karucee lo!
Charminglady, Loh! Pole sana. Kweli tusiangalie picha au umbo la mwili kwani Pilato hataangalia umbo bali cheti cha kuzaliwa.
Kaushauri kangu kwako Charminglady, tembea na cheti cha kuzaliwa wakuda wakikuona mwili huo ulio nao hawatasita kutupia chambo unaswe.
Pia, anda eitiini unatafuta nini humu JF? Umemaliza Homuweki yako??
Hivi huwaogopi?
Kiukweli haya Mawili yananikwaza sana hahahaha ! viguu anaweka juu ya sofa, haflash choo wala nini
Hahahahahaha, kwani vibaya kuweka miguu juu ya sofa?