Wanajeshi wamenipiga mbele ya mke wangu

Wanajeshi wamenipiga mbele ya mke wangu

Asante sana mkuu. Sasa tuchukulie ili kosa la Supu ya Mawe je twaweza kuliita Inchoate offence? Je ni kama ni hivyo je na huyu mama aliyekuwa ndani na kaona kosa linafanyika na hasimshauri mme kuwa kaacha gari barabarani tunaweza kumwita accessory maana amefacilitate kutendeka kosa?
Kwa jinsi nionavyo mie, hicho alichokifanya yeye ni kosa na ndo maana hao viumbe walimwadhibu (kimakosa), ila ninachojua mimi ni kwamba kujichukulia sheria mkononi ni kosa lingine. Kwa kosa alilolifanya, lina adhabu yake (Mfano; kulipa faini), na si kupigwa hivyo.
 
Aiseeeee hata kama ningekuwa mimi ambaye si mwanajeshi ningekuwasha makofi mawili safi kabisa, hivi unakuwa na akili gani kupaki barabarani kwenye eneo kama lile? Ulikosa sana ustaarabu na ulistahili adhabu
 
hata wao walijua hayo ndio maana wakatoa haya( usikionee huruma kiumbe usichokizaa au unyama mfanyie mwanao ili mtoto wa jirani akuogope na mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzio mfanye lolote baya utakalo) mioyo ya hao jamaa ina miongozo hyo sasa ww cheza vbaya wakunyakue
Jeshini wanafundisha kuhumiliate raia ama kuwa msaada kwa raia?
 
Aiseeeee hata kama ningekuwa mimi ambaye si mwanajeshi ningekuwasha makofi mawili safi kabisa, hivi unakuwa na akili gani kupaki barabarani kwenye eneo kama lile? Ulikosa sana ustaarabu na ulistahili adhabu

kweli zegebovu....hata km alikosea kupaki gari barabarani sio kupigwa na askari...ndo hawa hawa walipiga Traffic akifanya kazi yake mataa ubungo na ndo hawa hawa wanapiga masala eti kwa buti za bandari wanadai za jeshi na gwanda zimeandikwa US Army wkt wenzetu wanauza kwenye fancy shops...tuache kushabikia makosa ya kijinga.Pole ndugu Supu ya mawe...kupigwa mbele ya mkeo inauma lkn mama anaelewa bora ulivyokuwa mpole mana ungetaka kupambana wangekuua!
 
Hapo tumekuja njia moja japo ulitaka kuniita mwanajeshi. Makosa ya makusudi, au mtu kutenda au kukosa kutenda kitu anachotakiwa kutenda mimi sioni akili gani inaweza kutumika bila kutumia nguvu ya kijeshi. Wanajeshi sawa wanatumia nguvu wakati mwingine lakini ndivyo walivyofundishwa na sijui kama wewe Dina ulipitia JKT. Uko kipindi chetu wanasema unapata kwanza adhabu utauliza baadae kwa nini umepata adhabu. Mfano unakuta kuna mahali kuna piaka la taka lakini mtu anakula ndizi au kitu chochote anatupa kila mahali, mtu anagali kwa sababu ya haraka hasimami traffic lights au anapita mkono husio wake kisa ana haraka, au uzembe kazini mtu anatakiwa afanye kazi fulani lakini anaacha kwa visingizo vizivyo vya maana. Huoni nguvu wakati mwingine ni jibu kamili?

Imebidi nikuone mwanajeshi kwa jinsi ulivyokuwa 'unahalalisha' adhabu ya Supu ya Mawe.....

Kitu ninachosisitiza mimi, ni kuwa kuna mtu hafanyi kazi yake ndio maana unaishia huko kutamani mwanajeshi apewe rungu. Kama utawekewa pipa la taka na kuambiwa ukitupa taka chini faini isiyo na swali kiasi kadhaa...lazima wote tutaenda sawa tu. Kwa nini tutumie faini, kwa sababu wengine toka walikotokea hawakuwa na utaratibu wa kutupa uchafu kwenye chombo maalum/shimo la taka. Kwa sababu tabia hiyo hana, basi na tumbane mahali mpaka aende sawa...Lakini aliyeweka pipa la taka naye anakuja 'kujishangaza' kuwa mbona takataka ziko chini!

