Hakuna kitu kama hicho, sheria hazijahalalishwa kwa wanajeshi kuwadhuru raia, na kama ikitokea basi wanashitakiwa kama raia wa kawaida au kupitia mahakama yao ya jeshi..
Kuna hii kesi ya mtoto wa Fundikira, ambapo walizidisha kipigo wakaua mtoto wa watu, mbona walishitakiwa?
Wanajeshi walioua kizimbani leo
Hayo uyasemayo basi tutafika wakati hata kupishana na mwanajeshi akitembea kwa miguu issue, baiskeli balaa, bodai boda au bajaj ndio tusigune na gari ndio watufunge kabisa.
Jeshi lina maadili yake mkuu, lakini sio kulidhalilisha na kuwapiga wananchi wake badala ya kuwalinda, naomba uulize..Hakuna kabisa kwenye manual au guide zao zinaposema pigeni raia mtaani mtakapowaona wamevunja sheria za aina yoyote ile, hizo ni zana za kizamani tulipokuwa tunawaogopa viongozi, askari, mashushu na viongozi wenginepo, tusipojua hawa watu wapo kwa ajili yetu sisi, kutuhudimia na kutulinda, na kwamba ni raia kama sisi, na sio miungu..
Acha dhana potofu na zitakazoliabisha taia na kusahau kuwa hakuna wafanyakazi nchini wanaofuata maadili kama jeshi la wananchi na jeshi la polisi...
Kwa pale au kwa mazingira yale hakuwa na ujanja, halafu wanajeshi wako wengi asingeweza fanya lolote
Acha masikhara mkuu zile jezi ( bakabaka) wanacheza kareti moja inaitwa combat karet kazi ni kuvunja na kuua ashukuru walimpiga kistaarabu wange apply hiyo na hisi saiv tungeongea mengine!!!!!!!!
Ilikuwa juzi kwenye heka heka za kusheherekea pasaka mimi na demu wangu.
Maeneo ya barabara ya chuo kikuu (UDSM) inayoelekea changanyikeni nikawa nimepaki gari pembeni kidogo na barabara siku ipaki pembeni kabisa kiukweli kwa namna fulani nikamuacha demu wangu mi nikaingia sehem (hillpark) kununua vocha pamoja kumtumia mtu hela, nilipo maliza nikawa natoka nje nikakuta lile gari kubwa kabisa la jeshi limesimama nyuma ya gari yangu halafu kuna wanajeshi wawili wapo kwenye gari yangu wanaongea na wife wakimuuliza mwenye gari yupo wapi namimi nikawa natokea akasema huyo hapo... mamamamaaaaaaaa............... kabla hawajaniuliza kitu walinipokea kwa makofi na vibao, walinipiga sana kwa kweli, sikuweza kupigana nao hata kidogo kwasababu kuna wengine walikuwa wametulia tu kwenye gari lao. Mke wangu alishuka kuamulia waniache hawakumpiga lakn walimsukuma akadondokea mkono wa kushoka umeteguka.
Namshukuru sana Mungu, akashuka mwanajeshi mwingine sijui ni boss wao akawaambia waniache ndipo wakaondoka.
Mke wangu amewekewa muhogo mkononi huku mimi naugulia tu maumivu, nimeaibika sana mbele ya mke wangu japo naona aibu lakni najifanya uso mkavu kama ndimu.
Akili kidogo nguvu nyingi!
Nina uhakika baada ya hapo ulisepa maana wakikumata ukipelekwa kambini kwao ndio utajua kama DCM ni basi au kilakishaliMm nimewachapa watano hao wanajeshi wenu
Acha matusi mkuu,,,mi jamaa nawapenda sana. Hua wanafanya ubabe wao kwa wanaojifanya wababe pia, ila ukitii wala hawana shida na wewe. Mungu ibariki JWTZ