Naomba ujumbe huu tuwafikishie wengine juu ya hujuma hii watufanyiayo mitanado ya simu
Kila Mtanzania anayepiga simu mtandao wowote, asilimia kumi (10%) ya huo
muda wa maongezi zinakatwa, fedha hizo zinaenda kuchangia Kampeni za CCM. Kudhihirisha
hili, mtu yeyote mwenye simu, chukua simu yako, nenda kwenye sehumu ya
kuandika ujumbe mfupi (SMS); kisha andika neno "HAPANA" na tuma ujumbe huo
kwenda namba "15016." Utapokea ujumbe huu "Asante kwa ujumbe wako, utatolewa
kwenye huduma hii ya changia ushinde na CCM."Hii ni hujuma tunayofanyiwa
watumiaji wa huduma za mawasiliano bila ridhaa yetu au kujulishwa hivyo na
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Kesho yake, October 14,2010, nadhani baada ya wahusika kushtukia idadi ya
watu watu wanaojiondoa kwenye huduma hii; na nilipokuwa najiondoa kwenye
hujuma hii kwa kutumia lini yangu ya Zain & Zantel, nilipokea ujumbe huu
"Asante kwa ujumbe wako kama umeshiriki Changia ushinde utaondolewa kwenye
huduma. Kumbuka hakuna malipo kutumia mtandao wa mawasiliano wa CCM." Ujumbe
huu wa pili nauona kama ujanja wa kuwapumbaza watu kwani mantiki yake
imevurugwa kwa maksudi. Hata hivyo cha msingi hapa tusiangalie nyuma,
tumeshahujumiwa, dawa ni kujiondoa maana kujiondoa kwenye hujuma hii ni
bure. Mjulishe ndugu na rafiki yako tafadhali.
Habari ndo hiyo