Tukubali tumetoka mazingira tofauti na ulezi wetu ulikuwa tofauti. Kuna wengine wako kwenye gari ukiangalia abiria ni kama familia, yaani baba, mama na watoto. Lakini angalia hayo mauchafu yanayorushwa kutokea madirishani, sio chupa za maji, makaratasi ya ice-cream na kadhalika....utakuja kumlaumu huyo mtoto baadaye? Kwa hiyo haya yote yanaanzia chini, na ambaye alipishana nayo basi tumuwekee sheria. Na aliyeweka sheria na ahakikishe anaitumia kisawasawa, na iwe kweli kweli, siyo akiletewa kimemo na 'ndugu' wa aliyeivunja ailegeze...(hapa nimetoa mfano mmoja tu wa taka)

Lakini kwa vile mtekelezaji wa sheria hii naye amekuwa goigoi, ndio maana unaona suluhisho ni utumiaji wa nguvu. Na je, utumiaji wa nguvu utaupimaje? Kuna huyu wa leo wa vibao, atakuja mwingine wa mikanda na mabuti, au lupango (ndio, nilipita) kabisa?
 
POLE SANA mkuu ina maana hukuona hata jiwe pembeni ujibu mapigo ukiwa mbalii!!?
 
Saafi saana! Hayo ndiyo matokeo ya kukosa utii bila shuruti! Unapaki ngari yako vile unataka wewe eti kwa sababu uko na bibi yako! Kwa jeshi hamna kitu kama hiyo. Discipline is their slogan. Je, waonaje wakichukua nchi watu hawa?
 
Au wanajeshi wawe wakikuta gari limeablock wanampiga dereva risasi, si hawana muda wa kupoteza?
 
hata wao walijua hayo ndio maana wakatoa haya( usikionee huruma kiumbe usichokizaa au unyama mfanyie mwanao ili mtoto wa jirani akuogope na mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzio mfanye lolote baya utakalo) mioyo ya hao jamaa ina miongozo hyo sasa ww cheza vbaya wakunyakue
so wapo kwaajili ya nini?
 
Wanajeshi wanaweza kuwa walikuwa wanaenda haraka mahali kwa shughuli nyeti za kijeshi sasa ukiweka gari inayowazuia wasiendelee na safari uraiani mnaita wrong parking lakini kijeshi ni blockage. Unawa-block wasiwahi au wasiweze kwenda kwenye operation au task yao ndio maana wanakubamiza mikofi na mingumi hawana muda wa kupoteza kuita trafic inakuwa heri mtu moja aangamie wanayemdunda mingumi na miteke kuliko taifa liangamie.

Dawa ya kuepuka zahama kama hizo watu watii sheria za barabarani.Barabara haitumiki tu kama barabara ya magari ya kiraia bali ya kivita yanayoelekea shughuli nyeti.Kutotii sheria za barabarani ni hatari kwa yule asiyetii pia.Hao kwanza ni wastaarabu wangekuwa wengine ninaowajua hata uwezo wa kuandika jamii forum usingekuwa nao.

Kuhusu huyo mama kupigwa naye ana tatizo la kutojua sheria za barabarani.Kwenye kesi ya uendeshaji mbaya n.k dereva ndiye anayewajibika siyo abiria.Huyo mama sawa ni mkewe lakini kwa kesi ya hiyo gari yeye alikuwa ni abiria tu.Mambo ya ngoswe angemwachia ngoswe mwenyewe huyo dereva aliyeegesha gari vibaya wamalizane naye kuliko naye kuanza kutia kidomodomo.

Halafu kitendo cha mkeo kumpiga kidogo kinaonyesha huyo mama ni mrembo kila mwanajeshi alimgwaya akawa akimumezea mate wakawa wanampiga kidogo huku wanammezea mate.Angekuwa ana sura kama sura ya kufa wallahi wangempiga kipigo cha mbwa mwizi.

Hakuna kitu kama hicho, sheria hazijahalalishwa kwa wanajeshi kuwadhuru raia, na kama ikitokea basi wanashitakiwa kama raia wa kawaida au kupitia mahakama yao ya jeshi..
Kuna hii kesi ya mtoto wa Fundikira, ambapo walizidisha kipigo wakaua mtoto wa watu, mbona walishitakiwa?

Wanajeshi walioua kizimbani leo

Hayo uyasemayo basi tutafika wakati hata kupishana na mwanajeshi akitembea kwa miguu issue, baiskeli balaa, bodai boda au bajaj ndio tusigune na gari ndio watufunge kabisa.
Jeshi lina maadili yake mkuu, lakini sio kulidhalilisha na kuwapiga wananchi wake badala ya kuwalinda, naomba uulize..Hakuna kabisa kwenye manual au guide zao zinaposema pigeni raia mtaani mtakapowaona wamevunja sheria za aina yoyote ile, hizo ni zana za kizamani tulipokuwa tunawaogopa viongozi, askari, mashushu na viongozi wenginepo, tusipojua hawa watu wapo kwa ajili yetu sisi, kutuhudimia na kutulinda, na kwamba ni raia kama sisi, na sio miungu..
Acha dhana potofu na zitakazoliabisha taia na kusahau kuwa hakuna wafanyakazi nchini wanaofuata maadili kama jeshi la wananchi na jeshi la polisi...
 
