Wanajeshi wamenipiga mbele ya mke wangu

Wanajeshi wamenipiga mbele ya mke wangu

Aibu iliyoje.....nafikiri sheria hairuhusu hili.....siku zote nilifikiri wanajeshi wa Tanzania wana nidhamu...ti hihihihiih...pole...tunawafahamu hawana nidhamu.
 
ndio tatzo letu watz tunakuwa wa kwanza kuvunja sheria ila tukiadhibiwa hatuishi kulalama et tunaonewa, tunanyanyaswa....
Kuna tofauti kati ya kuadhibiwa na kupigwa, huyo amepigwa kama angeadhibiwa walikuwa wana uwezo wa kumkamata na kumpeleka kunakohusika, btw wajeda ni wataalamu wa kunyoosha tabia though mbinu wanayotumia sio nzuri
 
Ulikuwa na mkeo au demu wako

All in all pole

Ingawa hao wanajeshi hawana maana kwa kioenda kujichukulia sheria mkononi
 
Aibu iliyoje.....nafikiri sheria hairuhusu hili.....siku zote nilifikiri wanajeshi wa Tanzania wana nidhamu...ti hihihihiih...pole...tunawafahamu hawana nidhamu.
Analianzisha mwenyewe alafu ikatokea ukamshinda, wanakuja kikosi kizima na kupiga yoyote yule kikubwa uwe unaishi jirani na eneo ambapo tukio limetokea, jamaa approach yao ni kama nyumbu huwa mmoja akiamua kuvuka mto hata kama kuna hatari wote wanafuata
 
Sometimes uwa najiuliza watu wengine wanafanya makosa au kwa kukusudia au ngoja nifanye kwani watanifanyaje? Mimi kama mimi sioni mtu kama huyo utamsaidiaje ili ajue kuvunja sheria kwa makusudi ni kosa kubwa sana, na kwa ufahamu wangu na niko sahihi asilimia 100 hatakaa tena arudie ilo kosa la kupark barabarani. Kila mara atakapokumbuka kipigo hicho atatafuta wapi panaruhusiwa kupark. Kwa hiyo sometimes nchi hii inahitaji watu kama wanajeshi wawatie adabu watu wote wanaofanya vitu vya hovyo hovyo bila kujua wanaleta madhara kwa wengine

Na hii ni kwa sababu watendaji wetu nao hawako serious...assuming wangekuwa makini kusimamia sheria zao unafikiri huyo bwana angepaki sehemu isiyo rasmi? Manake na yeye angejua kabisa kuwa nikiacha gari hapa waheshimiwa wanakula elfu 50 kama faini (mfano), wala hatafanya makosa ya kipuuzi. Sawa kwa case ya huyu mleta mada, naye hatarudia kwa kuwa atakuwa anakumbuka hicho kipigo...amejifunza kwa njia ngumu...

Wanajeshi mie huwatamani kwenye sehemu za kiutendaji ambako mambo unaona kabisa hayaendi na watu wanafanyia kazi kimazoea. Maamuzi yanachukua miaka huku watu wanaumia...nabaki kujisemea labda wanajeshi wangetuonyesha njia...Ila sasa hofu yangu ni hapo wanapotumia ubavu zaidi kuliko akili ndio wanaponitisha...watatupelekaje puta?
 
Asante sana mkuu. Sasa tuchukulie ili kosa la Supu ya Mawe je twaweza kuliita Inchoate offence? Je ni kama ni hivyo je na huyu mama aliyekuwa ndani na kaona kosa linafanyika na hasimshauri mme kuwa kaacha gari barabarani tunaweza kumwita accessory maana amefacilitate kutendeka kosa?
Mkuu.. kwa mimi ninavyofahamu inchoate offences ni matendo ambayo si makosa kamili ila yanakua ni hatua moja wapo ya kuelekea kwenye kosa. Crime ni unlawful act ambayo ina adhabu yake.
 
