Wanajeshi wamenipiga mbele ya mke wangu

Wanajeshi wamenipiga mbele ya mke wangu

Kama ulikuwa na mkono mwepesi kwa wife ujipange!!!
Siku unanyanyua mkono anakwambia "Kama mpigaji kweli mbona hukuwapiga wanajeshi?"
 
Ilikuwa juzi kwenye heka heka za kusheherekea pasaka mimi na demu wangu.

Maeneo ya barabara ya chuo kikuu (UDSM) inayoelekea changanyikeni nikawa nimepaki gari pembeni kidogo na barabara siku ipaki pembeni kabisa kiukweli kwa namna fulani nikamuacha demu wangu mi nikaingia sehem (hillpark) kununua vocha pamoja kumtumia mtu hela, nilipo maliza nikawa natoka nje nikakuta lile gari kubwa kabisa la jeshi limesimama nyuma ya gari yangu halafu kuna wanajeshi wawili wapo kwenye gari yangu wanaongea na wife wakimuuliza mwenye gari yupo wapi namimi nikawa natokea akasema huyo hapo... mamamamaaaaaaaa............... kabla hawajaniuliza kitu walinipokea kwa makofi na vibao, walinipiga sana kwa kweli, sikuweza kupigana nao hata kidogo kwasababu kuna wengine walikuwa wametulia tu kwenye gari lao. Mke wangu alishuka kuamulia waniache hawakumpiga lakn walimsukuma akadondokea mkono wa kushoka umeteguka.

Namshukuru sana Mungu, akashuka mwanajeshi mwingine sijui ni boss wao akawaambia waniache ndipo wakaondoka.

Mke wangu amewekewa muhogo mkononi huku mimi naugulia tu maumivu, nimeaibika sana mbele ya mke wangu japo naona aibu lakni najifanya uso mkavu kama ndimu.

Tena wangekupiga zaidi maana unaonekana huna adabu kwa mkeo, huwezi kumuita jina hilo (kwenye red) mtu ambaye ni mkeo au unategemea awe mkeo.
 
Pole kaka lakini niseme tu moja kati ya watu wanaonikera sana ni watu wasiokuwa makini na uendeshaji na kutozingatia sheria. Parking zipo kwanini usitumie...
 
Wanajeshi wetu wajinga na hawana nidhamu....wanajifanya wababe lakini wakati wa mabomu ya mbagala na g/mboto walikimbia.....hakuna tofauti kabisa na interahamwe na wabakaji wa kawaida....pole ndugu yangu...nafikiri mishahara yao imechelewa sbb ya sikukuu ndio maana walikupiga wapumbavu wakubwa hao.....mungu atawalaani...

ww utakuwa kibaka kama sio teja..... Ni sawa na kumuombea laana baba yako... Usipotii sheria utagongwa vitasa tu
 
Nadhani mimi ndio ungekuwa mwisho wa maisha yangu...sababu nisingekubali lazima ningerusha ngumi kujibu!
 
Kuna msemo unasema YOU RUB MY SHOULDER I RUB YOURS.ukipaki vibaya ina maana huna ustaarabu wa kiwango cha juu jibu utakalopata ni lile lisilo la listaarabu la kiwango cha juu kama ulichokionyesha ikiwemo kukulamba makofi na mangumi.

Hao wengine unaosema wanapaki vibaya hawapigwi kuna msemo unasema bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi shauri yako.

wanajeshi hawakuonesha ustaarabu, na uzuri zaidi hawa watu inajulikana wazi hawana ustaarabu
 
hapo ulifundishwa namna ya kupaki vizui, Yaani watu kama nyie mnaniudhi? mnakuwaga na haraka zenu halafu mnahisi watu wengine hawana haraka au nyie kodi ya barabara mnayolipia ni kubwa zaidi. Asante afande kwa somo, ningemtip huyo afande alieendesha operation hapo.
 
Ilikuwa juzi kwenye heka heka za kusheherekea pasaka mimi na demu wangu.