Duuu hakuna watu waonga kama wanajeshi hata siku moja hawawezi kupiga mtu au watu hadi wawezaidi ya mmoja!😛hoto:
 
Mara useme demu wangu mara mke wangu.

Wizi mtupu toka lini mke akawa demu
 
Kupaki gari barabarani ilihali barabara inatumiwa na watu wengine wenye shughuli usizozijua ni kukosa ustaarabu sana sana, huyu jama alistahili hiyo adhabu aliyopewa plus jela miezi mitatu, just assume kama kulikuwa na mama mjamzito anakimbizwa hosp afu we unapark barabarani na kublock wengine angeweza kusababisha hata kifo au ajali watu wengine wakapoteza maisha, huu ujinga haufai kuchekewa
 
Mmh, angeripoti tu, angeona ambavyo mripotiji na wapokea ripoti ambavyo wangekumbwa na 'shambulio la aibu'

Nafikiri Kituo cha Polisi kiko hatua chache toka eneo hilo. Ulitakiwa kutoa taarifa Polisi. Hilo ni 'shambulio la kudhuru mwili' na kwa sheria zetu linatoa adhabu nzuri tu.Hutakiwi kuwaachi hivihivi tu hata kama ulikuwa umefanya kosa.
 
Hakuna kitu kama hicho, sheria hazijahalalishwa kwa wanajeshi kuwadhuru raia, na kama ikitokea basi wanashitakiwa kama raia wa kawaida au kupitia mahakama yao ya jeshi..
Kuna hii kesi ya mtoto wa Fundikira, ambapo walizidisha kipigo wakaua mtoto wa watu, mbona walishitakiwa?

Wanajeshi walioua kizimbani leo

Hayo uyasemayo basi tutafika wakati hata kupishana na mwanajeshi akitembea kwa miguu issue, baiskeli balaa, bodai boda au bajaj ndio tusigune na gari ndio watufunge kabisa.
Jeshi lina maadili yake mkuu, lakini sio kulidhalilisha na kuwapiga wananchi wake badala ya kuwalinda, naomba uulize..Hakuna kabisa kwenye manual au guide zao zinaposema pigeni raia mtaani mtakapowaona wamevunja sheria za aina yoyote ile, hizo ni zana za kizamani tulipokuwa tunawaogopa viongozi, askari, mashushu na viongozi wenginepo, tusipojua hawa watu wapo kwa ajili yetu sisi, kutuhudimia na kutulinda, na kwamba ni raia kama sisi, na sio miungu..
Acha dhana potofu na zitakazoliabisha taia na kusahau kuwa hakuna wafanyakazi nchini wanaofuata maadili kama jeshi la wananchi na jeshi la polisi...

Hutu tusheria mnatosoma na kukariri mwaka wa kwanza vyuoni bila kutuelewa mnatisha.Tofautisha mwanajeshi akiwa kazini na akiwa hayuko kazini.Hao waliochapa mangumi huyo dereva walikuwa kazini hao wengine walioua mtoto hawakuwa kazini na huyo mtoto hakuwablock kama huyo dereva aliyeblock gari la kijeshi.

Ni kosa kuzuia askari hata polisi tu wa kawaida wasifanye kazi zao.Wanajeshi wakiwa kazini Ukiwa-block na kagari kako used toka japan wakikupa kibano usije sema hukuambiwa.Unaposema wako kwa ajili ya watu ni sawa ila hujafafanua watu wa aina gani? nikueleze tu ni kuwa wako kuwalinda raia wema watiifu kwa sheria sio wahalifu.Kama ulitaka wamlinde huyo mhalifu aliye-wablock si kazi yao kulinda mhalifu kama huyo.Kinachoweza kumlinda mtu kama huyo ni UTII WA SHERIA ZIKIWEMO ZA BARABARANI BILA SHURUTI.
 
parking ya bongo noma sana mtu anaona vibarabara vyetu vilivyo na anapaki tu barabarani .nani akusubiri sasa yaani ww ufanye makosa halafu useme umeonewa.

kwa scenario hyo, kumpiga mwenzako ni sawa? wangapi wanapaki barabarani na hawapigwi.?

kuna wakati ustaharabu unatakiwa kwa kiwango cha juu sana
 
Back
Top Bottom