baba anjela
JF-Expert Member
- Mar 17, 2013
- 431
- 310
ilikuwa juzi kwenye heka heka za kusheherekea pasaka mimi na demu wangu.
Maeneo ya barabara ya chuo kikuu (udsm) inayoelekea changanyikeni nikawa nimepaki gari pembeni kidogo na barabara siku ipaki pembeni kabisa kiukweli kwa namna fulani nikamuacha demu wangu mi nikaingia sehem (hillpark) kununua vocha pamoja kumtumia mtu hela, nilipo maliza nikawa natoka nje nikakuta lile gari kubwa kabisa la jeshi limesimama nyuma ya gari yangu halafu kuna wanajeshi wawili wapo kwenye gari yangu wanaongea na wife wakimuuliza mwenye gari yupo wapi namimi nikawa natokea akasema huyo hapo... Mamamamaaaaaaaa............... Kabla hawajaniuliza kitu walinipokea kwa makofi na vibao, walinipiga sana kwa kweli, sikuweza kupigana nao hata kidogo kwasababu kuna wengine walikuwa wametulia tu kwenye gari lao. Mke wangu alishuka kuamulia waniache hawakumpiga lakn walimsukuma akadondokea mkono wa kushoka umeteguka.
Namshukuru sana mungu, akashuka mwanajeshi mwingine sijui ni boss wao akawaambia waniache ndipo wakaondoka.
Mke wangu amewekewa muhogo mkononi huku mimi naugulia tu maumivu, nimeaibika sana mbele ya mke wangu japo naona aibu lakni najifanya uso mkavu kama ndimu.
wewe unastaİlİ kuchapwa mke wako unamwita demu kwelİ kichapo kinakufaa.