Maeneo ya barabara ya chuo kikuu (UDSM) inayoelekea changanyikeni nikawa nimepaki gari pembeni kidogo na barabara siku ipaki pembeni kabisa kiukweli kwa namna fulani nikamuacha demu wangu mi nikaingia sehem (hillpark) kununua vocha pamoja kumtumia mtu hela, nilipo maliza nikawa natoka nje nikakuta lile gari kubwa kabisa la jeshi limesimama nyuma ya gari yangu halafu kuna wanajeshi wawili wapo kwenye gari yangu wanaongea na wife wakimuuliza mwenye gari yupo wapi namimi nikawa natokea akasema huyo hapo... mamamamaaaaaaaa............... kabla hawajaniuliza kitu walinipokea kwa makofi na vibao, walinipiga sana kwa kweli, sikuweza kupigana nao hata kidogo kwasababu kuna wengine walikuwa wametulia tu kwenye gari lao. Mke wangu alishuka kuamulia waniache hawakumpiga lakn walimsukuma akadondokea mkono wa kushoka umeteguka.

Namshukuru sana Mungu, akashuka mwanajeshi mwingine sijui ni boss wao akawaambia waniache ndipo wakaondoka.

Mke wangu amewekewa muhogo mkononi huku mimi naugulia tu maumivu, nimeaibika sana mbele ya mke wangu japo naona aibu lakni najifanya uso mkavu kama ndimu.

Wanajeshi wamezidi ubabe. Wanashindwa kwenda kusaidia waathirika wa mafuriko wanajua kupiga wananchi. Ni kukosa kazi ndo kunawasumbua. Bro ulikuwa na makosa lakini sio sababu ya wao kukupiga. Kila kosa lina adhabu yake, sidhani adhabu ya kuegesha gari vibaya ni kupigwa. Pole Kaka ningekuwa mwanasheria ningekusimamia kesi.
 
We ni haki yako kupigwa make inaonekana ulikuwa na mchepuko,headin umesema MKE afu kwenye stor mwanZon umesema n DEMU ako,,....ndo tiba hyo usirudie tena na huyo akitolewa tu hlo hogo anarudi njia kuuuu

Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨
 
Wanajeshi wamezidi ubabe. Wanashindwa kwenda kusaidia waathirika wa mafuriko wanajua kupiga wananchi. Ni kukosa kazi ndo kunawasumbua. Bro ulikuwa na makosa lakini sio sababu ya wao kukupiga. Kila kosa lina adhabu yake, sidhani adhabu ya kuegesha gari vibaya ni kupigwa. Pole Kaka ningekuwa mwanasheria ningekusimamia kesi.

Ningekupeleka kambini ukae masaa sita ungeliheshimu jeshi lako "kukosa kazi '
 
Ningekupeleka kambini ukae masaa sita ungeliheshimu jeshi lako "kukosa kazi '

Hamna lolote! Narudia tena wamekosa kazi! Naheshimu mtu anayeheshimu ubinadamu kwanza, sio ubabe wanaonyesha kwa mnyonge. Kama wewe ni mwanajeshi basi chukua hii nafasi kujua kwamba tunawaheshimu zaidi mkionyesha kujali jamii kuliko huo ubabe wenu. Kazi yenu ni kulinda wananchi sio kututwanga mangumi kila chance mnayoipata na kuendekeza ngono maana kwa hilo pia mpo tena sana.
 
acha wakupige wewe hukufuata sheria za barabarani, na huo mchepuko ndio uliokuponza kwanza inaonekana dem wako ana gundu. tena una
bahati ulipigwa na basodaa. ulistahili upate ajali. achana na michepuko.
 
Wajeda wanakiburi sana hasa wakiwa wamevaa sare zao. Kuna jamaa mmoja (kwasasa ni marehemu) alikuwa anawachapa mbaya! Wajenda walikuwa wanamwogopa sana. Dawa ya hawa wajeda ni kujifunza karate na ngumi. Ukiwa fiti hata wakiwa wa 5 hawakusumbui!!!!!
 
mdanganye kama ajipendi asubutu.
 
mdanganye kama ajipendi asubutu.

Mimi hapa, siombi initokee, ila siku ikinitokea siwezi kukaa kupigwa tu! Nitajitetea kwa namna yeyote ile. Kukaa tu kupigwa ni uoga! Kama wanataka wanimalizie hapo hapo, ila sitokubali kirahisi.
 
Hii hadithi ni ya kutunga...

Ilikuwa juzi kwenye heka heka za
kusheherekea pasaka mimi na demu wangu.
Mke wangu alishuka kuamulia waniache hawakumpiga lakn walimsukuma akadondokea mkono wa kushoka umeteguka.
 
wajeda hawana nidhamu badala ya kulinda nchi na ujangili pamoja na mipaka wao kazi kupga watu wanaopark magari vbaya. Shame on them.
 
Back
Top Bottom