Wanajeshi wamenipiga mbele ya mke wangu

Wanajeshi wamenipiga mbele ya mke wangu

Hata kama una kosa hakuna anayeweza muhukumu mwenzake kwa kipigo wakati kuna mahakama.

Siku nyingine tembea na silaha hata kama ni manati..kwani silaha haijui kama huyu ni mwanajeshi..au la...
 
Ilikuwa juzi kwenye heka heka za kusheherekea pasaka mimi na demu wangu.

Maeneo ya barabara ya chuo kikuu (UDSM) inayoelekea changanyikeni nikawa nimepaki gari pembeni kidogo na barabara siku ipaki pembeni kabisa kiukweli kwa namna fulani nikamuacha demu wangu mi nikaingia sehem (hillpark) kununua vocha pamoja kumtumia mtu hela, nilipo maliza nikawa natoka nje nikakuta lile gari kubwa kabisa la jeshi limesimama nyuma ya gari yangu halafu kuna wanajeshi wawili wapo kwenye gari yangu wanaongea na wife wakimuuliza mwenye gari yupo wapi namimi nikawa natokea akasema huyo hapo... mamamamaaaaaaaa............... kabla hawajaniuliza kitu walinipokea kwa makofi na vibao, walinipiga sana kwa kweli, sikuweza kupigana nao hata kidogo kwasababu kuna wengine walikuwa wametulia tu kwenye gari lao. Mke wangu alishuka kuamulia waniache hawakumpiga lakn walimsukuma akadondokea mkono wa kushoka umeteguka.

Namshukuru sana Mungu, akashuka mwanajeshi mwingine sijui ni boss wao akawaambia waniache ndipo wakaondoka.

Mke wangu amewekewa muhogo mkononi huku mimi naugulia tu maumivu, nimeaibika sana mbele ya mke wangu japo naona aibu lakni najifanya uso mkavu kama ndimu.

Hahahaa, sasa umeambiwa jf ndiyo kituo cha polisi?
Hapo mkuu ulikuwa na makosa kupaki barabarani, huwezi jua jamaa walikuwa na mission gani na uliwachelewesha kiasi gani na kusababisha hasara au vifo vya watu kiasi gani, wale kila saa wako vitani kaka. Hata kama ni wewe pata picha mjingamjinga fulani ameziba barabara eti kaenda kununua vocha....dafuq!!! Pamoja na kwamba hawakufuata sheria lakini shukuru wamekupiga ina maana wamekusamehe tu, wakikupeleka mbele ya sheria mkuu ungeumia vibaya mno.
 
Mwanzo umesema ulikuwa na demu wako, halafu mwisho unasema walimkuta wife kwenye gari, duh!
wife+demu=?
 
hawa si ndo wanafanya ukabaji huko daraja la kawe..?! wamekuwa National parking systems sasa..., hawajakupiga faini kweli...
 
Ilikuwa juzi kwenye heka heka za kusheherekea pasaka mimi na demu wangu.

Maeneo ya barabara ya chuo kikuu (UDSM) inayoelekea changanyikeni nikawa nimepaki gari pembeni kidogo na barabara siku ipaki pembeni kabisa kiukweli kwa namna fulani nikamuacha demu wangu mi nikaingia sehem (hillpark) kununua vocha pamoja kumtumia mtu hela, nilipo maliza nikawa natoka nje nikakuta lile gari kubwa kabisa la jeshi limesimama nyuma ya gari yangu halafu kuna wanajeshi wawili wapo kwenye gari yangu wanaongea na wife wakimuuliza mwenye gari yupo wapi namimi nikawa natokea akasema huyo hapo... mamamamaaaaaaaa............... kabla hawajaniuliza kitu walinipokea kwa makofi na vibao, walinipiga sana kwa kweli, sikuweza kupigana nao hata kidogo kwasababu kuna wengine walikuwa wametulia tu kwenye gari lao. Mke wangu alishuka kuamulia waniache hawakumpiga lakn walimsukuma akadondokea mkono wa kushoka umeteguka.

Namshukuru sana Mungu, akashuka mwanajeshi mwingine sijui ni boss wao akawaambia waniache ndipo wakaondoka.

Mke wangu amewekewa muhogo mkononi huku mimi naugulia tu maumivu, nimeaibika sana mbele ya mke wangu japo naona aibu lakni najifanya uso mkavu kama ndimu.

