Wanajeshi wamenipiga mbele ya mke wangu

Wanajeshi wamenipiga mbele ya mke wangu

Ilikuwa juzi kwenye heka heka za kusheherekea pasaka mimi na demu wangu.

Maeneo ya barabara ya chuo kikuu (UDSM) inayoelekea changanyikeni nikawa nimepaki gari pembeni kidogo na barabara siku ipaki pembeni kabisa kiukweli kwa namna fulani nikamuacha demu wangu mi nikaingia sehem (hillpark) kununua vocha pamoja kumtumia mtu hela, nilipo maliza nikawa natoka nje nikakuta lile gari kubwa kabisa la jeshi limesimama nyuma ya gari yangu halafu kuna wanajeshi wawili wapo kwenye gari yangu wanaongea na wife wakimuuliza mwenye gari yupo wapi namimi nikawa natokea akasema huyo hapo... mamamamaaaaaaaa............... kabla hawajaniuliza kitu walinipokea kwa makofi na vibao, walinipiga sana kwa kweli, sikuweza kupigana nao hata kidogo kwasababu kuna wengine walikuwa wametulia tu kwenye gari lao. Mke wangu alishuka kuamulia waniache hawakumpiga lakn walimsukuma akadondokea mkono wa kushoka umeteguka.

Namshukuru sana Mungu, akashuka mwanajeshi mwingine sijui ni boss wao akawaambia waniache ndipo wakaondoka.

Mke wangu amewekewa muhogo mkononi huku mimi naugulia tu maumivu, nimeaibika sana mbele ya mke wangu japo naona aibu lakni najifanya uso mkavu kama ndimu.


hawana akili hao leo asubuhi gari yao namba 3067JW05 imewagonga watoto wawili na kuwaua hapohapo, kisa gari yajeshi iliamua kutumia upande wa pili wa gari zinazokwenda tegeta wakati wao wakiwa na bos wao mwenye cheo cha col, walikuwa wanaenda town wakijifanya wanahraka nyuma kukiwa na wapumbavu wengine wakiwafuata. ninazo picha sijaua jinsi ya kuzipost
 
Pole. Nalijua eneo ulilotaja. Ki ukweli walichokufanyia mbele ya mkeo ni sawa tu. Mbele ya hiyo business centre yaani barabarani hakuna parking kabisa labda gari uiweke barabarani. Chuo waliweka designated parking ambayo ni nzuri tu ipo kushoto mwa hapo na opposite na CRDB/UDBS. Wajeuri huwa mnaweka gari barabarani kwa kisingizio nachukua vocha mara moja kumbe unapimiwa unga,mchele na sukari na pengine ku gonga vyombo! Kumbuka hiyo ni njia inayosaidia watu wa Kimara,Mbezi,Goba,Tegeta nk. Na sometimes wrong parking eneo hilo huwa inasababisha foleni kubwa.Pia ni njia kuu ya vijana wetu wa kambi ya Changanyikeni hivyo they will never torelate foolishness. Waambie na wenzio wenye tabia hiyo!
 
IMG-20140422-00408.jpg

Hiki ndiyo kilichotokea, watoto wawili wamegongwa hapo Tanki bovu na kufariki angalia direction ya gari. haya ni matumizi mabaya ya bara bara na wanajeshi tunaowavalisha na kuwalisha bure ndiyo chanzo cha ubabe, ukiwauliza wanajifanya wanajua ngumi kuliko wenngine na hasa wakiwa wakiwa zaidi ya mmoja ndiyo ujinga unaongezeka. hebu kuweni mfano kwenye jamii. namba ya gari ni 3067JW05
 
ndio tatzo letu watz tunakuwa wa kwanza kuvunja sheria ila tukiadhibiwa hatuishi kulalama et tunaonewa, tunanyanyaswa....

Hii ndio adhabu iliyothibitishwa na sheria? Humjui mtu ana matatizo gani, uanze kumpiga tu, hata wanyama hawapaswi kutendwa hivyo, sembuse binadamu!!!!
Wanajeshi wawe wanatumia akili badala ya nguvu...
 
Thupu ya mawe unapigwa mbele ya wife?kuna umuhimu wa kujifunza tai ch na urevenge kwa thoja yeyote utayekutana naye njiani.Au thio mthera wangu?
 
Mkuu pole kwa kipigo.
Naamini hutapark gari kizembe tena...
 
Mkuu ningekuwa mie yani lile kofi moja tu ningefyatuka nduki wale jamaa hawana maana hata wakiua hamna wa kuwaulza!
 
parking ya bongo noma sana mtu anaona vibarabara vyetu vilivyo na anapaki tu barabarani .nani akusubiri sasa yaani ww ufanye makosa halafu useme umeonewa.
Walikuwa wengi mbona yeye alijitutumua kumtetea, mke alionesha ujasiri kuliko hicho kidume
 
Pole mkuu, lakini yote haya yaonyesha hawa wanajeshi hawajui wala kutambua wajibu wao nchini, kama wangekushikilia na kuwaita ma traffic police wakugonge faini hapo wengine tungeelewa, sasa kukupa mkong'ong'oto namna hiyo na kumsukuma mama watoto bila huruma hapo wamevunja sheria, na wewe ulitakiwa ukashtaki polisi, pamoja na kwamba kosa lako ni la barabarani wao wanajeshi wangeshitakiwa kwa kosa la kushambulia na kudhuru, bado wabongo hatujui sheria na haki zetu.
Nalaani kabisa tendo hilo li kinyama la wanajeshi wetu, kama ni kweli...
 
Kawaida m2 hujifunza kutokana na makosa,ila wao wamegeuza nakuwa "mtu hujifunza kutokana na kipigo" pole mkuu.
 
Pole sana.
Kama kwenye movie za zamani vile...ukalipize kisasi kambini kwao...nyata huku ukijibanza hadi kambini,kisha anza kutoa kichapo heavy.Mbona wanapigika tu wale.

*starring siku zote huwa na demu,na huwa mwisho wa siku anashinda...nasubiri kwa hamu episode ya series yako.
 
View attachment 152987

Hiki ndiyo kilichotokea, watoto wawili wamegongwa hapo Tanki bovu na kufariki angalia direction ya gari. haya ni matumizi mabaya ya bara bara na wanajeshi tunaowavalisha na kuwalisha bure ndiyo chanzo cha ubabe, ukiwauliza wanajifanya wanajua ngumi kuliko wenngine na hasa wakiwa wakiwa zaidi ya mmoja ndiyo ujinga unaongezeka. hebu kuweni mfano kwenye jamii. namba ya gari ni 3067JW05

attachment.php
 
Back
Top Bottom