Wanajeshi wamenipiga mbele ya mke wangu

Wanajeshi wamenipiga mbele ya mke wangu

Ungeandika namba za gari ufungue kesi.
 
kwa scenario hyo, kumpiga mwenzako ni sawa? wangapi wanapaki barabarani na hawapigwi.?

kuna wakati ustaharabu unatakiwa kwa kiwango cha juu sana

Kuna msemo unasema YOU RUB MY SHOULDER I RUB YOURS.ukipaki vibaya ina maana huna ustaarabu wa kiwango cha juu jibu utakalopata ni lile lisilo la listaarabu la kiwango cha juu kama ulichokionyesha ikiwemo kukulamba makofi na mangumi.

Hao wengine unaosema wanapaki vibaya hawapigwi kuna msemo unasema bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi shauri yako.
 
Wanajeshi wetu wajinga na hawana nidhamu....wanajifanya wababe lakini wakati wa mabomu ya mbagala na g/mboto walikimbia.....hakuna tofauti kabisa na interahamwe na wabakaji wa kawaida....pole ndugu yangu...nafikiri mishahara yao imechelewa sbb ya sikukuu ndio maana walikupiga wapumbavu wakubwa hao.....mungu atawalaani...
 
ni kosa kubwa mno kupaki hovyo!! pole mkuu ila next time utakuwa makini - mnaudhi sana nyie watu wenye tabia kama hizo.

Sasa huyo mkeo hata kusogeza gari hajui au ndiyo nyie mnaowabania wake zenu wasiguze magari bila sababu za msingi?
 
Ahaaaa!! Mimi huyu wa leo Supu ya Mawe katekenywa tu, wewe Dina husiombe ngozi ya ng'ombe (buti) ya jeshi ikupitie!! Nakumbuka kuna dada mmoja uko majeshini alikuwa anatembea ndivyo sivyo, wenyewe wanaita kutembea kihindi, alipigwa ngwara akiwa bado hewani alikuwa anaimba kichagga, ile kuja kutua chini mkono ulikuwa nyang'a nyang'a. Sasa wale kafinywa na tu anakimbilia JF akepigwa hasingekuwa JF. Halafu huyu mtu Supu ya Mawe simwelewi, tangu lini mke wako kipenzi ukamwita DEMU, acha ya kumwita Demu bado huyo mtu anapark barabarani, kama alivyosema mwenzetu huyo kablock njia ili wamsubiri amalize shughuli zake ndio aondoe gari wengine wapite. bora kafinywa kidogo. Tabia ya tunaziendekeza saa nyingine au kwa kiburi watanifanyaje au ujinga, na sheria ikiwa kali ama fine kubwa au kucharazwa bakora watu wataacha. Nenda Mji wa Moshi tupa salio la voucher ya simu au tema mate uone mgambo watakavyokudaka. Na hata kama hawajakuona wengine watu wa kawaida watakauona, fine ni hapo hapo 50 halfu lazima ikutoke, na kwa sababu ya ukali wa sheria ndiyo maana unaona mji wa Moshi ni msafi. Si hivyo tu hata maofisi, mtu anatoroka kazi serikalini kwa sababu hakuna anayekusumbua, hayo nenda ukayafanye sector binafsi. Utii bila shuruti ndiyo inatakiwa vinginevyo afinywe tu na hasilete kelele hapa JF kuonewa huruma

Imebidi nikuone mwanajeshi kwa jinsi ulivyokuwa 'unahalalisha' adhabu ya Supu ya Mawe.....

Kitu ninachosisitiza mimi, ni kuwa kuna mtu hafanyi kazi yake ndio maana unaishia huko kutamani mwanajeshi apewe rungu. Kama utawekewa pipa la taka na kuambiwa ukitupa taka chini faini isiyo na swali kiasi kadhaa...lazima wote tutaenda sawa tu. Kwa nini tutumie faini, kwa sababu wengine toka walikotokea hawakuwa na utaratibu wa kutupa uchafu kwenye chombo maalum/shimo la taka. Kwa sababu tabia hiyo hana, basi na tumbane mahali mpaka aende sawa...Lakini aliyeweka pipa la taka naye anakuja 'kujishangaza' kuwa mbona takataka ziko chini!

Tukubali tumetoka mazingira tofauti na ulezi wetu ulikuwa tofauti. Kuna wengine wako kwenye gari ukiangalia abiria ni kama familia, yaani baba, mama na watoto. Lakini angalia hayo mauchafu yanayorushwa kutokea madirishani, sio chupa za maji, makaratasi ya ice-cream na kadhalika....utakuja kumlaumu huyo mtoto baadaye? Kwa hiyo haya yote yanaanzia chini, na ambaye alipishana nayo basi tumuwekee sheria. Na aliyeweka sheria na ahakikishe anaitumia kisawasawa, na iwe kweli kweli, siyo akiletewa kimemo na 'ndugu' wa aliyeivunja ailegeze...(hapa nimetoa mfano mmoja tu wa taka)

Lakini kwa vile mtekelezaji wa sheria hii naye amekuwa goigoi, ndio maana unaona suluhisho ni utumiaji wa nguvu. Na je, utumiaji wa nguvu utaupimaje? Kuna huyu wa leo wa vibao, atakuja mwingine wa mikanda na mabuti, au lupango (ndio, nilipita) kabisa?
 
Una lako jambo au na wewe ulishawahi kufinywa kidogo nini??

Wanajeshi wetu wajinga na hawana nidhamu....wanajifanya wababe lakini wakati wa mabomu ya mbagala na g/mboto walikimbia.....hakuna tofauti kabisa na interahamwe na wabakaji wa kawaida....pole ndugu yangu...nafikiri mishahara yao imechelewa sbb ya sikukuu ndio maana walikupiga wapumbavu wakubwa hao.....mungu atawalaani...
 
Ahaaaa!! afungue kesi ya kupark vibaya barabarani na kutenda kosa au ile ya kupigwa kwa kutendewa kosa, kwa maana nyingine can offender open lawsuit for the punishment he got through is offense (Nameless girl tufafanulie hapo)
Ungeandika namba za gari ufungue kesi.
 
Bora hata wewe umepigwa makofi tena na wanajeshi
kuna jamaa alichapwa viboko na mlinzi wa shule mbele ya mke wake
 
yaani thread ya kupigwa na wanajeshi imeletwa MMU???au kwasababu SUPU YA MAWE kapigwa mbele ya demu wake???
 
Last edited by a moderator:
wangewapiga wajumbe walio weng nisingewashangaa pole mkuu yote n maisha
 
Hata kujitutumua basi kurusha ngumi mbili tatu!


Weeee! Dhubutuuuu! Labda mpaka muda huu ndiyo angekuwa ndiyo angekuwa anakumbuka ya kwamba Jf ipo abadike yaliyomkuta!

Chezea JWTZ wewe! Ila muda mwingi wanakuwaga wastaarabu kwa raia!

Pole sana SUPU YA MAWE
 
Last edited by a moderator:
Hao wanajeshi nao hawajakupiga vizuri,wangekua wamekukung'uta vizuri ucngekuja humu kulialia.
 
supu ya mawe: next time paki katikati ya barabara ili wakuogope. kosa ulilofanya ni kupaki nusu nusu ambayo ni ishara ya kutojiamini, ndio maana ukapewa kipondo.
 
Back
Top Bottom