Hukunijibu swali langu. Na hata ilo la kutaka apelekwe tarifi nilipendekeza. Kwa hiyo kwa maoni yako ulitaka bado waendelee kupoteza muda waite polisi waje kumchukua na kumpeleka trafiki ili apigwe faini? Na je unajua anaweza kukataa kulipa faini na akataka apelekwe mahakamani, je akishapelekwa mahakamani basi hao wanajeshi waitwe tena kuja kutoa ushaidi muda uendelee kupotea. Mimi ingawa siyo mwanajeshi kama unavyotaka kuniita adhabu aliyopewa ni mhafaka na najua hatakaa hata siku moja kurudia kosa ilo, na mimi namwona ni mtu mzuri maana baada ya funzo amejileta kwetu kutwambia ehee!! jamani msifanye makosa kama yangu vinginevyo mtaambulia adhabu kama niliyopata na kama wewe Dina ulikuwa na nia ya kufanya hivyo hutafanya hivyo kwa kupitia somo la Supu Ya Mawe

Inaonekana mlolongo ni mrefu, lakini huo ndio utawala wa sheria.....hiyo yote unayotetea ni kuchukua sheria mkononi. Unakumbuka wanajeshi hawa hawa walimpiga trafiki muongoza magari Ubungo? Ni kutumia tu 'uanajeshi' wao, ili kuficha ubabe wao tu...
 

Mkuu,
Kwani walikuwa wanakutandika huku wamekushikilia?

Ulipaswa kuvumilia vibao viwili ama vitatu then nduki!

Pole Sana.
 
Hapo tumekuja njia moja japo ulitaka kuniita mwanajeshi. Makosa ya makusudi, au mtu kutenda au kukosa kutenda kitu anachotakiwa kutenda mimi sioni akili gani inaweza kutumika bila kutumia nguvu ya kijeshi. Wanajeshi sawa wanatumia nguvu wakati mwingine lakini ndivyo walivyofundishwa na sijui kama wewe Dina ulipitia JKT. Uko kipindi chetu wanasema unapata kwanza adhabu utauliza baadae kwa nini umepata adhabu. Mfano unakuta kuna mahali kuna piaka la taka lakini mtu anakula ndizi au kitu chochote anatupa kila mahali, mtu anagali kwa sababu ya haraka hasimami traffic lights au anapita mkono husio wake kisa ana haraka, au uzembe kazini mtu anatakiwa afanye kazi fulani lakini anaacha kwa visingizo vizivyo vya maana. Huoni nguvu wakati mwingine ni jibu kamili?

Na hii ni kwa sababu watendaji wetu nao hawako serious...assuming wangekuwa makini kusimamia sheria zao unafikiri huyo bwana angepaki sehemu isiyo rasmi? Manake na yeye angejua kabisa kuwa nikiacha gari hapa waheshimiwa wanakula elfu 50 kama faini (mfano), wala hatafanya makosa ya kipuuzi. Sawa kwa case ya huyu mleta mada, naye hatarudia kwa kuwa atakuwa anakumbuka hicho kipigo...amejifunza kwa njia ngumu...

Wanajeshi mie huwatamani kwenye sehemu za kiutendaji ambako mambo unaona kabisa hayaendi na watu wanafanyia kazi kimazoea. Maamuzi yanachukua miaka huku watu wanaumia...nabaki kujisemea labda wanajeshi wangetuonyesha njia...Ila sasa hofu yangu ni hapo wanapotumia ubavu zaidi kuliko akili ndio wanaponitisha...watatupelekaje puta?
 
pole sana!je unakumbuka numba ya gari hilo walilo kuwa nalo?...
 
Pole mkuu, lakini yote haya yaonyesha hawa wanajeshi hawajui wala kutambua wajibu wao nchini, kama wangekushikilia na kuwaita ma traffic police wakugonge faini hapo wengine tungeelewa, sasa kukupa mkong'ong'oto namna hiyo na kumsukuma mama watoto bila huruma hapo wamevunja sheria, na wewe ulitakiwa ukashtaki polisi, pamoja na kwamba kosa lako ni la barabarani wao wanajeshi wangeshitakiwa kwa kosa la kushambulia na kudhuru, bado wabongo hatujui sheria na haki zetu.
Nalaani kabisa tendo hilo li kinyama la wanajeshi wetu, kama ni kweli...

Wanajeshi wanaweza kuwa walikuwa wanaenda haraka mahali kwa shughuli nyeti za kijeshi sasa ukiweka gari inayowazuia wasiendelee na safari uraiani mnaita wrong parking lakini kijeshi ni blockage. Unawa-block wasiwahi au wasiweze kwenda kwenye operation au task yao ndio maana wanakubamiza mikofi na mingumi hawana muda wa kupoteza kuita trafic inakuwa heri mtu moja aangamie wanayemdunda mingumi na miteke kuliko taifa liangamie.