Kama una namba ya gari lao nenda kashitaki kwa mnadhimu mkuu wa Jeshi pale Upanga HQs. Kuna kisa kama hiki kilitokea, na mnadhimu alichukua hatua.
 
Hao wanajeshi walikua wa nchi gani?
Zanzibar?
Tanganyika?
Shirikisho?
 
Gari lingekua na bendera ya ccm wasinge kufanya kitu
 
Laaaah
huwa tunapiga hata makelele ya kuwatisha
mfn
mimi nilikuwa na mpenzi wangu,askar wakaja kwenye pikipiki yangu kuikagua
niliwaka huku nikiwatisha napiga simu kwa bosi wao,mbona walifyata
 
Itabidi kujifunza karate maana hao wanasifa sana halafu hawana busara hata chembe

Acha masikhara mkuu zile jezi ( bakabaka) wanacheza kareti moja inaitwa combat karet kazi ni kuvunja na kuua ashukuru walimpiga kistaarabu wange apply hiyo na hisi saiv tungeongea mengine!!!!!!!!
 
ndio tatzo letu watz tunakuwa wa kwanza kuvunja sheria ila tukiadhibiwa hatuishi kulalama et tunaonewa, tunanyanyaswa....

Huwezi kulazimisha utii wa sheria kwa kuvunja sheria zingine , kilichofanywa na wanajeshi hawa ni utovu wa nidhamu ambao unatakiwa kukemewa na kila mtu
Wangemkamata wakampeleka polisi ili polisi wafanye kazi yao ningewaona wana akili kuliko uhayawani walioufanya.
 
pole sana,ila hakika,hutorudia tena,kuegesha gari kimakosa(ukupigao ndio ukufunzao.)
 
Ilikuwa juzi kwenye heka heka za kusheherekea pasaka mimi na demu wangu.

Maeneo ya barabara ya chuo kikuu (UDSM) inayoelekea changanyikeni nikawa nimepaki gari pembeni kidogo na barabara siku ipaki pembeni kabisa kiukweli kwa namna fulani nikamuacha demu wangu mi nikaingia sehem (hillpark) kununua vocha pamoja kumtumia mtu hela, nilipo maliza nikawa natoka nje nikakuta lile gari kubwa kabisa la jeshi limesimama nyuma ya gari yangu halafu kuna wanajeshi wawili wapo kwenye gari yangu wanaongea na wife wakimuuliza mwenye gari yupo wapi namimi nikawa natokea akasema huyo hapo... mamamamaaaaaaaa............... kabla hawajaniuliza kitu walinipokea kwa makofi na vibao, walinipiga sana kwa kweli, sikuweza kupigana nao hata kidogo kwasababu kuna wengine walikuwa wametulia tu kwenye gari lao. Mke wangu alishuka kuamulia waniache hawakumpiga lakn walimsukuma akadondokea mkono wa kushoka umeteguka.

Namshukuru sana Mungu, akashuka mwanajeshi mwingine sijui ni boss wao akawaambia waniache ndipo wakaondoka.

Mke wangu amewekewa muhogo mkononi huku mimi naugulia tu maumivu, nimeaibika sana mbele ya mke wangu japo naona aibu lakni najifanya uso mkavu kama ndimu.

1) Ni mkeo au "demu" wako.?

2) Ulipaki pembeni kidogo au hukipaki pembeni kabisa?

Kwa jinsi ulivyoandika, unaonesha wewe ni mapepe na nnauhakika uliipaki gari barabarani na ukawa unazuwia njia. Na kichapo ulichokula kilikuwa halali yako. Nyie ndiyo madereva wenye dharau njiani, mnapaki gari kokote na hamjali wala kujuwa kuwa mnasababisha kero kwa madereva wengine.

Nawapa pongezi wanajeshi, na nnauhakika hutarudia tena.

Na hii iwe fundisho kwako na madereva wengine wabovu kama wewe.

Hongera Jeshi, muwashughulikie hawa madereva wabovu.
 
nimecheka kidogo mkuu SUPU YA MAWE ila sio kwa nia mbaya

Poleni sana

Na huyo ni demu wako au mkeo? Sahihisha post yako maana umetumia maneno yote mawili. After all "demu" sio neno zuri kumuita umpendaye
 
Last edited by a moderator:
Mkuu pole sana kwa kuchukua kichapo wakati mwingine vichapo vinasaidia kurekebisha tabia za kipuuzi.
Madereva wengi wanapuuza sana suala la kupaki magari yao kwa utaratibu unaofaa.
 
Back
Top Bottom