Dawa ya kuepuka zahama kama hizo watu watii sheria za barabarani.Barabara haitumiki tu kama barabara ya magari ya kiraia bali ya kivita yanayoelekea shughuli nyeti.Kutotii sheria za barabarani ni hatari kwa yule asiyetii pia.Hao kwanza ni wastaarabu wangekuwa wengine ninaowajua hata uwezo wa kuandika jamii forum usingekuwa nao.

Kuhusu huyo mama kupigwa naye ana tatizo la kutojua sheria za barabarani.Kwenye kesi ya uendeshaji mbaya n.k dereva ndiye anayewajibika siyo abiria.Huyo mama sawa ni mkewe lakini kwa kesi ya hiyo gari yeye alikuwa ni abiria tu.Mambo ya ngoswe angemwachia ngoswe mwenyewe huyo dereva aliyeegesha gari vibaya wamalizane naye kuliko naye kuanza kutia kidomodomo.

Halafu kitendo cha mkeo kumpiga kidogo kinaonyesha huyo mama ni mrembo kila mwanajeshi alimgwaya akawa akimumezea mate wakawa wanampiga kidogo huku wanammezea mate.Angekuwa ana sura kama sura ya kufa wallahi wangempiga kipigo cha mbwa mwizi.
 
ha ha haha wangekupeleka ukaogelee kwenye tope ukome kuegesha gari huku umeacha kalio la gari barabarani
 
wengi wameunga mkono kupigwa.

Kama hali ndio hii; kwa uvunjaji wowote wa sheria muhusika naapigwe papo hapo na waliomkamata, ama askari au raia, badala ya kupelekwa mahakamani.
 
Aibu yako mwenyewe unaiandikaje humu. Bora hata ili siku nyingine ujifunze kupaki gari vizuri!!!
Kwa mtu anayemheshimu mkewe hawezi mwita demu labda utuambie ulikuwa na changudoa
 
How would you feel ukiwa umefanyiwa ivi wewe?
How would you feel kitendo hichi akafanyiwa mtoto wako tena kipigo hicho kikampelekea kupata madhara makubwa ya mwili?

hata angekuwa mtoto wangu haitaniuma najua amevunja sheria ndio maana anaadhibiwa..... Jeshin kuna kauli kama hii " ukifuata maelekezo hakuna atakae kuumiza lakin usipofuata maelekezo utaumia." unajua sku hiz watu wamekuwa mabush lawyer vibaya mtu anaona kabisa kibao no parcking halafu unaenda kupak hiv unafikir ufanywe nn??
 
hata angekuwa mtoto wangu haitaniuma najua amevunja sheria ndio maana anaadhibiwa..... Jeshin kuna kauli kama hii " ukifuata maelekezo hakuna atakae kuumiza lakin usipofuata maelekezo utaumia." unajua sku hiz watu wamekuwa mabush lawyer vibaya mtu anaona kabisa kibao no parcking halafu unaenda kupak hiv unafikir ufanywe nn??
Ndo maana kuna sheria zimewekwa kwaajili ya watu wa aina hiyo.... ni rahisi sana kufikiria kuwa "haitaniuma kama ni mwanangu" kifikra ila ni ngumu sana kivitendo.
 
akafungue tu kwani wao ni nani ......wana mambo ya ajabu sana hao

jaman tambua kuwa lile ni jeshi nasio taasisi wala kampuni wala chama. Ndio maana hujawahi kusikia kuwa askari ameandamana wala askar kagoma. Nyinyi mkitaka kufuata sheria zenu milizopata vyuon lakin jeshin hakuna kitu kama hicho.... Jeshin ni amri na utekelezaji tu. Ukishindwa kutekeleza amri hapo ni kuumia tu hakuna mjadala..... Ndo maana ukiskia askari wamegoma basi nchi iko matatan..... Wale wapo kwaajili ya usalama wenu halafu unaenda kuzuia njia na gari lako ww ni nan?! Ndio maana inaitwa @TPDF (tanzania people defence force) pale ni force hakuna discussion. Ukitaka hzo nenda huko mviwata na cwt
 
Ndo maana kuna sheria zimewekwa kwaajili ya watu wa aina hiyo.... ni rahisi sana kufikiria kuwa "haitaniuma kama ni mwanangu" kifikra ila ni ngumu sana kivitendo.

hata wao walijua hayo ndio maana wakatoa haya( usikionee huruma kiumbe usichokizaa au unyama mfanyie mwanao ili mtoto wa jirani akuogope na mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzio mfanye lolote baya utakalo) mioyo ya hao jamaa ina miongozo hyo sasa ww cheza vbaya wakunyakue
 
Back
Top Bottom